Baada ya kutumia tv ya kichina ndio nimeamini kwa nini mchina anapigwa vita ya uchumi

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,146
11,192
Sasa ndio naamini kwa nini mchina anapigwa vita na kuwekewa figisu barani ulaya na America yote ni kutokana na bidhaa zake kuwa cheap lakini ni nzuri,na ndio naamini sio kila kitu kutoka china ni feki.

Mwaka 2015 nilinunua tv 3 moja ya nyumbani na mbili za kuweka eneo la biashara, mbli zilikuwa ni brand za samsung na Lg na nilichukua kwenye maduka yao kabisa na moja ilikuwa ni ya star x ya bei cheap zote zilikuwa ni 32 inch.

lakini mwaka wa Nne huu ile tv ya samsung kioo kizima kimejaa mistari na ya Lg, ndio ilikufa kabisa, na zote zilikuwa zinatumika kuanzia asuhi nonstop hadi usiku ndio zilikuwa zinazimwa

lakini kinachinishangaza ni tv ya kichina hadi leo inapiga mzigo na haina kasoro yoyote na inawashwa asubihi hadi usiku nonstop, hapo ndipo nilipomini kuwa figisu anazowekewa mchina kwenye bidhaa zake sababu ndio hizi, ana vitu vizuri na bei ni cheap,

Angalia huawei jinsi anavyoandamwa,na inasemekana china anaingiza barani ulaya bidhaa nyingi imara za kielectroniki kwa bei cheap ndio maana wanamuwekea vikwazo
 
Ni kweli mm nina hiyo star x inch 43 ina mwaka wa nne sasa na inapiga mzigo fresh tu iko poa saana
 
mkuu mimi nimeshangaa aisee, vitu vingi vinavyosifika kuwa ni og ndio majanga
Ni kweli mm nina hiyo star x inch 43 ina mwaka wa nne sasa na inapiga mzigo fresh tu iko poa saana
 
samsung na lg ni brand zinazoheshimika kwa ubora duniani, so lazima tuhoji hizi bidhaa za kichina zinazoitwa feki iweje zidumu mda mrefu, ndio maana nikasema kuwa hata ulaya wameona tishio la bidhaa za china ndio maana anawekewa vikwazo
Wewe jamaa wa wapi?

Samsung na LG ni kampuni za South Korea na anaempiga vita China ni mMarekani wapi na wapi loh! Mahaba mengine haya ya pemba
 
Star X hata mimi nawakubali,mwaka wa pili sasa haijasumbua,ingawa nilitishiwa kuwa ni kimeo sana...
 
Kweli tena ilikua inahusu maswala ya ofisini na sio nyumbani....ronjo hizi jamanii hii ndio shida ya wachina kujifunza kiswahili
IMG_20190604_155647.jpeg
 
samsung na lg ni brand zinazoheshimika kwa ubora duniani, so lazima tuhoji hizi bidhaa za kichina zinazoitwa feki iweje zidumu mda mrefu, ndio maana nikasema kuwa hata ulaya wameona tishio la bidhaa za china ndio maana anawekewa vikwazo
Europe bado hawajamwekea mchina zengwe aliyemuwekewa zengwe ni only U.S kwa sababu ana nguvu kumzidi China.

Na si muda mrefu Mama EU ataanza kumpa ban china
 
Back
Top Bottom