Habari wakuu,
Huwa napenda kutoa baadhi ya matukio ya maisha yangu ili kupata ushauri na pia kama rejea au funzo kwa watu wengine katika jamii au jf
Kuna kipindi nilikuja humu kuomba ushauri wa namna ya kuifanya familia yangu kuwa familia kubwa yenye kuigwa, nashukuru nilipata ushauri na mwingine niliufanyia kazi miongoni mwao ni kuwa nilifanikisha kukaa na wanafamilia tukatengeneza katiba na kuchaguana viongozi ili kuendesha mirathi kimfumo wa utawala na demokrasia
Hivyo tulianza utekelezaji ambapo mwenyekiti ndio mtu mkubwa katika kutekeleza majukumu ya kifamilia endapo alichaguliwa kwa kura ya siri na pia alikuwa sio mkubwa wetu kwa kuzaliwa pamoja na viongozi wengine tukapeana majukumu mbalimbali katika kusimamia mirathi na kuanzisha miradi mingine kutokana na ukusanyaji wa mapato
Mimi nilikuwa miongoni mwa viongozi pia kwani katika kuchaguana hakuna aliyeachwa bila cheo chochote yani wote tulichaguana kulingana na nafasi za uongozi na majukumu, kwa upande wangu nilikuwa mkusanyaji wa pesa ambapo nipo na dada yangu ambae yeye ndio mkusanyaji mkuu mimi ni msaidizi wake
Sasa kilichofanya nijitoe katika uongozi ni baada ya kuona kaka zetu wakubwa kiumri na sio kivyeo (japo mmoja ndio mwenyekiti yani anaefuatia kwa ukubwa) wanahujumu jitihada za ukusanyaji ambapo ili wewe mkusanyaji uipate hiyo pesa iingie kwenye mfuko wa familia mpaka ugombane nao maana wanataka kuimanupulate ili kuzurumu au kuchakachua kabla haijaingia kwenye mfuko wa familia
Kumbuka katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi tumefanikiwa kupata wawekezaji wa eneo letu na walijenga flemu za biashara kwa mikataba na pia kuna maeneo mengi tulipangisha kwa wafanyabiashara hivyo mapato yameongezeka tofauti na kipindi cha nyuma kabla ya uongozi
Sasa baada ya kujiuzulu au kujitoa katika uongozi kwa sababu nilizotaja hapo juu ndugu zangu hawanishirikishi chochote kinachohusu familia hata kama hakigusi mirathi moja kwa moja mfano matukio ya kifamilia kama harusi, ugonjwa na hata au baadhi ya misiba. Yani kujitoa kwenye uongozi ni kana kwamba nimejivua undugu hizi jamii zetu shida sana
Nini maoni yako mdau mimi ndio mwenye shida au ndugu wa familia karibu kwa ushauri