Baada ya kupandisha nauli, Mishahara nayo itapanda?

beeper

JF-Expert Member
Dec 30, 2013
251
105
Habari,

Hivi SERIKALI inapopandisha bei za nauli MISHAHARA nayo inaangaliwa? Watu bidhaa wanafaidika kwa kuongeza bei lakini mishahara ipo palepale mfano sukari ilipopanda haikushuka ilipo. Tofauti ya kuoanda ni kubwa.

Wiki hii mmetangaza kupanda kwa nauli lakini hali za mishahara kwa sisi makabwela tunatumia huo usafiri ipo palepale. Naomba SERIKALI iliangalie hili.
 
Hizo nauli buana yaani unaweza ukahamia Burundi kweli. Eti nauli ya Dodom Iringa ni kubwa kuliko Dodoma Mbeya?
Dodoma Singida nauli yake ni kubwa kuliko Dodoma Mwanza?
Tz kuna maajabu mengi sana kuzidi Serengeti.
Sababu ni utofauti wa Bei ya Mafuta ndugu mteja, tafadhari taja eneo ulipo unasafiri kutoka wapi kuelekea wapi?
 
Hivi Wanavyopanga hizo nauli hua wanashirikisha watumiaji? ,Nauli Iringa Shinyanga tulikua tunasafiri kwa tsh elf 35, l Ila sasa hivi ni elfu 60,najaribu kucalculate hapa lakini sielewi.

Nashauri serikali iunde chama cha abiria Tanzania,ili na sisi tupate Msemaji
 
Dar Mtwara thalathini na titha au aru40 kutoka ishirini na TANU😂😂

Yaani 25-40😂=-15 Hii nchi hapana Kwa kweli... Ongezeko la sh100 ya mafuta imeleta balaa
 
Habari,

Hivi SERIKALI inapopandisha bei za nauli MISHAHARA nayo inaangaliwa? Watu bidhaa wanafaidika kwa kuongeza bei lakini mishahara ipo palepale mfano sukari ilipopanda haikushuka ilipo. Tofauti ya kuoanda ni kubwa.

Wiki hii mmetangaza kupanda kwa nauli lakini hali za mishahara kwa sisi makabwela tunatumia huo usafiri ipo palepale. Naomba SERIKALI iliangalie hili.
Kwani watu wote hapa nchini wanalipwa mshahara kila mwezi???
 
Habari,

Hivi SERIKALI inapopandisha bei za nauli MISHAHARA nayo inaangaliwa? Watu bidhaa wanafaidika kwa kuongeza bei lakini mishahara ipo palepale mfano sukari ilipopanda haikushuka ilipo. Tofauti ya kuoanda ni kubwa.

Wiki hii mmetangaza kupanda kwa nauli lakini hali za mishahara kwa sisi makabwela tunatumia huo usafiri ipo palepale. Naomba SERIKALI iliangalie hili.
Ukiongea uhusu mshahara, unakua unabagua kundi kubwa sana la watanzania ambao wanapambana kila siku kujipatia mkate wa kila siku.

Fikiria mtu anatoka mbagala kwenda kufanya kazi Kariakoo kazi yenyewe ni umachinga kwa siku anaweza akauza bidhaa na kupata faida ya 5K labda. Je, mtu huyu ataweza kumudu gharama za usafiri kweli!?!
 
Dar mwanza kutoka ilipokuwa awali 45 ikapanda to 67 sahivi ati 78 bado naona kama ni muujiza!,ila nyie ccm inatuona maboya nahisi Kuna namna tunatakiwa tufanye si bure!
 
LATRA kupandisha nauli ni sahihi kabisa kutokana na bei ya mafuta kupanda ila pia wawe wanashusha bei ya mafuta inaposhuka. Kama mamlaka yao haina kushusha basi wasipandishe nauli.
 
Back
Top Bottom