Baada ya October 29 tusitarajie Nchi kuwa Sawa tena.

Baada ya October 29 tusitarajie Nchi kuwa Sawa tena.

Mr Kipara

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2013
Posts
566
Reaction score
1,029
Naandika huku nikiwa na huzuni kubwa kwa Taifa letu kupoteza nguvu kazi kubwa (vijana), inakadiriwa zaidi ya vijana elfu 20+ waliuawa kwenye kile kilichoitwa Uchaguzi.

Itakuwa nikujidanganya kwa kudhani mambo ni shwari kama ilivyokuwa kabla ya hicho kilichoitwa Uchaguzi, ukweli nikwamba Taifa limechukuwa Mkondo mwingine kabisa kiasi kwamba kama Watawala wataendelea kushupaza shingo hakuna atakaye kuwa salama.

Huku mitaani wenye Baiskeli na Pikipiki za SSH wanaziogopa hata kuziendesha,hata wale wanaopeperushaga Bendera za kijana kwenye Majumba yao wamezishusha kwa hofu ya kuchomewa nyumba zao.

Ndugu zangu, siioni ile Tz tulioiziea tena, kwanamna mambo yanavyokwenda Taifa limevimba kila mtu analia kivyake hata kama hakukutwa na hii misiba.

Tumekwisha tengeneza Taifa la visasi, hawa watu waliopoteza ndugu zao tusije kujidanganya kwamba watasahau,utakuwa ni uwenda wazimu kufikiria hivyo.

Tujiandae kwa mambo magumu huko mbele, nina hakika hata Watawala hawatakaa kwa amani kama zamani kwasababu hata wao wanajua nini kinakwenda kutokea.

Nawasilisha.
 
Naandika huku nikiwa na huzuni kubwa kwa Taifa letu kupoteza nguvu kazi kubwa (vijana), inakadiriwa zaidi ya vijana elfu 20+ waliuawa kwenye kile kilichoitwa Uchaguzi. Itakuwa nikujidanganya kwa kudhani mambo ni shwari kama ilivyokuwa kabla ya hicho kilichoitwa Uchaguzi,ukweli nikwamba Taifa limechukuwa Mkondo mwingine kabisa kiasi kwamba kama Watawala wataendelea kushupaza shingo hakuna atakaye kuwa salama. Huku mitaani wenye Baiskeli na Pikipiki za SSH wanaziogopa hata kuziendesha,hata wale wanaopeperushaga Bendera za kijana kwenye Majumba yao wamezishusha kwa hofu ya kuchomewa nyumba zao. Ndugu zangu, siioni ile Tz tulioiziea tena, kwanamna mambo yanavyokwenda Taifa limevimba kila mtu analia kivyake hata kama hakukutwa na hii misiba. Tumekwisha tengeneza Taifa la visasi,hawa watu waliopoteza ndugu zao tusije kujidanganya kwamba watasahau,utakuwa ni uwenda wazimu kufikiria hivyo. Tujiandae kwa mambo magumu huko mbele,nina hakika hata Watawala hawatakaa kwa amani kama zamani kwasababu hata wao wanajua nini kinakwenda kutokea. Nawasilisha..............
Tusubiri mipasho mingine leo tena wameshamuandalia ni kama hakuna kilichotokea kwa mujibu ya Al ya muliro
 
Bila kukaa chini na kuangalia wapi tumejikwaa Nchi inakwenda kubaya sana. Huku kwa ground ukisikiliza mazungumzo ya watu mpaka unaogopa watu wamekasirika ni hatari, Taifa linakwenda kuangamia.
kwa hao haramu unampigia mbuzi gitaa yaani wako uchi ila wanaziba sura kwa mikono
 
Hiyo inaitwa FACTORY RESET. Wazungu wameumizana sana miaka hiyo hadi leo unawaona wakula bata.
 
Back
Top Bottom