Baada ya kumkopesha pesa amenizushia nimemtishia maisha na kumbaka

Dunia hadaa, walimwengu shujaa.

Wanawake waache tu wanipitie mbali kabisa.
 
Mpnz wng hawezi kunikopesha hela abadan..na wala mm siwezi
 
Story ndefuu...msamehe then mpotezee kwa akiri zake huyoo nilivyompima anaweza Hata kuja kukuitia mwizi Na ukafa....sio mwema kwako..kasahau kama shida sio ya siku moja...Msahau IPO siku atakukumbuka.
kweli kabisa ipotezee tu usije ukafanyiwa kama ya yule mshikaji wa st augustine kule mwanza
 
Nashukuru kupita hapa, mm wangu anataka nimkopeshe lak 5 kutokana na hilo lilikupata itabidi siku ya kumpa nimwite mjumbe
 
Hata hvo unaonekana mbahr ndio mana kaamua kusepa. Ulikuwaga unamkula kwa mkopo ama hata elf 20 tu kumpa anaoooombaa kama anadai marejesho bwana.

Kwa nini asiseme kama hataki "mkopo" kuliko kumsingizia ubakaji.

Kila siku nalia kwa nini nyumba za ibada zinazidi kujengwa na kufulika waumini lakini hatuoni jamii ikibadilika.
 
Nilichojifunza mimi juu ya wanawake akikuomba umkopeshe ni anakutega tu na ukimpa hupaswi kumdai kwa kua ni mpenzi wako.
 
Mbona kesi yako cha mdoli sana hyo. Wengine wanatoa game hata mara 3 ila sikilizia huo mzinga wake mbeleni huko.

Istoshe mbona case iko wazi. Kwani ulifkiri unamgegeda bure bure. Hapo ni kwamba umelipia huduma.

Wanajiuza kwa njia nyingi hawa. Wake up young man !!!

Hapo kwenye kukuchafulia jina huyo binti ni mburulaz i.e. Elimu Ndogo. Next tym angalia na wanawake waku date. Know ur Standards.
 
Mkuu pole sana kwakuharibiwa jina mtaani!! Mpenzi au mchumba hakopeshwagi pesa ila anapewa. Hata siku moja usijaribu kumkopesha mchumba..wewe ukimpa jua tu umemsaidia.
Mimi nakushauri achana nae na usonge na maisha yako na ujifunze kwa yaliyokukuta
 
Mimi sikopeshi mwanamke yoyote.. Usijatibu na wala usithubutu kukopesha mwanamke... Hata nenda kaZini .. Hio pesa isamehe ni malipo ya kulala na mtoto wa watu kabla hujalipa mahari
 
Ila kijana una sura ngumu kweli, unaanzaje anzaje kumdai mke wako? Msichana unayelal naye ndani ni kama mkeo.. Akikuambia kanunua chupi utasemaje?
Acha ukauZu..
Mnamo mwezi wa tatu nilianzisha mahusiano ya kimapenzi na msichana ambaye tunafanya naye kazi sehemu moja, kiukweli mapenzi yetu yalikuwa matamu kama mjuavyo penzi changa linavyonoga na kushamiri.

Huyu mwanamke yeye bado anaishi kwao na mie nimepanga chumba changu so mara nyingi tulikuwa na kawaida ya kulala pamoja mara kwa mara tunapotoka au kama tuko off basi anakuja kwangu na tunaspend siku pamoja.

Kiukweli hatukufuhamiana sana kiundani sana maana tulikutana tu kazini na kutoka napoishi hadi kwao ni kama 15km , kwahyo tulikutana tu kazini na baada ya kuwa marafiki ndani mwezi kama mmoja ndio tukazama kwenye mapenzi. Kiukweli tulipendana sana maana binti alikuwa mchangamfu, mwelewa, cute na alikuwa talkative vitu ambavyo nilimpenda sana.

Mwanzoni mwa mwezi wa sita tukiwa chumbani tumelala ndipo akanieleza kuwa anahitaji nikopesha laki mbili na nusu mwisho wa mwezi atanirudishia, nilipomuuliza za nini akasema kuwa anataka akajiunge na chuo fulani cha masuala ya Utalii kwahyo alikuwa amepungukiwa na kama laki na nusu na hela za maandalizi mengine kwa ajili ya chuo.
Ni kweli wiki kadhaa zilizopita aliwahi kuniambia kuwa anataka akasome chuo so nilikuwa aware na mpango wake.

Nilijifikiria nimpe hyo hela au nisimpe maana kiukweli nilikuwa nampenda na tulikuwa tumezoeana sana na sikuhisi kuwa anadanganya au ana lengo gani.
Basi nikamwambia nikamwambia hela anyoitaka sina ila nina Laki mbili tu so nikampa kwa masharti kuwa mwezi ajao atairejesha , akakubali vizuri tu.

Zilipita kama siku tano hivi akaniambia kuwa anahitaji tena nimpe elfu 20 ana shida nayo, nikamuuliza ya nini tena wakati juzijuzi nimempa laki 2 ? akasema Ana shida nayo tu hawezi kuniambia, nami nikamwabie siwezi kumpa hadi aniambie,
Aliposisitiza sana nikamwabia mie saiv nimeishiwa hela na nimebakiwa elfu 40 tu ya akiba ( nilisema hvo kumdanganya ).

Baada ya kuona anakomalia sana nimpe elfu 20 , nikamwambia siwezi kumpa maana ndio hela niliyobakiwa nayo, tena nikamwambia labda nikupe ukae nayo wewe mie nikihitaji nitakuwa nachukua kwako.

Niliamua kumpa tena ile elf 40 kama kumpima uaminifu wake na pia kumfanya asinisumbue kuniomba pesa.

Baada ya siku kama tatu alinipigia simu akiomba achukue elf 25 kwenye ile elf 40 niliyompa akae nayo, mie nikamwambia asitoe hata mia maana tulishaelewana tayari, aliposisitiza sana achukue ( kwa alivyokuwa anakomalia nilijua ameshaitumia ila anataka comfirmation tu ).
Nilimzuia asichukue akakubali, so baada ya siku mbili nilimwabia kesho wakati anakuja kazini aniletee ile pesa elf 35 nina kazi nayo, kwanza aliniruka akasema hana na akakata simu.

Kesho yake kazini hakuja asema anaumwa. nilipomwabia vipi ile hela akasema aliitumia yote labda anitafutie nyingine.
Kwanza akawa ananijibu kwa mkato kitu ambacho sio kawaida yake.

Kesho yake alipokuja job akawa ananikwepa hata kuongea, ilibidi nimsubiri hadi wakat tunatoka kazini nilimchukua kwa nguvu hadi kwangu maana sio mbali kutoka kazini.
Baada ya kujitetea sana akaniambia tusubiri mwisho wa mwezi maana ilibaki week tu, nikamkubalia,

Cha ajabu mwezi ulipoisha hakunilipa ile laki 2 pamoja na ile elf 40, hapo sasa na mahusiano yakawa ya kuzinguana maana mie nikawa mkali sasa mpaka akawa ananikwepa.

Siku moja asubuh nikapigiwa simu na mwenyekiti wa mtaa akiniambia nifike kwake muda huo kuna tatizo, nilipofika nikamkuta huyo mpenzi wangu akiwa na kaka na mdada mwingine, wote kaka na yule tunafanya kazi sehemu moja.

Mwenyekiti wa mtaa akaniambia huyo dada (mpenzi wangu ) ameleta mashitaka kuwa nimemtishia maisha na akadai kuwa niliwahi kumteka na kumbaka, nilishangaa sana, mie nikajitetea kuwa huyu ni. mpenzi wangu na namdai Lak240,000/=

Yulee mpenzi wangu akaniruka kuwa simdai hiyo bali namdai elf 40 , mie nikamuuliza kama anadai nilimbaka ilikuwaje nikamwazima elf 40?? basi alikosa majibu na kwa kuwa tulipeana wawili chumban hakukuwa na ushahidi na alikiri mwenyewe kuwa nilimpa elf 40 nikakubali anilipe.

Basi wakaomba walupeleke kwanza nyumban kwao ili wajue kuwa mtoto wao kalipishwa faini na wakaahidi kurudi Kesho yake ili tuyamalize.

Baada ya hapo hawakurudi tena maana yake nikawa numpoteza pesa yangu na amenichafulia jina mtaani huyu mwanamke,

Nilipokuja kufatilia ndio nikagundua kumbe aliwahi kuolewa na ana mtoto mmoja!!!

Wadau nimfanyaje huyu mwanamke ili angalau nirudishe heshima yangu aliyonichafua
 
Ww utajapoteza uhai kuwa makini na hawa viumbe.

Imeandikwa ishini nao kwa akili ww unatumia masaburi kuishi nao itakula kwako
 
Back
Top Bottom