Baada ya reforms ya Elimu, tuhamishie reforms kwenye Ajira

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Mimi ni mmoja kati ya watu tuliovutiwa sana na hotuba ya Raisi Magufuli aliyoitoa pale UDSM ambapo naweza kusema kwamba alitangaza blue print ya Serikali yake ya jinsi anavyotaka kuiboresha Elimu yetu, na kilichonivutia ni uamuzi wa kwamba Chuo Kikuu kibakie kwa wale waliofika kidato cha Sita na kufaulu tu na hawa wengine waende kwenye vyuo vyao stahiki vinavyotoa Diploma na hivi Vyuo tunavyo kama CBE, NIT, Dar tech, n.k!

Sasa kinachofatwa ilipaswa pia kuwe reforms kwenye ajira ili ajira ziendane na aina ya Elimu mtu anayopata kwa mfano haingii akilini Bank teller awe Shahada ya Chuo Kikuu wkt hiyo ni kazi ambayo inaweza kufanywa na mhitimu wa Diploma, au mtu anayekaa dirishani TRA ambaye ndiyo mtu wa kwanza anyekutana mteja awe na Shahada ya Chuo Kikuu kazi hiyo inaweza kufanywa na mtu wa Diploma tu, mtu anayewasha na kuzima mitambo Tanesco hahitaji awe na degree ya electrical engineering hiyo kazi inaweza kufanywa na mtu mwenye Diploma ya technical colleges zetu, n.k hii reform ni muhimu na pia hivi vyuo vyote ambavyo leo badala ya kutoa Diploma wamehamia kwenye Bachelors na Masters pia vilazimishwe na vibakie kutoa diploma tu na hapa naongelea Vyuo kama Dar tech, Mbeya tech, NIT, CBE n. ili kazi ya kutoa degree ibakie kwa Chuo kilichosajiliwa kama Chuo Kikuu tu na si vinginevyo!
 
Jana, kwa msaada wa King snr nilipata Course Structure ya Special Diploma ( Mathematics & Chemistry) . Niliiomba ili niitathimini na kujiridhisha ikiwa hii program itasaidia. Course Structure niliyopatiwa ni ya First Year.

Baada ya kuipitia, hivi sasa naweza kuongea kwa kujiamini kwamba kwa sasa serikali haina mbadala labda kama inafikiria kuajiri walimu wa sayansi kutoka nje ya Afrika au ina mpango wa kufuta over 75% ya mikondo ya sayansi nchini!

13c1170bbdb5e0d89d8049c799c1ab6e.jpg

Kwanza tukumbuke jambo moja.
Wanafunzi wanaoji-commit sayansi ni wachache sana! O Level nilisoma one of the best private schools in town enzi zile... tulikuwa na kila kitu needed for science students! However, kati ya mikondo 6 iliyokuwapo ni 2 tu ndo ilikuwa ya sayansi huo mmoja wala haukuwa reliable.

Hiyo ilikuwa ni shule yenye kila kitu including enough teachers but still at least 70% ya wanafunzi waliikacha sayansi! What about shule zetu zile ambazo hata mwalimu wa historia hakuna?!

A Level nilienda Tambaza! Enzi hizo Tambaza walikuwa wanachukua wanafunzi WENGI SANA wa A Level! Lakini pamoja na yote hayo; PCM tulikuwa mkondo mmoja TU na tulikuwa hatufiki 50! Kipindi cha Maths tulikuwa tuna-join na PGM na tulikuwa tunaenea darasani( sio lecture hall) mbali ya kupokea wanafunzi kibao wanaohamia!

26fa45cadcd45b045ecc548ec460dbda.jpg

Kutokana na hilo, unakuta tatizo la msingi hapa ni kukosekana kwa wanafunzi wengi wa sayansi ambao hatimae wangeweza kwenda kusoma education in science subjects.

To be honest, for now hakuna better option zaidi ya hii Diploma Special Program. Jana serikali imetangaza kutaka kuajiri walimu wastaafu wa sayansi! Huu ni udanganyifu na hadaa kubwa kwa wananchi labda kama hao walimu wamestaafu mwaka jana! Ni hadaa kutaka kuaminisha wananchi kwamba moja ya mikakati ya kukabiliana na upungufu wa zaidi ya Walimu 25,000 ni kuajiri wastaafu!

Labda niwakumbushe!

Katika kukabiliana na hili janga, serikali iliyopita ilianza na Wahitimu wa A Level wa masomo ya sayansi wa miaka ya nyuma ambao hawakuwa na issue za kueleweka mtaani! Hawa ni wanafunzi ambao walipiga A level far back 1990s! Serikali iliahidi full sponsorship na ajira kwenda kusoma Special Advanced Diploma in Education ( Science subjects ). Hata hivyo waliopatikana ilikuwa ni kama tone la maji kwenye bahari!

Baada ya hiyo strategy kutotoa matunda; serikali ikarudi kwa wastaafu na kutangaza ajira kwao! Labda kama waliongezeka wengine lakini nakumbuka idadi ya wastaafu ambao walijitokeza haikufika hata 100 ( mia moja). Hivyo basi, leo hii serikali hii wanataka kuurejea mkakati ule ule ulioshindwa miaka 2 tu iliyopita!

Baada ya kugonga mwamba hizo 2 recruitment mix, ikaonekana the only possible solution kwa sasa ni Diploma special program... yaani kabla madogo hawajabadilika hapa kati kati; unawadaka njiani! Mtoto wa miaka 17 ukimwambia baada ya miaka 3 utakuwa unakula Laki 6 kila mwezi lazima akimbilie... unafanya mchezo na Smartphone nini!!

Hivyo basi, kama nilivyosema hapo awali; nimeipitia Course Structure ya Chemistry & Maths. Nilichokiona ni kwamba, wakishafika UDOM wanasoma tena yale masomo waliyo-specialize. Ikiwa wewe ni Chemistry & Maths; unaendelea kupigwa nondo za chemistry na maths ili kukuweka fit zaidi.

0f740eeae97612e4cacbf0b303f19032.jpg

Hiyo ni 3 years program! Sasa mtu kama huyo ikiwa hata baada ya hapo atashindwa kufundisha O Level basi hata akifika A level hataweza! Kuelewesha nako ni kipaji!

Hivyo basi, ningeishauri serikali iache danadana kwenye serious issues kv kwa sasa HAWANA option! According to Zitto Kabwe, out of 7800 students ni 88 tu ndio wana Div IV. Ikiwa takwimu hizi za Zitto ni sahii; hiyo ni just 1% ! Ipi rationale ya kutupa mayai 100 wakati lililoharibika ni moja tu?! Ikiwa Zitto anafahamu idadi ya wenye Div IV, why not the government!

Kwa mtindo huu, Ikiwa JK Aliiua Elimu, basi JPM Ataizika Rasmi! Mambo mengine hayahitaji mihemuko bali busara! Binafsi huwezi kunishawishi kwamba ni bora shule isiwe na Mwalimu kabisa kuliko kuwa na Mwalimu aliyesoma sekondari miaka 4 na kufaulu na akasoma miaka mingine 3 zaidi ya Diploma!
 
Attachments

  • 13c1170bbdb5e0d89d8049c799c1ab6e.jpg
    13c1170bbdb5e0d89d8049c799c1ab6e.jpg
    39.2 KB · Views: 66
elimu ya awamu ya jk ilijaa magugu na jpm anagoa magugu ili yasiharibu hiyo elimu
 
Sasa ikiwa kauli ya Zitto kwamba wenye Div IV wapo 88; ipi busara ya kurudisha nyumbani wanafunzi 7800 kwa ajili ya 88 ambao, hata ukitoa tamko tu kwamba wasio wajiondoe wenyewe; kwa kukwepa aibu watu watatoroka na mabegi ucku ucku!

That's one but second, mwezi March kulikuwa na figisufigisu ya kwenda field second year ( sina details za kutosha, hivyo kama kuna wahusika hapa, naomba clarification). Wakati wapo home wanajiandaa kwenda Field; wote wakaambiwa warudi chuo kuendelea na masomo! Hata hivyo, masomo hayakuendelea hadi waliporudishwa nyumbani! Sasa danadana zote hizo za nini?! Tatizo hasa ni nini?! Div IV, Mgomo wa Lecturers au pesa?!
 
Ninachoweza kukonclude ni kuwa Tanzania siasa mbele, na kwa vile wanasiasa ndio wanaofanya maamuzi then proffessionals wamezibwa ama kugubikwa na siasa.
sio elimu tu Watanzania tune adopt maisha ya ujanjaujanja tuu kila sector sio private au public!!
mtu atokee hapa aniambie wapi safi hakuna doa hata makanisani ujanjaujanja tuu. sasa ma upele na majipu yanatokea kwenye weak glands ndio tunaona!! lakini we need radical change na tuanze moja. Hata siasa yewnyewe dira haipo!!
Nchi nyingi za wajanja wana think Tank- Tanzania hiyo kitu haiipo twategemea charismatic ya mtawala!!
ujanjaujanja hata katika familia!! tutapona?
 
ELIMU inaishi kwenye fikra za watu na ni urithi endelevu haiwezi kufa wala kuzikwa,ila inaweza kudumazwa kwa mitazamo mgando.Ubunifu unapokosekana wa kimaono yasiyoendana na wakati hufanya elimu kudumaa.Mtazamo mpya juu ya elimu yetu unahitajika.
 
Hapo ndio tatizo kubwa sasa ninaanza kuelewa vizuri ni kwanini Baba Jesca.hana maono na exposure.Hizi ni kasoro za mazoea ya kukariri formula.
Lazima kuwe na mbinu mbadala za kisayansi kulingana na mazingira ya sasa.
Nadhani hata hao wagunduzi wa formula wasinge kubali maboresho wasinge weza kukabiliana na huu ulimwengu wa teknolojia shindani.
 
Jana, kwa msaada wa King snr nilipata Course Structure ya Special Diploma ( Mathematics & Chemistry) . Niliiomba ili niitathimini na kujiridhisha ikiwa hii program itasaidia. Course Structure niliyopatiwa ni ya First Year.

Baada ya kuipitia, hivi sasa naweza kuongea kwa kujiamini kwamba kwa sasa serikali haina mbadala labda kama inafikiria kuajiri walimu wa sayansi kutoka nje ya Afrika au ina mpango wa kufuta over 75% ya mikondo ya sayansi nchini!

View attachment 354241

Kwanza tukumbuke jambo moja.
Wanafunzi wanaoji-commit sayansi ni wachache sana! O Level nilisoma one of the best private schools in town enzi zile... tulikuwa na kila kitu needed for science students! However, kati ya mikondo 6 iliyokuwapo ni 2 tu ndo ilikuwa ya sayansi huo mmoja wala haukuwa reliable.

Hiyo ilikuwa ni shule yenye kila kitu including enough teachers but still at least 70% ya wanafunzi waliikacha sayansi! What about shule zetu zile ambazo hata mwalimu wa historia hakuna?!

A Level nilienda Tambaza! Enzi hizo Tambaza walikuwa wanachukua wanafunzi WENGI SANA wa A Level! Lakini pamoja na yote hayo; PCM tulikuwa mkondo mmoja TU na tulikuwa hatufiki 50! Kipindi cha Maths tulikuwa tuna-join na PGM na tulikuwa tunaenea darasani( sio lecture hall) mbali ya kupokea wanafunzi kibao wanaohamia!

View attachment 354243

Kutokana na hilo, unakuta tatizo la msingi hapa ni kukosekana kwa wanafunzi wengi wa sayansi ambao hatimae wangeweza kwenda kusoma education in science subjects.

To be honest, for now hakuna better option zaidi ya hii Diploma Special Program. Jana serikali imetangaza kutaka kuajiri walimu wastaafu wa sayansi! Huu ni udanganyifu na hadaa kubwa kwa wananchi labda kama hao walimu wamestaafu mwaka jana! Ni hadaa kutaka kuaminisha wananchi kwamba moja ya mikakati ya kukabiliana na upungufu wa zaidi ya Walimu 25,000 ni kuajiri wastaafu!

Labda niwakumbushe!

Katika kukabiliana na hili janga, serikali iliyopita ilianza na Wahitimu wa A Level wa masomo ya sayansi wa miaka ya nyuma ambao hawakuwa na issue za kueleweka mtaani! Hawa ni wanafunzi ambao walipiga A level far back 1990s! Serikali iliahidi full sponsorship na ajira kwenda kusoma Special Advanced Diploma in Education ( Science subjects ). Hata hivyo waliopatikana ilikuwa ni kama tone la maji kwenye bahari!

Baada ya hiyo strategy kutotoa matunda; serikali ikarudi kwa wastaafu na kutangaza ajira kwao! Labda kama waliongezeka wengine lakini nakumbuka idadi ya wastaafu ambao walijitokeza haikufika hata 100 ( mia moja). Hivyo basi, leo hii serikali hii wanataka kuurejea mkakati ule ule ulioshindwa miaka 2 tu iliyopita!

Baada ya kugonga mwamba hizo 2 recruitment mix, ikaonekana the only possible solution kwa sasa ni Diploma special program... yaani kabla madogo hawajabadilika hapa kati kati; unawadaka njiani! Mtoto wa miaka 17 ukimwambia baada ya miaka 3 utakuwa unakula Laki 6 kila mwezi lazima akimbilie... unafanya mchezo na Smartphone nini!!

Hivyo basi, kama nilivyosema hapo awali; nimeipitia Course Structure ya Chemistry & Maths. Nilichokiona ni kwamba, wakishafika UDOM wanasoma tena yale masomo waliyo-specialize. Ikiwa wewe ni Chemistry & Maths; unaendelea kupigwa nondo za chemistry na maths ili kukuweka fit zaidi.

View attachment 354246

Hiyo ni 3 years program! Sasa mtu kama huyo ikiwa hata baada ya hapo atashindwa kufundisha O Level basi hata akifika A level hataweza! Kuelewesha nako ni kipaji!

Hivyo basi, ningeishauri serikali iache danadana kwenye serious issues kv kwa sasa HAWANA option! According to Zitto Kabwe, out of 7800 students ni 88 tu ndio wana Div IV. Ikiwa takwimu hizi za Zitto ni sahii; hiyo ni just 1% ! Ipi rationale ya kutupa mayai 100 wakati lililoharibika ni moja tu?! Ikiwa Zitto anafahamu idadi ya wenye Div IV, why not the government!

Kwa mtindo huu, Ikiwa JK Aliiua Elimu, basi JPM Ataizika Rasmi! Mambo mengine hayahitaji mihemuko bali busara! Binafsi huwezi kunishawishi kwamba ni bora shule isiwe na Mwalimu kabisa kuliko kuwa na Mwalimu aliyesoma sekondari miaka 4 na kufaulu na akasoma miaka mingine 3 zaidi ya Diploma!
Mkuu ingekuwa Ndalichako anapitiaga JF nina Imani lazima angekutafuta akae na wewe na watu wengine wenye akili kama yako kama wa nne hivi aunde pool ya kumshauri! Hakuna ulichokisema ambacho sio sahihi! Subiri uone ni wangapi watapatikana mwaka huu kusoma education science, Kama walikuwaga wanadahili division one hadi three bado kukawa na uhaba itakuwaje wanavyoanza kudahili one na two? One na two za form six zote Tanzania nzima haziweizi kujaza Yombo five ya pale UDSM, na ni nani anapata division one mfano ya PCB au PCM anasoma education wakati medicine, telecom, computer science, electrical na computer engineering zipo? So one hamna so wanabaki wakipambana na division two ambazo pia ni chache. Kuna Vyuo vitafungwa especialy vya private, na DIT, MBEYA TEC, CBE automatically vitarudi kwenye diploma na certificate zao. Tatizo la serekali yetu ni Kutaka kujidai tu narudi enzi za Nyerere bila Kujua mazingira yamebadilika
 
Sasa ikiwa kauli ya Zitto kwamba wenye Div IV wapo 88; ipi busara ya kurudisha nyumbani wanafunzi 7800 kwa ajili ya 88 ambao, hata ukitoa tamko tu kwamba wasio wajiondoe wenyewe; kwa kukwepa aibu watu watatoroka na mabegi ucku ucku!

That's one but second, mwezi March kulikuwa na figisufigisu ya kwenda field second year ( sina details za kutosha, hivyo kama kuna wahusika hapa, naomba clarification). Wakati wapo home wanajiandaa kwenda Field; wote wakaambiwa warudi chuo kuendelea na masomo! Hata hivyo, masomo hayakuendelea hadi waliporudishwa nyumbani! Sasa danadana zote hizo za nini?! Tatizo hasa ni nini?! Div IV, Mgomo wa Lecturers au pesa?!
Pesa mkuu! World Bank walipomaliza mkataba wakaacha project mikono ni mwa serekali mkuu, serekali kujeuka wakakuta mkwanja nao hamna figisufigisu zikaanza, waliosoma mambo ya project wanajua kipengele kinachoitwa SUSTANABILITY hichi kipengele kama hujui kukiandika vizuri hela ya mradi hupati sasa cha kujiuliza WORLD BANK ambayo inafanya miradi mikubwa Mikubwa dunia nzima walikioverlook? Jibu ni hapana wataalamu walioandika huu mradi waliwadanganya jamaa wa WORLD BANK kuhusu SUSTANABILITY, Siunajua tena serekali ya mkwere ilikuwa Imejaa usanii mwingi Mno, NOTE: Nasema Haya Kwa kuwa kuna tetesi Kwamba huu mradi ulikuwa unafadhiliwa na WORLD BANK.
 
...na ni nani anapata division one mfano ya PCB au PCM anasoma education wakati medicine, telecom, computer science, electrical na computer engineering zipo? So one hamna so wanabaki wakipambana na division two ambazo pia ni chache.
Na hapa ndipo ulipo ukweli mchungu zaidi ambao tunaukwepa! Ulichosema ni sahihi kwa 100%. Na hapa tusisahau idadi kubwa ya A Level science graduates ambao hubadili gia angani na kwenda kusoma Accounts, Banking n.k! Kwahiyo wanaanza kujichuja kwa wale wanaoenda favorable programs ulizotaja hapo juu; wenye II wanakimbilia Accounts wanaobaki; wachache ( majority ni Div III ) ndo hao wanaenda vyuo vya ualimu na wengine wanakuwa hawabebeki kabisa na hivyo wengi wao kuishia kutumia vyeti vya form IV badala ya vya form VI kwenye mihangaiko yao ya kujiendeleza kielimu!
 
Mimi naishangaa sana serikali, vijana wote hawa ambao wana diploma/degrees na walisoma masomo ya sayansi but bado hazijawapa matokeo chanya kwanini wasitangaze kuwa kuna special program ya miezi kadhaa then wakaingizwa huko kwenye kufundisha? Haitamaliza tatizo lakini itasaidia kwa kiasi chake
 
Jamani mjadala wa vilaza umefungwa. Serikali imesema muende kwenye vyuo vya saizi yenu.
Hakuna uhitaji mkubwa kihiiiiivyo wa walimu wa sayansi. Kwani anayepaswa kufundisha sayansi sekondari lazima asome degree? Anaweza akasoma diploma kwenye vyuo stahiki na akawa mwalimu wa sayansi kidato cha 1 - 4.

Msijenge taswira kwamba hao vilaza wa udom kufukuzwa kwao ni pigo na watasababisha balaa ktk elimu ya sayansi.
 
Na hapa ndipo ulipo ukweli mchungu zaidi ambao tunaukwepa! Ulichosema ni sahihi kwa 100%. Na hapa tusisahau idadi kubwa ya A Level science graduates ambao hubadili gia angani na kwenda kusoma Accounts, Banking n.k! Kwahiyo wanaanza kujichuja kwa wale wanaoenda favorable programs ulizotaja hapo juu; wenye II wanakimbilia Accounts wanaobaki; wachache ( majority ni Div III ) ndo hao wanaenda vyuo vya ualimu na wengine wanakuwa hawabebeki kabisa na hivyo wengi wao kuishia kutumia vyeti vya form IV badala ya vya form VI kwenye mihangaiko yao ya kujiendeleza kielimu!
Hiyo ilikuwa zamani. Siku hizi ajira hakuna maana graduates wamejazana mitaani wanasaka kazi kila Leo. Nani atampa kazi nyingine graduate wa ualimu wa sayansi? Kama itatokea basi kazi hiyo itakuwa na maslahi kiduchu kuliko ualimu. Acheni kukariri na kujiipaa faraja
 
Mimi ni mmoja kati ya watu tuliovutiwa sana na hotuba ya Raisi Magufuli aliyoitoa pale UDSM ambapo naweza kusema kwamba alitangaza blue print ya Serikali yake ya jinsi anavyotaka kuiboresha Elimu yetu, na kilichonivutia ni uamuzi wa kwamba Chuo Kikuu kibakie kwa wale waliofika kidato cha Sita na kufaulu tu na hawa wengine waende kwenye vyuo vyao stahiki vinavyotoa Diploma na hivi Vyuo tunavyo kama CBE, NIT, Dar tech, n.k!

Sasa kinachofatwa ilipaswa pia kuwe reforms kwenye ajira ili ajira ziendane na aina ya Elimu mtu anayopata kwa mfano haingii akilini Bank teller awe Shahada ya Chuo Kikuu wkt hiyo ni kazi ambayo inaweza kufanywa na mhitimu wa Diploma, au mtu anayekaa dirishani TRA ambaye ndiyo mtu wa kwanza anyekutana mteja awe na Shahada ya Chuo Kikuu kazi hiyo inaweza kufanywa na mtu wa Diploma tu, mtu anayewasha na kuzima mitambo Tanesco hahitaji awe na degree ya electrical engineering hiyo kazi inaweza kufanywa na mtu mwenye Diploma ya technical colleges zetu, n.k hii reform ni muhimu na pia hivi vyuo vyote ambavyo leo badala ya kutoa Diploma wamehamia kwenye Bachelors na Masters pia vilazimishwe na vibakie kutoa diploma tu na hapa naongelea Vyuo kama Dar tech, Mbeya tech, NIT, CBE n. ili kazi ya kutoa degree ibakie kwa Chuo kilichosajiliwa kama Chuo Kikuu tu na si vinginevyo!
Hivi watu wana mawazo gani!!?? hapo ndo unapothibitisha bado tunatumia sera za kikoloni za white collar education na system hii ndo ndo tunataka iendelee kutumika!! mhitimu wa chuo kikuu wa leo kalishwa sumu yeye ni wa kuajiriwa kwenye ofisi tu akikosa anailaumu serikali baada ya kuweka mazingira ya elimu ya kumfanya mhitimu wa chuo kikuu kuwa mjasiriamali unaanza kuweka matabaka ya degree zitolewe wapi!! acheni ulimbukeni tutazalisha wasomi wengi wenye akili kama hizo.
 
Lakini Wakoloni ndiyo Wazungu na ambao wameendelea na ndiyo tunawaiga!
 
Bado ningependa kuamini hii taarifa ya kuwa div.3 hawatachaguliwa kwenda kusoma degree si ya kweli kwani sijaona mantiki yake zaidi ya kuambiwa "wakubwa wanafikiria hivyo". Kwa hiyo kila mkubwa nchi hii analeta yake kwani hatuna institutions ambazo huangalia sera na wadau wakachangia kuja na kitu kinacho-eleweka. Mind you kwenda chuo kikuu toka enzi hizo ni pass mbili at A level (watu walichukuliwa na E mbili). Hapa chini ni matokeo halisi (points, division, subject performance). Hao wote ni Div.3 Form six (2014)
12 III G/STUDIES - 'C' PHYSICS - 'D' CHEMISTRY - 'C' BIOLOGY - 'B' BAM - 'C'
11 III G/STUDIES - 'D' PHYSICS - 'C' CHEMISTRY - 'C' BIOLOGY - 'B' BAM - 'C'
10 III G/STUDIES - 'D' PHYSICS - 'C' CHEMISTRY - 'B' BIOLOGY - 'B' BAM - 'B+'

Siamini mtu mwenye akili timamu atawazuia hawa kenda chuo kikuu labda kama hizo pass zao hamzikubali. Wenye Div.3 na ufaulu hafifu watachujwa na vyuo based on cut off point ya chuo na competition iliyopo.
 
Acha kujidanganya wewe, Dunia nzima inafwata mzumo wa Kizungu wa Kibepari pmj na wa Kikomunisti na hii ni pamoja na mfumo wa Elimu sisi ni nani mpaka tutake tuwe tofauti?
 
Pesa mkuu! World Bank walipomaliza mkataba wakaacha project mikono ni mwa serekali mkuu, serekali kujeuka wakakuta mkwanja nao hamna figisufigisu zikaanza, waliosoma mambo ya project wanajua kipengele kinachoitwa SUSTANABILITY hichi kipengele kama hujui kukiandika vizuri hela ya mradi hupati sasa cha kujiuliza WORLD BANK ambayo inafanya miradi mikubwa Mikubwa dunia nzima walikioverlook? Jibu ni hapana wataalamu walioandika huu mradi waliwadanganya jamaa wa WORLD BANK kuhusu SUSTANABILITY, Siunajua tena serekali ya mkwere ilikuwa Imejaa usanii mwingi Mno, NOTE: Nasema Haya Kwa kuwa kuna tetesi Kwamba huu mradi ulikuwa unafadhiliwa na WORLD BANK.
Hata mimi nipo certain kwamba tatizo hapa ni pesa na mengine yote ni siasa tu! Na ukweli kuhusu pesa unaonekana sana pale ambapo wanafunzi waliotakiwa kwenda field walishindwa kufanya hivyo!

Kuhusu World Bank kufadhili hii program; hata mimi nilipata hizo taarifa cuz' hawa jamaa kitambo kidogo walikuwa na project inayoitwa Developing Science, Mathematics & ICT (SMCIT) Teachers in Sub Sahara Africa! Sasa nadhani serikali ya JK ilipitia hapo!
 
Acha kujidanganya wewe, Dunia nzima inafwata mzumo wa Kizungu wa Kibepari pmj na wa Kikomunisti na hii ni pamoja na mfumo wa Elimu sisi ni nani mpaka tutake tuwe tofauti?
ndo toa mfano ni nchi gani imefanikiwa kwa mfumo huo unaotajwa hapo juu zaidi ya kuwa ulianzishwa afrika kwa maslahi ya wakoloni, ni kweli lazima kuwe na vyuo vya kutoa degree na diploma lakini sio kama unavyotaka wewe haiwezekani UDSM na UDOM pekee watoe degree wengine watoe diploma isitoshe hivyo ulivovitaja cbe ifm nit ni vyuo vya serikali kwa nini wasiviendeleze viweze kupokea wanafunzi wengi na warekebishe ufundishaji hapo tutaendelea, ila tz nzima kuwe na vyuo viwili tu vya kutoa degree!!
 
Back
Top Bottom