Baada ya kupata taste ya kumiliki gari, mwezi January naachana na babywoka nanunua Subaru Forester

Mlolongo

JF-Expert Member
Jul 4, 2019
3,274
5,898
Nimejifanyia self-assessment katika kipindi cha miezi mitano nimeona kinatosha kunipa picha ya utamu na uchungu wa kumiliki gari.

Wakati naagiza gari uchumi wangu haukua stable kivile, plus little (almost none) experience ya kumiliki gari ikapelekea nikaagiza babywoka.

Miezi minne kutoka sasa kama mipango yangu ya kiuchumi ikienda sawia basi nina mpango wa kuachana na babywoka yangu na kuagiza Subaru Forester.

Kwanza nilikua nishapanga kuwa gari yangu ya pili kumiliki lazima itakua Toyota Premio New model. Naipenda sana hii gari, it is my dream car.

Screenshot_20201001-165940_1601560816561.jpg

Juzi wakati napiga story na rafiki yangu mpambanaji mwenzangu kuhusu utafutaji wa pesa. Sasa nikachomekea story za magari, nikamuuliza what's is your dream car? Akasema Subaru Forester!

Mie nikamwambia naizimia sana Premio New Model. Jamaa akasema mbona napenda magari ya kike hayo. Akasema 'Saloon' cars zote (Premio, Allion, Cresta nk) ni gari za kike.

Wanaume wapambanaji watafutaji wanamiliki SUV (xtrail, forester, Prado nk). Daaah baada ya mabishano meengi mchizi akanishawishi kuwa kama kweli nina ndoto za mbali, basi niachane na habari za Saloon Cars. Hizo tuwaachie Ulaya na Japan huko wenye barabara kama mkeka.

Inshaallah, napambana kweli kweli kufikia January mwishon au February 2021 niuze hiki kibebiwoka changu nivute mnyama Forester (nikipata ya 2010 mpaka 2015 hivi sio mbaya)

Screenshot_20201001-170227_1601560980149.jpg

ADDITIVE POINT:
Hapo haitakua mwisho wa kupambana. Roho yangu itasuuzika sana siku nikinunua Volkswagen Touareg.

Yaani nataka nipambane mpaka yule Ex-girlfriend wangu aliyeniacha kwenye mataa eti kisa nachelewa kumaliza chuo, akaolewa na yule mshikaji anafanya kazi wizara ya mipango Dodoma siku akiniona aseme "Yereuwiiiii"
 
"Yaani nataka nipambane mpaka yule Ex-girlfriend wangu aliyeniacha kwenye mataa eti kisa nachelewa kumaliza chuo, akaolewa na yule mshikaji anafanya kazi wizara ya mipango Dodoma siku akiniona aseme "Yereuwiiiii"

Nilipofika hapa nikagundua wewe bado MVULANA.
 
Sedans sio gari za kike Bana!! Cresta,allion na premio unaziita gari za kike? Basi huyo jamaa yako bado hayajui Magari kabisa na sidhani kama umeshawahi kuendesha Safar ndefu za mikoani ili upate uzoefu wa sedans zinavyonyanyasa hizo SUV..
Kwa taarifa yako hiyo cresta ni bonge moja la ndinga kushinda Subaru forester pia Kwa mtu anayejua Magari ukimwuliza toleo lipi la Subaru forester limetulia atakuambia ni second generation..

Engine capacity zote zinafanana pia second generation ya Subaru ndiyo babu-kubwa kuliko hiyo matoleo ya 2008,nimeendesha Subaru forester crosssport hii gari ni noma kushinda hiyo New model
 
kweli second generation i ponge la ji subaru, ni tamu sana na limetulia kwa rod arifuuuuuuu
 
Yaani nataka nipambane mpaka yule Ex-girlfriend wangu aliyeniacha kwenye mataa eti kisa nachelewa kumaliza chuo, akaolewa na yule mshikaji anafanya kazi wizara ya mipango Dodoma siku akiniona aseme "Yereuwiiiii"
Aiseee🤦🏽‍♂️😂😂
 
Back
Top Bottom