Baada ya majoho, hili la makoti meupe pia likemewe

Baada ya majoho, hili la makoti meupe pia likemewe

kabon14

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2016
Posts
1,233
Reaction score
872
Ni wiki chache zimepita tanga waziri wa elimu prof.Ndalichako atoe tamko kuhusu matumizi holela ya majoho katika mahafali mbalimbali Na kusema kuwa vazi Hilo linapaswa kutumiwa Na wahitimu wa vyuo vikuu pekee, hii Ni kwa ajili ya kulinda HADHI YA VAZI HILO..!!
(Mengi yalijadiliwa)


Katika pitapita zangu nimejionea udhalilishaj mwingine wa wazi jingine linalotumiwa Na watu muhimu Sana hapa nchini Na hata duniani kote.

>Koti jeupe/white coat ( lab coat, clinical coat e.t.c)

wp_ss_20161209_0001.png


Vazi Hilo Ni maalum kwa watu wanaohusika na huduma za kiafya

Sasa sifahamu Kama na hata huko nchi za wenzetu vazi Hilo hutumiwa kiholela Kama ilivyo hapa kwetu( anayefahamu zaidi anijuze) lakini kimsingi haileti picha nzuri na tunashusha hadhi ya vazi hilo

Miaka kadhaa iliyopita lilianza kutumiwa na wauza bucha, ikazoeleka na tukaona Ni jambo la kawaida Tu

wp_ss_20161208_0001.png


Sifahamu aliyetoa wazo Hilo kwanini alichagua rangi nyeupe( anayefahamu anijuze)

Nikiwa safarini wiki hii nilistaajabu kuona vazi hilo
Linatumiwa Na wamachinga(nakosa jina zuri la kuwaita)
ila ninamaana ya wale jamaa wanaouza vyakula Na vinywaji katika vituo vya mabasi.

Hii nimeiona katika stand ya mabasi ya mkoa flani hapa Tanzania

WP_20161208_004.jpg
WP_20161208_009.jpg
WP_20161208_013.jpg
WP_20161208_014.jpg
WP_20161208_016.jpg
WP_20161208_017.jpg


Nilipowaona nilidhani ni madaktar wanafunz wako kwenye mafunzo kwa vitengo, lakini niliamin kuwa fikra zangu sio sahihi baada ya kuwaona wakiwa wamebeba chips Na kuuza madirishani.

Mwenye uelewa zaidi kuhusu hii kitu ni vema atujuze.

Ahsanteni.
 
Hao wengine wanajaribu kuvaa "mavazi kama ya madaktari lakini siyo ya madaktari"
 
Matumizi ya joho ni tofauti na koti jeupe.Joho ni kama ngao ya ushindi anayovalishwa shujaa wa vita.
Ndio sababu linatakiwa kuvaliwa na wahitimu wa vyuo maana safari yao ya elimu ni sawa na vita lakini wameikamilisha.
Ni makosa kumvalisha muhitimu wa form four joho kwa sababu hajakamilisha vita vyake kwani bado ana safari ndefu ya kukamilisha elimu yake kwa kufika chuo kikuu na kuhitimu.

Koti jeupe ni alama ya usafi.Nguo/koti nyeupe linavaliwa na watu wanaofanya kazi nyeti sana kama zinazohusu afya ya binadamu, vyakula vya binadamu, afya ya mifugo, utengenezaji wa bidhaa za viwandani zenye kuhitaji kiwango kikubwa cha usafi.

Mtu anapovaa koti jeupe, havai kama alama ya ufahari wa kazi yake bali kama alama ya usafi unaohitajika kazini kwake.Kwenye hali hizo, rangi nyeupe hutumika ili iwe rahisi sana kugundua uchafu kama utakuwepo.
 
Matumizi ya joho ni tofauti na koti jeupe.Joho ni kama ngao ya ushindi anayovalishwa shujaa wa vita.
Ndio maana linatakiwa kuvaliwa na wahitimu wa vyuo maana safari yao ya elimu ni sawa na vita lakini wameikamilisha.
Ni makosa kumvalisha muhitimu wa form four joho maana hajakamilisha vita vyake kwani bado ana safari ndefu ya kukamilisha elimu yake kwa kufika chuo kikuu na kuhitimu.

Koti jeupe ni alama ya usafi.Nguo/koti nyeupe linavaliwa na watu wanaofanya kazi nyeti sana kama zinazo husu afya ya binadamu, vyakula vya binadamu, afya ya mifugo, utengenezaji wa bidhaa za viwanda zenye kuhitaji kiwango kikubwa cha usafi.

Mtu anapovaa koti jeupe, havai kama alama ya ufahari wa kazi yake bali kama alama ya usafi unaohitajika kazini kwake.Kwenye hali hizo, rangi nyeupe hutumika maana ni rahisi sana kugundua uchafu kama utakuwepo.
Lakini mkuu wangetofautisha kwenye mtindo wa ushonaji wa hayo mavazi,maana kwa hayo jamaa hapo juu inaleta sintofaham
 
Lakini mkuu wangetofautisha kwenye mtindo wa ushonaji wa hayo mavazi,maana kwa hayo jamaa hapo juu inaleta sintofaham
Sioni sintofahamu yoyote kwenye hilo swala, labda kama umenuia kuleta matabaka.

Mbona suruali anazovaa Magufuli zina mtindo wa ushonaji sawa na zile za wamachinga na haziibui sintofahamu yoyote?
Halafu hili jambo ni dogo sana kiasi cha kuhitaji mjadala.
 
Haha mtataka namasikini wapigwe marufuku kuvaa suti. ..
 
hapo utawwagusa wauza senene, wanaozunguka mitaani wamevaa makoti utafiiri madaktari.
 
Back
Top Bottom