Baada ya Panya Road sasa kikundi kingine kimeibuka

Baada ya Panya Road sasa kikundi kingine kimeibuka

kyalankota

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2014
Posts
2,594
Reaction score
1,463
Kikundi kingine mbadala wa panyaroad kinaitwa LIBYA kimeibuka, kinahusisha wanafunzi watoro wa primary na sekondary. Wanajihusisha na kuvuta na kuuza bangi.

Source: ITV
 
Ukifuatiliwa kwa makini utashangaa kuna mkono lowassa ili ule msemo wake wa vijana ni bomu linalokaribia kulipuka litimie
 
Ukifuatiliwa kwa makini utashangaa kuna mkono lowassa ili ule msemo wake wa vijana ni bomu linalokaribia kulipuka litimie

Unaitaji mume wewe na unafkr kwa kuptia makalio yan lowasa anawashkia bangi mdomon wewe mdmu
 
Akili zake mgando kabisa na ubungo wake utakuwa wa kondoo na sio mbuzi
 
Kikundi kingine mbadala wa panyaroad kinaitwa LIBYA kimeibuka, kinahusisha wanafunzi watoro wa primary na sekondary. Wanajihusisha na kuvuta na kuuza bangi.

Source: ITV

Sasa Ni Kikundi Cha Wahalifu au Ni Kikundi Cha Wavuta Bangi? Hivi Wahalifu Wote Duniani Kumbe Huvuta Bangi? Very Interesting!
 
Unaitaji mume wewe na unafkr kwa kuptia makalio yan lowasa anawashkia bangi mdomon wewe mdmu

Hujamwelewa vyema mdau alichokisema ni kuwa kuna kipindi ndg lowasa alitoa onyo kuwa kwa ukosefu huu wa ajira elimu duni vijana ni bomu linalosubiri kulipuka sasa ndio tunaona taratibu bomu likitoa moshi.
 
Kundi jipya la kihalifu linalojulikana kwa jina la Libya limeibuka jijini la Dar es Salaam na kuvamia eneo la kituo cha daladala cha Tabata Mawenzi na kufanya uharibifu mkubwa uliosababisha magari kadhaa kuvunjwa vioo na kuzua taharuki kubwa miongoni mwa wakazi, wafanyabiashara na wapita njia katika eneo hilo.

Kundi hilo limeibuka ikiwa ni miezi chache baada ya kundi la vijana wa kihalifu, maarufu kama ‘Panya Road’ kufanya vurugu na kuzusha hofu kubwa jijini Dar es Salaam. Tukio hilo lilitokea jana na vijana wawili wametiwa mbaroni na hadi tunakwenda mitamboni walikuwa wakiendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kwa tuhuma za kuhusika na vurugu hizo.

Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mary Nzuki, alithibitisha kutokea vurugu hizo, vurugu hizo zilizuka juzi majira ya saa 8 mchana baada ya vijana hao kutoka kwenye mazishi ya mwenzao anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira. Hata hivyo, Kamanda Nzuki alisema vijana wawili walikamatwa kwa tuhuma za kufanya vurugu na kuvunja vioo vya magari na hadi jana walikuwa wakishikiliwa na polisi.

Kijana huyo, Amiri Shabani (14-15), maarufu kwa jina la “Ega”, ambaye ni mkazi wa maeneo ya mtaa wa Twiga, kata ya Kimanga, anadaiwa kuuawa usiku wa kuamkia juzi. Habari kutoka eneo hilo zinaeleza kuwa, kijana huyo aliuawa kwa kupigwa na wananchi hao baada ya kumvamia njiani mwanamke aliyekuwa akipita eneo la Mawenzi na kujaribu kumpora mkoba wake, ambao ndani yake kulikuwa na fedha.

Hata hivyo, baadhi ya mashuhuda, walisema kuwa, jaribio la kijana huyo halikufanikiwa, kwani jitihada zake za kutaka kuupora mkoba wa mwanamke huyo ziligonga ukuta.

Mashuhuda hao walisema mwanamke huyo akiwa anapita njia katika eneo hilo, kijana huyo alimvamia na kujaribu kuupora mkoba wake.

Walisema mwanamke huyo alitoa upinzani mkali kwa kuung’ang’ania mkoba wake, huku akipiga mayowe kuomba msaada.

Kwa mujibu wa mashuhuda hao, kelele za mayowe ya mwanamke huyo zilifanikiwa kuwavuta wananchi wengi, ambao walifika katika eneo hilo na kumsaidia na kIsha kuanza kumshambulia kijana huyo hadi kumuua.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Twiga, Kata ya Kimanga, Said Runje, alisema mwili wa kijana huyo ulizikwa katika makaburi ya Kwa Chonde, eneo la Tabata, juzi mchana.

Alisema kabla ya kwenda makaburini, wakiwa kwenye eneo la msiba, vijana hao walitoa ilani kwa kuapa kwamba, wangelipiza kisasi kupinga kuuawa kwa mwenzao baada ya kurejea kutoka kwenye mazishi.

Alisema habari za tishio hilo zilizagaa ghafla katika maeneo mengi ya Tabata, hali iliyowafanya wafanyabiashara kufunga biashara zao, zikiwamo za maduka na wakazi kujifungia ndani ya nyumba zao wakihofia vijana hao kuwadhuru.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alikana kuhusishwa vijana hao na kundi la ‘Panya Road’, akisema hakuna mwananchi aliyetoa taarifa polisi kuhusu kuibuka upya kwa vijana wa kihalifu wa aina hiyo. Hata hivyo, aliahidi kulizungumzia suala hilo leo baada ya kupata taarifa kamili.

Chanzo: NIPASHE
 
Back
Top Bottom