Baada ya Mwigulu kufutwa uwaziri, hii ndio post niliyoielewa sana kutoka Twitter

"Mwigulu alikuwa na nafasi ya kuwa shujaa, mara nyingi tu. Mara zote ambazo mauaji yalifanyika, watu walipotea na mamlaka ya uteuzi ikamfunga mikono, alipaswa kujiuzulu kwa sababu kama umepewa kazi na unakwazwa katika kuifanya basi hiyo kazi haina maana. Timing."
Angewawahi akajiuzuku angejizolea bonge la u staa ila kwa sasa anatia huruma.
 
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo..

Ushauri huu nadhani sasa ni wa kumpa Muheshimiwa sana kutoka Bumbuli, February Marope.
Maana ndiye aliyebaki kwenye list ya "out"
Tusubiri maana kipindi cha pili kimeanza..
 
Bora alivyongojea kutumbuliwa maana alijijuwa kuliko angetaka kujiuzulu wangekuwahi fasta na hata kama angefanikiwa angejiweka nafasi mbaya zaidi na hata kupotezwa kabisa kwenye ramani maana baba hakubali kushindwa na wanawe
 
N
Mwigulu tulimwambia humu, azungumze kama Waziri akaamua kunyamaza ili asijiharibie ndoto za Urais. Sasa amekosa sympathy ya wananchi na chamani huko sasa hivi anaoga matusi tu.
Huko jimboni safari hii Kishoa atamgalagaza
 
"Mwigulu alikuwa na nafasi ya kuwa shujaa, mara nyingi tu. Mara zote ambazo mauaji yalifanyika, watu walipotea na mamlaka ya uteuzi ikamfunga mikono, alipaswa kujiuzulu kwa sababu kama umepewa kazi na unakwazwa katika kuifanya basi hiyo kazi haina maana. Timing."
Kweli alichelewa mno na tatizo alishindwa kusoma alama za nyakati. Kwa heshima alipaswa awe ameshajiuzulu mapema kabisa badala ya kusubiri utenguzi
 
Wateuliwa wengine wajifunze kutoka kwa Mwigulu.
Ukiona unapelekeshwa pelekeshwa na aliyekuteua, acha kazi kulinda heshima yako.
 
Yeye mwenyewe muuaji! Anapenda kusikia adui wake wa kisiasa wanateswa na kuuwawa! Hivyo kwa matukio hayo ya kutisha katu asingeweza kujiuzulu!

HII NI COMMENT BORA KABISA KWA MWAKA WETU WA FEDHA WA 2018-2019!
 
Back
Top Bottom