Baada ya kutoswa, Sumaye sasa ateta na viongozi wa CHADEMA

Sumaye huyo huyo ndiye alisema Moshi, kama mfanyabiashara anataka biashara zake ziende vizuri asijiunge na upinzani. Inakuwaje leo anataka kujiunga na upinzani, je anataka mambo yake yaende vibaya????
 
Sumaye hana moral authority wa kuwa mtaji kwa cdm,alipokuwa madarakani kajilimbikizia ardhi hovyo kama Kibaigwa na Mvomelo hawapendi ata kulisikia hilo jina na alikuwa na majibu ya dharau kwa wapinzani. Kwa nn asitulie ajilie marupurupu yake ya ustaafu? Kama ccm wameshindwa kumpa japo uNEC cdm watampa cheo kipi? Labda udiwani.


Mkuu madiwani wa Chadema ni watu ambao wana hadhi na heshima kwenye jamii kuliko Sumaye kwa sasa. usiwafananishe naye kwa namna yoyote ile na yeye. Kwa kifupi Sumaye hafai hata kuwa normal card holder wa chadema.

1. Tunajua roho mbaya aliyonayo kwa wananchi: Rejea alivyotuma FFU kung'oa mabomba ya Maji karatu kwa kuwa tu yamepatikana kwa juhudi za Dr Slaa. (wakati huo kumbuka kwa miaka yote CCM walishindwa kuchimba hata kisima)

2. Kumbuka alivyooua kwa makusudi mashamba ya nafco kule hanang' (jimboni kwake) kisa baadhi ya mameneja walimwambia hujasoma in comparison na wao kwa wakati kitu ambacho ni kweli. Mashamba hayo yalikuwa yameajiri zaidi ya watu elfu tano na hell of value chain attached to it. Worse enough Wakati huo akiwa waziri wa kilimo!

3. Wananchi wa hanang' wanajua jinsi ambavyo amekuwa kimya kwa watu wanaohujumiwa na genge la majambazi wafanya biashara wanaofahamika ambao wanafahamika kwa kuchoma magari, maduka na kila aina ya ukatili kwa mtu ambaye anafanya biashara kihalali kwa kuwa tu wao wanataka kuhodhi kila biashara kwa ubabe. Mpaka leo wanah

4. Hakuna asiyejua kwamba anasupoti chadema sasa kama confort zone yake ya kupata pyschological relief! Ifike mahali tuseme hell no!


Ni hayo tu kwa leo, inshallah muda mwingine tutaona what next.
 
Sisi tutaongea tu, lakini ndo hivyo tayari wameshateta, tusubiri kitakachojiri.

I like it, watu wamekaa nyumbani mnajifariji kwa kuandika tu kwenye JF. wachukua maamuzi wana vigezo vyao na kama watamtaka ataingia tu CDM. Mbona kwa Millya mliongea sana na akaingia. Great thinkers vipi? cha maana ni kushauri tu kama anaingia asiingie kutaka uongozi. taratibu zitafuatwa na kama akikosa uongozi awe mpole na kujenga chama asiwe kama Shibuda.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Huyu alijulikana kama zero ama apendisha number na kuwa chanya? Imean 1 plus and above?
 
  • NI KUHUSU MUSTAKABALI WAKE KISIASA

Mussa Juma, Arusha na Boniface Meena, Dar | Mwananchi | October 05, 2012

SIKU chache baada ya kushindwa katika uchaguzi wa ndani kwenye nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amekutana na viongozi wa Chadema ikidaiwa kuwa ni kujadili pamoja na mengine, uwezekano wa kuhamia huko ili agombee urais katika Uchaguzi Mkuu ujao 2015.

Sumaye ambaye anatajwa kuwa alikuwa na mpango wa kuwania urais kupitia CCM, alishindwa katika uchaguzi wa kuwania ujumbe wa Nec, baada ya kupata kura 481 dhidi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk Mary Nagu aliyepata kura 648.

Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa Chadema, zimeeleza kuwa Sumaye hakuridhishwa na mchakato wa uchaguzi huo wa Nec na kwa matokeo hayo, alikutana na viongozi wa Chadema kujadili mustakabali wake kisiasa.

Jana, mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya Chadema, ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alithibitisha Sumaye kukutana na viongozi wa Chadema. Hata hivyo alisema hawajafikia mwafaka.

Source Sumaye ateta na Chadema

Kwa nini asiende kama mwanachama wa kawaida kwanza kisha mambo ya urais yafuate taratibu zilizowekwa?
 
hawa ccm wanafaya watazania mataira!!kwa hiyo we sumayye unadhani tu kwa kuwa ulishakuwa waziri mkuu basi ukienda CHADEMA utapitishwa kuwa raisi???uar very wrong.kwa lipi ulilolifanya??we subiria jela tu 2015 CHADEMA ITAKAVYOANZA KUWASHULIKIA MAFISISADI!!
 
Mussa Juma, Arusha na Boniface Meena, Dar
SIKU chache baada ya kushindwa katika uchaguzi wa ndani kwenye nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amekutana na viongozi wa Chadema ikidaiwa kuwa ni kujadili pamoja na mengine, uwezekano wa kuhamia huko ili agombee urais katika Uchaguzi Mkuu ujao 2015.


Sumaye ambaye anatajwa kuwa alikuwa na mpango wa kuwania urais kupitia CCM, alishindwa katika uchaguzi wa kuwania ujumbe wa Nec, baada ya kupata kura 481 dhidi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk Mary Nagu aliyepata kura 648.

Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa Chadema, zimeeleza kuwa Sumaye hakuridhishwa na mchakato wa uchaguzi huo wa Nec na kwa matokeo hayo, alikutana na viongozi wa Chadema kujadili mustakabali wake kisiasa.

Jana, mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya Chadema, ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alithibitisha Sumaye kukutana na viongozi wa Chadema. Hata hivyo alisema hawajafikia mwafaka. Alisema mawasiliano ya Chadema na Sumaye yalianza mara tu baada ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Septemba 30, mwaka huu yaliyomwengua kigogo huyo kwenye kinyang’anyiro hicho.


“Ni kweli kuna watu wa CCM tumewasiliana nao baada ya uchaguzi ule (wa Nec) na Sumaye tunawasiliana naye pia lakini siwezi kusema tumefikia wapi,” alisema mjumbe huyo na kuendelea: “Suala kwamba amekubaliwa kujiunga na Chadema au la, nadhani huu ni uamuzi wake.

Ninachoweza kusema ni kwamba vikao vilikuwepo na vinaendelea kukaliwa.” Alisema baada ya matokeo ya Hanang’ na hali ya kisiasa ndani ya CCM, Chadema kimekuwa kikiwasiliana na Sumaye na kikubwa ambacho kinajionyesha ni kada huyo wa CCM kutoridhishwa na hali ya mambo ndani ya chama chake.


Mjumbe huyo wa Chadema alisema chama hicho Wilaya ya Hanang’ kinaandaa mkutano maalumu wa kuwapokea wanachama wapya wa CCM, wengi wao wakiwa baadhi ya walioanguka kwenye uchaguzi wa Nec wilayani humo. Habari zaidi zimeeleza kuwa Chadema kimepanga siku yoyote juma lijalo, kuwapokea wanachama wapya kutoka CCM, baadhi wakiwa wale walioshindwa kwenye uchaguzi wa ndani ya chama hicho uliofanyika wilayani Hanang’.

Mmoja wa watu wa karibu na Sumaye alisema anachojua ni kwamba Chadema wanamtaka Sumaye na siyo Sumaye kukitaka chama hicho cha upinzani. “Wamekuwa wakimfuatafuata mara nyingi na mazungumzo ya aina hiyo si mageni baina ya Sumaye na Chadema. Ila ninachoweza kusema, safari hii chochote kinaweza kutokea kutokana na hasira alizonazo (Sumaye). Ngoja tusubiri, atafanya mkutano na waandishi Jumapili.”


Sumaye, Mbowe wazungumza
Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Sumaye alisisitiza kuwa atazungumzia masuala yote yanayohusiana na uchaguzi huo wa Hanang’ atakapokutana na waandishi wa habari, Dar es Salaam. “Nitakutana na waandishi wa habari kuzungumzia kilichotokea naomba tu mwendelee kunipa muda,” alisema Sumaye na kuongeza kuwa alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda Dar es Salaam.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yeye si msemaji wa Sumaye... “Sitaki kumzungumzia Sumaye. Mimi si msemaji wake. Tumsubiri yeye azungumze kuhusu hilo.”


Kada wa CCM Hanang’ anena
Katika hatua nyingine, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Hanang’, Goma Gwaltu amekionya chama hicho kuwa kisipodhibiti vitendo vya rushwa katika chaguzi zake, kitakufa. Gwaltu alisema jana kwamba kwa mazingira yaliyopo sasa ndani ya CCM bila hatua kali kuchukuliwa, kiongozi asiye na fedha hawezi kushika uongozi na ndiyo sababu anaungana na wana-CCM wengine katika wilaya hiyo, ambao wanafikiria kukihama chama hicho.


“Kama wewe una nia ya kuendelea na siasa siyo rahisi kushinda hapa Hanang’ ukiwa hukubaliani na watu fulani, sasa mimi naona ni bora tu kutafuta chama kingine kwani siyo dhambi,” alisema Gwaltu bila kuwataja ambao wanataka kuhama CCM.

Hata hivyo, Gwaltu alisema kwa upande wake, hafikirii kuendelea na mambo ya siasa wala kulalamika makao makuu ya CCM kuhusiana na alichokiita hujuma alizofanyiwa.

MY TAKE.

1. Ni kweli Sumae anataka kutuaminisha kuwa katika uchaguzi ule hakukata pesa kwa wapiga kura au yeye alizidiwa kiasi cha kukata???
2. Kama Chadema watakubali ahamie ili atimize azma yake ya kugombea Urais (Haijalishi kama atashinda au La). Je hii itamaanisha kuwa SUMAE ni bora kuliko Dr. Slaa (aliegombea 2010) au Zitto alietanganza Kugombea 2015 na mwenyekiti Mbowe hajasema kama tagombea au la???
3. Chadema wamejiaandaje kufilter wanachama wanaohamia kutoka vyama vingine hasa CCM ambao ni Mamluki???

 
Am sorry Waungwana Hii story Imeandikwa kwenye Gazeti la Mwananchi la Leo tarehe 4/10/2012
 
jamani tumemchoka sumaye huku
kila saaa
aanzishe chama chake sidhani kama hata tlp wanamtaka
 
He saved as a PM for 10 yrs & yet he believe he has a new thing for this country. This is just next to impossible.
 
Kazi sana jamani,duu Sumaye akihama CCM nitamshangaa sana,kweli si dhambi ila CCM imemjenga sana angetulia sana tu tena asaidie kujenga chama si kuhama!maana akiwa CDM sidhani kama atakuwa na mvuto kivileee!!
 
Aaaaaaaa
sumaye tena loo
kapi la ccm halina nafasi huku
mimi hata sihitaji nguvu nyingi kufikiri na kuamua
mimi nasema abaki huko huko au aende CUF mke wa (ccm)akagombee
 
Tunawakaribisha Chadema lakini wasije kwa lengo la kutaka uongozi, bali waje kwa lengo la kuendeleza ukombozi wa mtanzania.
 
Back
Top Bottom