Baada ya kutoswa, Sumaye sasa ateta na viongozi wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya kutoswa, Sumaye sasa ateta na viongozi wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Oct 5, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,035
  Likes Received: 37,814
  Trophy Points: 280
  Waziri mkuu mstaafu bwana Sumaye ameripotiwa kuteta na viongozi wa chadema.Hii ni baada ya kutoswa ujumbe wa NEC.

  Hata hivyo,sitashangaa kusikia Sumaye akikanusha taarifa hizi siku yoyote ile kwani ndio utamaduni wao.Tatizo wana mtazamo wa kizamani kwamba bila kupitia ccm huwezi kuwa raisi.Wako radhi kunyanyasika ndani ya ccm na sio kuwa na ujasiri wa kuhama.Wakati utafika watakuja kukubali ukweli kwamba ni makosa kuwa watumwa wa chama cha siasa.

  Kwa taarifa zaidi soma gazeti la mwananchi la leo trh 05/10/2012.

  ****************
  Mussa Juma, Arusha na Boniface Meena, Dar | Mwananchi | October 05, 2012


  SIKU chache baada ya kushindwa katika uchaguzi wa ndani kwenye nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amekutana na viongozi wa Chadema ikidaiwa kuwa ni kujadili pamoja na mengine, uwezekano wa kuhamia huko ili agombee urais katika Uchaguzi Mkuu ujao 2015.

  Sumaye ambaye anatajwa kuwa alikuwa na mpango wa kuwania urais kupitia CCM, alishindwa katika uchaguzi wa kuwania ujumbe wa Nec, baada ya kupata kura 481 dhidi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk Mary Nagu aliyepata kura 648.

  Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa Chadema, zimeeleza kuwa Sumaye hakuridhishwa na mchakato wa uchaguzi huo wa Nec na kwa matokeo hayo, alikutana na viongozi wa Chadema kujadili mustakabali wake kisiasa.

  Jana, mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya Chadema, ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alithibitisha Sumaye kukutana na viongozi wa Chadema. Hata hivyo alisema hawajafikia mwafaka.

  Alisema mawasiliano ya Chadema na Sumaye yalianza mara tu baada ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Septemba 30, mwaka huu yaliyomwengua kigogo huyo kwenye kinyang'anyiro hicho.

  "Ni kweli kuna watu wa CCM tumewasiliana nao baada ya uchaguzi ule (wa Nec) na Sumaye tunawasiliana naye pia lakini siwezi kusema tumefikia wapi," alisema mjumbe huyo na kuendelea: "Suala kwamba amekubaliwa kujiunga na Chadema au la, nadhani huu ni uamuzi wake. Ninachoweza kusema ni kwamba vikao vilikuwepo na vinaendelea kukaliwa."

  Alisema baada ya matokeo ya Hanang' na hali ya kisiasa ndani ya CCM, Chadema kimekuwa kikiwasiliana na Sumaye na kikubwa ambacho kinajionyesha ni kada huyo wa CCM kutoridhishwa na hali ya mambo ndani ya chama chake.

  Mjumbe huyo wa Chadema alisema chama hicho Wilaya ya Hanang' kinaandaa mkutano maalumu wa kuwapokea wanachama wapya wa CCM, wengi wao wakiwa baadhi ya walioanguka kwenye uchaguzi wa Nec wilayani humo.

  Habari zaidi zimeeleza kuwa Chadema kimepanga siku yoyote juma lijalo, kuwapokea wanachama wapya kutoka CCM, baadhi wakiwa wale walioshindwa kwenye uchaguzi wa ndani ya chama hicho uliofanyika wilayani Hanang'.

  Mmoja wa watu wa karibu na Sumaye alisema anachojua ni kwamba Chadema wanamtaka Sumaye na siyo Sumaye kukitaka chama hicho cha upinzani.


  "Wamekuwa wakimfuatafuata mara nyingi na mazungumzo ya aina hiyo si mageni baina ya Sumaye na Chadema. Ila ninachoweza kusema, safari hii chochote kinaweza kutokea kutokana na hasira alizonazo (Sumaye). Ngoja tusubiri, atafanya mkutano na waandishi Jumapili."

  Sumaye, Mbowe wazungumza
  Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Sumaye alisisitiza kuwa atazungumzia masuala yote yanayohusiana na uchaguzi huo wa Hanang' atakapokutana na waandishi wa habari, Dar es Salaam.


  "Nitakutana na waandishi wa habari kuzungumzia kilichotokea naomba tu mwendelee kunipa muda," alisema Sumaye na kuongeza kuwa alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda Dar es Salaam.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yeye si msemaji wa Sumaye... "Sitaki kumzungumzia Sumaye. Mimi si msemaji wake. Tumsubiri yeye azungumze kuhusu hilo."

  Kada wa CCM Hanang' anena
  Katika hatua nyingine, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Hanang', Goma Gwaltu amekionya chama hicho kuwa kisipodhibiti vitendo vya rushwa katika chaguzi zake, kitakufa.


  Gwaltu alisema jana kwamba kwa mazingira yaliyopo sasa ndani ya CCM bila hatua kali kuchukuliwa, kiongozi asiye na fedha hawezi kushika uongozi na ndiyo sababu anaungana na wana-CCM wengine katika wilaya hiyo, ambao wanafikiria kukihama chama hicho.

  "Kama wewe una nia ya kuendelea na siasa siyo rahisi kushinda hapa Hanang' ukiwa hukubaliani na watu fulani, sasa mimi naona ni bora tu kutafuta chama kingine kwani siyo dhambi," alisema Gwaltu bila kuwataja ambao wanataka kuhama CCM.

  Hata hivyo, Gwaltu alisema kwa upande wake, hafikirii kuendelea na mambo ya siasa wala kulalamika makao makuu ya CCM kuhusiana na alichokiita hujuma alizofanyiwa.

  Source: Sumaye ateta na Chadema
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Salary Slip Mh. Sumaye sidhani kama ana mvuto wa kuongeza wapiga kura, abaki tuu huko CCM atulie maisha ni zaidi ya kuwa Raisi. Hiyo network ilishindwaji kumsaidia wakati akiwa Waziri Mkuu kufikia angalau nafasi ya tatu au ya pili kwenye kura za CCM za kumsaka mgombea wa uraisi? Dr Slaa kwa wananchi wa kawaida ambao ndio wenye ufunguo wa Ikulu ana jina kubwa kuliko huyu waziri mkuu mstaafu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  Keshajichafua... Hafai
   
 4. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Kumbe!! safi sana kweli madaraka matamu bora aende hukohuko
  Mwaka 2005 NEC alikuwa wa 5 nyuma ya Kigoda kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais
  Muda bado watu viroho papo
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Kila kitu kina wakati wake...his time to lower down his ego and rest has come. If he pursues that road to opposition, must expect the worse!
   
 6. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Baada ya Kutoswa NEC....

  SUMAYE, CHADEMA WATETA

  -Ni kuhusu hatma yake Kisiasa

  Waziri Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne Fredlick Sumaye ameteta na CHADEMA juu hatma yake kisiasa baada ya kutoswa na Nec ya CCM katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni wilayani Hanang.

  Sumaye alidondoshwa na Waziri wa Uwekezaji Mary Nagu kwenye uchaguzi huo wa NEC-CCM katika kile kinachoelezwa ni kutokana na mbinu chafu za kifisadi zilizoratibiwa na EL.

  Je ni mwanzo wa vigogo wa CCM kutimkia CDM? Maana ni wazi EL na kambi yake ameiteka NEC na hatma ya kambi ya Wapambanaji wa Ufisadi iko matatani sasa. Wachambuzi wa mambo, wanampa nafasi EL katika kuiteka NEC na hata kuteuliwa kugombea urais kupitia CCM mwaka 2015.
   
 7. o

  obwato JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sumaye hana moral authority wa kuwa mtaji kwa cdm,alipokuwa madarakani kajilimbikizia ardhi hovyo kama Kibaigwa na Mvomelo hawapendi ata kulisikia hilo jina na alikuwa na majibu ya dharau kwa wapinzani. Kwa nn asitulie ajilie marupurupu yake ya ustaafu? Kama ccm wameshindwa kumpa japo uNEC cdm watampa cheo kipi? Labda udiwani.
   
 8. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Apewe kadi, but sio uongozi. Afanye kazi kama wengine to earn Uongozi
   
 9. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  BIG NO!

  Huyo sumaye abaki huko huko kwanza ana kashfa nyingi na wasije wakatumia kashfa kukichafua na chama chetu kipenzi, pia nakumbuka miaka ya nyuma alitumika kuuwa watu kipindi kile yy ni waziri mkuu.
  Pia hana mvuto wa kisiasa labda kwenye familia yake.

  Hatutaki magamba ya kobe CHADEMA.
   
 10. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  mkuu huyu hata udiwani hafai maybe balozi wa nyumba kumi japo sidhan sana kama atafaa.
   
 11. C

  Concrete JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Huenda ana mpango wa kugombea udiwani kwenye kata mojawapo huko Hanang,

  Huu utakuwa ni mwanzo mzuri kwake kwa kuamua kutafuta chama chenye nguvu ili kupata ushindi.
   
 12. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Matatizo ya kuunga unga elimu ndo hayo, mara diploma ya kilimo, mara sijui anasoma OPEN, mara aonekane University Computing Centre(UCC) kusoma short course ya Computer, angetulia tu Pwani na Ng'ombe wake akavune maziwa.
   
 13. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Lakini SLAA kwa kinywa chake alitamka na hapa nanukuu "TUNAWAKARIBISHA WALE WATAKAOSHINDWA CCM" wachukue
  tu huo mfupa, labda wao wanauweza.
   
 14. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Anataka Urais, baaaaaaaaaaaaaaaaaaaaas.
   
 15. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Lakini Uwaziri Mkuu unaweza kumbeba akakubalika CDM.
   
 16. O

  Omokora Nyangi Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tatizo kubwa la Sumaye ni "struggle for power", na hili ni tatizo kwa viongozi wengi wa Africa, Asia na Latin America. Ndio maana mwisho wa maisha ya watu kama yeye huwa wa aibu.

  Namshauri akae apumzike kama Warioba na Msuya walivyotulia. Na akumbuke nini kiliwatokea Dr. Salim na Malecela mara walipotaka kupewa dhamana ya kuongoza tena na tena! Asidhani ni yeye tu awezaye kuleta mabadiliko nchi hii, nchi itaendelea au isiendelee bila kujali yeye ni kiongozi au la, na asithubutu kulipa kisasi kwa mahasimu wake!
   
 17. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Sisi tutaongea tu, lakini ndo hivyo tayari wameshateta, tusubiri kitakachojiri.
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hana mvuto tena apumzike tu ale mafao yake.
   
 19. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Omokora Nyangi

  Hivi huwezi kugombea Urais hadi uwe mjumbe wa NEC taifa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Sumaye ni bora ahamie CDM kiakili lakini kimwili abaki ccm ili akibomoe vizuri chama chake.Ajitahidi awe pandikizi huku wafuasi wake wakihamia cdm, yeye awe mtoa siri kwa cdm za ccm atasaidia sana mabadiliko ya demokrasia
   
Loading...