Baada ya maka 62 Cuba, haitakuwa na Kiongozi anayeitwa Castro baada ya Raúl kutangaza kujiuzulu Ukatibu Mkuu wa Chama

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Hatimaye, baada ya maka 62, taifa la Cuba litaamka siku ya Jumatatu bila kuwa na Kiongozi wa Nchi anayeitwa Castro! Raúl Castro anatarajiwa kuachia madaraka kama Katibu Mkuu wa Chama, cheo kinachotajwa kuwa na nguvu kuliko cha Rais nchini humo.

Raúl, anayetarajiwa kutimiza miaka 90 mwezi Juni, analiacha taifa hilo bila chakula cha kutosha na hali mbaya kiuchumi, likitangaza kuporomoka kwa uchumi kwa asilimia 11 mwaka 2020 kutokana na athari za COVID19, huku likiwa kaika uhusiano mbaya na Marekani baada ya utawala wa Rais Trump kukaza vikwazo vya kiuchumi vilivyokuwa vimelegezwa wakati wa utawala wa Obama.

Licha ya kujiuzulu wadhifa wake kama Kiongozi Mkuu wa Taifa hilo mwaka 2018, Raúl alikuwa na nguvu kubwa ya madaraka kutokana na nafasi ya chama katika kuendesha siasa za Cuba.

Raúl ametangaza nie yake ya kujiuzulu uongozi wa chama wakati wa kuanza kwa Mkutano Mkuu siku ya Ijumaa, na mrithi wake anatarajiwa kupatikana mkutano utakapomalizika siku ya Jumatatu.

Matarajio ya wengi, hata hivyo, yapo kwa mrithi wake aliyemchagua kubeba mikoba yake alipoachia madaraka ya urais mwaka 2018, Miguel Díaz-Canel Bermúdez.

Díaz-Canel anatarajiwa kuchukua nafasi zote mbili, yaani Urais na Ukatibu Mkuu wa Chama, kama ilivyo desturi ya nchi hiyo, ambapo Fidel Castro alishikilia nyadhifa zote hizo kwa miaka 30.

Zama za Castro nchini Cuba zitakumbukwa kwa uongozi wenye kutunishiana misuli na ‘mabeberu’ kutokana na tofauti zao za kiitikadi, hasa wakati wa vita baridi. Raúl aliingia madarakani kama Katibu Mkuu wa Chama mwaka 2008 baada afya ya kaka yake, Fidel Castro kufifia.
 
Back
Top Bottom