Nahisi umeandika ukiwa unakimbia ndo maana hukuwa na muda wa kuwaza vizuri.
Nakuomba ujue kuwa nafasi ya uraisi si ya majaribio,kama ni majaribio basi tosha. Kwa nchi kuongozwa kwa utashi wa mtu na si kwa kufuata katiba na sheria za nchi. ..hapo ni big NO brother,..Huyo mtu wako mshauri aende kwa kina ngosha wenzie kujaribu tu kupewa jimbo...atakuja kukupa salaamu!
Nafikiri watanzania tunataka rais mweledi,awe chini ya katiba na sheria za nchi. Asiwe na visasi,awe na mapenzi ya kweli kwa nchi na watu wake.
Ngosha,hebu kaa ufikirie tena halafu urudi na kama wazo la raisi ajaye bado litakuwa hilo hilo basi nakushauri ufanye ibada ya kufunga na kuomba umuulize Mungu akupe jina.