Baada ya Sauti ya Wakatoliki kunena kiume jana, kuanzia leo wasianze Kutishwa na Wanasiasa kwani yatawakuta zaidi ya Corona

Tunajua Tanzania yako Madhehebu mengi ya Kiimani ila tusidanganyane wala tusizunguke kusema ukweli kwamba tokea Uhuru wa nchi hii hadi sasa Kanisa Katoliki lina nguvu ya 75% ndani ya Watanzania wengi na hata katika Kuamua Tawala (za Kisiasa) katika nchi hii. Wenye Akili najua kwa hili mtakuwa mmenielewa mno tu.

Asije kutokea Mwanasiasa yoyote kwasababu tu ya Ushamba na Ujuha wake au chuki zake na Ukatili wake wa Asili akathubutu kutaka ama Kuwatisha au Kulipiza Kisasi Kanisa Katoliki na Msimamo wao walioutoa jana au watakaoendelea kuutoa.

Ukiwagusa tu pabaya Kanisa Katoliki jua umeigusa Nguvu moja Kubwa yenye Mamlaka ya Kiimani si tu Tanzania bali hata duniani (ulimwenguni) kote. Kanisa Katoliki likiamua nchi isitawalike au Mtawala aone Ikulu ni pamoto au Kumjengea Chuki kwa Watawaliwa wanaweza na Kufanikiwa. Mifano ya hii iko mingi kwa mfuatiliaji mzuri wa Masuala Mtambuka yanayoendelea au yaliyotokea huko nyuma.

Nimelisema hili mapema hivi baada ya Kudokezwa kuwa yupo Mwanasiasa Mmoja amechukizwa na Msimamo wao Thabiti wa jana hivyo anataka Kuwakomoa katika Taasisi zao za Elimu na Tina nchini hasa kupitia Misamaha yao ya Kodi au Fursa fulani fulani. Nawaonya (Namuonya) huyo (huyu) Mwanasiasa kuwa All - Rounder nasema asije Kuthubutu kwani ataharibu zaidi kuliko Kujenga. Akubali ukweli na ashirikiane nao kiukaribu kwa Maslahi mema na Ustawi wa Tanzania yetu hii.

Heko sana Kanisa Katoliki Tanzania.
Washaanza kutishwa,ila hakuna mtu hapa tanzania ana ubavu dhidi ya wakatoliki wataufyata mkia
 
Y
Mbona wa Ngara aliweka lockdown waumin wake uliona kuna wakumzuia,
Yan achukue tahadhari waumini wake wasidhurike halafu azuiwe!!! Embu awaambie waumini wake wasivae barakoa uone watakachomfanyia..nyie mnafikiri kila mtu na kila Taasisi ni wa kuwafanyia huo ubabe wenu? Au mnafikiri Kanisa katoliki Ni hao wasanii kina gwajima na kakobe?!!!
 
Kanisa Katoliki ni habari nyingine hiyo. kama Vatican ni nchi ndani ya nchi ya Italia hilo linatosha kuwa somo.

advataizi moja wapo kuwa Katoliki haliogopi chochote ni hii hapa pichani.

Screenshot_20210305-144011_BBC News.jpg
 
Back
Top Bottom