Baada ya kujitenga na mirathi ndugu zangu wamenitenga

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
5,557
Reaction score
8,195
Habari wakuu,

Huwa napenda kutoa baadhi ya matukio ya maisha yangu ili kupata ushauri na pia kama rejea au funzo kwa watu wengine katika jamii au jf

Kuna kipindi nilikuja humu kuomba ushauri wa namna ya kuifanya familia yangu kuwa familia kubwa yenye kuigwa, nashukuru nilipata ushauri na mwingine niliufanyia kazi miongoni mwao ni kuwa nilifanikisha kukaa na wanafamilia tukatengeneza katiba na kuchaguana viongozi ili kuendesha mirathi kimfumo wa utawala na demokrasia

Hivyo tulianza utekelezaji ambapo mwenyekiti ndio mtu mkubwa katika kutekeleza majukumu ya kifamilia endapo alichaguliwa kwa kura ya siri na pia alikuwa sio mkubwa wetu kwa kuzaliwa pamoja na viongozi wengine tukapeana majukumu mbalimbali katika kusimamia mirathi na kuanzisha miradi mingine kutokana na ukusanyaji wa mapato

Mimi nilikuwa miongoni mwa viongozi pia kwani katika kuchaguana hakuna aliyeachwa bila cheo chochote yani wote tulichaguana kulingana na nafasi za uongozi na majukumu, kwa upande wangu nilikuwa mkusanyaji wa pesa ambapo nipo na dada yangu ambae yeye ndio mkusanyaji mkuu mimi ni msaidizi wake

Sasa kilichofanya nijitoe katika uongozi ni baada ya kuona kaka zetu wakubwa kiumri na sio kivyeo (japo mmoja ndio mwenyekiti yani anaefuatia kwa ukubwa) wanahujumu jitihada za ukusanyaji ambapo ili wewe mkusanyaji uipate hiyo pesa iingie kwenye mfuko wa familia mpaka ugombane nao maana wanataka kuimanupulate ili kuzurumu au kuchakachua kabla haijaingia kwenye mfuko wa familia

Kumbuka katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi tumefanikiwa kupata wawekezaji wa eneo letu na walijenga flemu za biashara kwa mikataba na pia kuna maeneo mengi tulipangisha kwa wafanyabiashara hivyo mapato yameongezeka tofauti na kipindi cha nyuma kabla ya uongozi

Sasa baada ya kujiuzulu au kujitoa katika uongozi kwa sababu nilizotaja hapo juu ndugu zangu hawanishirikishi chochote kinachohusu familia hata kama hakigusi mirathi moja kwa moja mfano matukio ya kifamilia kama harusi, ugonjwa na hata au baadhi ya misiba. Yani kujitoa kwenye uongozi ni kana kwamba nimejivua undugu hizi jamii zetu shida sana

Nini maoni yako mdau mimi ndio mwenye shida au ndugu wa familia karibu kwa ushauri
 
Mambo ya mirathi kipengele sana, wenye roho ndogo wanatoana hata uhai..

Kabla ya kujitoa uliwaita ndugu zako wote, uliwaeleza kinagaubaga, mbivu na mbichi zijulikane?
Sikuwaita wote ila niliwaambia jinsi tunavyopata tabu kukusanya pesa na jinsi wakubwa wanvyohujumu shida ni kuwa wakubwa zetu wanaogopeka na baadhi ya wanafamilia kwahiyo ukiwakazia wewe ndio waonekana hero
 
Kuna familia ya rafiki yangu wao wamegawanyika makundi mawili.

Ndani na nje ya nchi.

Wale wa nje ya nchi wakawaambia wenzao kuwa hawataki chochote waendelee na mirathi.

Hivyo wale wa ndani wakabeba vyote .

Sometimes inategemea na makuzi.

Hao wa nje 70 % ya maisha yao ilikuwa nje ya nchi so nyumbani hawakuona umuhimu wowote.
 
Kwanini hazina mashiko mkuu unajua kugombana kisa pesa sio kuzuri
Sometimes inabidi ujifunze kuvumilia naelewa sana unachokiandika na najua maumivu unayoyapata ila kukutenga haina maana kwamba wamekusahau ila watakua wamepewa maelezo negative kuhusu wewe ndio maana wengine wakafuata aliewaelekeza ndio mwenye makosa sio wewe ndugu, wewe sio kosa lako kuachia ngazi na kutokujihusisha na makusanyo ya hizo fedha ila kosa ni kuwawekea ngumu hao ndugu zako uliowabaini km ni wabadhirifu wa mali zenu za mirathi na kutokuwepo kwako wewe ni nafuu kwao ndio maana wanakuweka mbali ili waendelee kupiga sababu ukiweka karibu utawasanua wengine sasa mkosanuka wengi huoni kwamba itakua shida?

Imagine familia ina watu km wewe 8 na jumla mpo 10 hao kaka zako wawili wapigaji unahisi watapumua si patachimbika? Ulichotakiwa kufanya ni kuweka kikao nao km kawaida na usingejivua kwanza ungeeleza ukweli wote then ungeeleza kwamba km hii hali itaendelea namna hii basi mimi nitajivua hili koti la uongozi maana linanishinda, lakini umechelewa kufanya hivyo sasa cha kufanya ni wewe ndio unaetakiwa kurudi na kuweka mambo sawa sawa na kueleza ukweli ili watu waelewe kwamba walichoambiwa sio ukweli wewe kukaa mbali na kukaa kimya hujui labda wao wameambiwa wewe ndio Mwizi mkubwa wa mapato ya familia unakusanya pesa unazila unajuaje?

Ndio chanzo cha kukuangalia vibaya sababu ya kile walichoambiwa kuhusu kwa namna negative sio positive ndio wanasemezana tulijua yule mtu mzuri kumbe anakusanya pesa anakula mwenyewe pesa zetu za miradi yeye anazitafuna bila aibu? Hapo cha kufanya anza kujenga ukaribu rudi kwenye vikao vyenu ukaeleze ukweli maana watu washapewa sifa mbaya kuhusu wewe ndio maana wamekuweka kando. Pole sana.
 
Ndio chanzo cha kukuangakia vibaya kumbe tulijua yule mtu mzuri kumbe anakusanya pesa anakula mwenyewe pesa zetu za miradi yeye anazitafuna bila aibu? Hapo cha kifanya anza kujenga ukaribh rudi kwenye vikao vyenu ukaeleze ukweli maana watu washapewa sifa mbaya kuhusu wewe ndio maana wamekuweka kando. Pole sana.
Dah kweli hasira amekimbi kabla hajaweka mambo wazi ili mbivu na mbichi zijulikane
 
Kwanini hazina mashiko mkuu unajua kugombana kisa pesa sio kuzuri
Sasa kama mnagombana na mwisho wanalipa kuna shida? Huenda wewe unavijihela kidogo kwahiyo unataka wenzako walipe ontime wakati wanaunga unga maisha lazima wavumilie kidogo. Afu mambo ya kuzila zila kwa mwanaume hayapendezi. Rudi kwenye familia
 
Ungewaita na kuwachana wote kwa pamoja..
Mkuu sikuwaita kwasababu wanajua na nilikuwa nawasiliana nao mara kwa mara wanafamilia wote na ndio utaratibu tulioweka ili kuwahabarisha makusanyo au uwekezaji mpya unaotokea

Hivyo kila tunapopata changamoto huwa tunawashirikisha wanafamilia wote kwa simu na hadi najiuzulu niliwaambia mmoja mmoja kwa kutumia simu lengo lilikuwa sitakutaka kuendelea kugombana na kaka zangu kwa ajili ya mirathi
 
Kuna familia ya rafiki yangu wao wamegawanyika makundi mawili.

Ndani na nje ya nchi.

Wale wa nje ya nchi wakawaambia wenzao kuwa hawataki chochote waendelee na mirathi.

Hivyo wale wa ndani wakabeba vyote .

Sometimes inategemea na makuzi.

Hao wa nje 70 % ya maisha yao ilikuwa nje ya nchi so nyumbani hawakuona umuhimu wowote.
Sometimes bora hivyo tu uwaachie ving'ang'anizi wa mirathi wale
 
Sometimes inabidi ujifunze kuvumilia naelewa sana unachokiandika na najua maumivu unayoyapata ila kukutenga haina maana kwamba wamekusahau ila watakua wamepewa maelezo negative kuhusu wewe ndio maana wengine wakafuata aliewaelekeza ndio mwenye makosa sio wewe ndugu, wewe sio kosa lako kuachia ngazi na kutokujihusisha na makusanyo ya hizo fedha ila kosa ni kuwawekea ngumu hao ndugu zako uliowabaini km ni wabadhirifu wa mali zenu za mirathi na kutokuwepo kwako wewe ni nafuu kwao ndio maana wanakuweka mbali ili waendelee kupiga sababu ukiweka karibu utawasanua wengine sasa mkosanuka wengi huoni kwamba itakua shida?

Imagine familia ina watu km wewe 8 na jumla mpo 10 hao kaka zako wawili wapigaji unahisi watapumua si patachimbika? Ulichotakiwa kufanya ni kuweka kikao nao km kawaida na usingejivua kwanza ungeeleza ukweli wote then ungeeleza kwamba km hii hali itaendelea namna hii basi mimi nitajivua hili koti la uongozi maana linanishinda, lakini umechelewa kufanya hivyo sasa cha kufanya ni wewe ndio unaetakiwa kurudi na kuweka mambo sawa sawa na kueleza ukweli ili watu waelewe kwamba walichoambiwa sio ukweli wewe kukaa mbali na kukaa kimya hujui labda wao wameambiwa wewe ndio Mwizi mkubwa wa mapato ya familia unakusanya pesa unazila unajuaje?

Ndio chanzo cha kukuangalia vibaya sababu ya kile walichoambiwa kuhusu kwa namna negative sio positive ndio wanasemezana tulijua yule mtu mzuri kumbe anakusanya pesa anakula mwenyewe pesa zetu za miradi yeye anazitafuna bila aibu? Hapo cha kufanya anza kujenga ukaribu rudi kwenye vikao vyenu ukaeleze ukweli maana watu washapewa sifa mbaya kuhusu wewe ndio maana wamekuweka kando. Pole sana.
Mkuu umeongea vyema kiuhalisia wale ndugu wakubwa kutokuwepo kwangu kwenye uongozi ndio wamefurahia ili waendelee kupiga fix zao kwenye Ile mirathi na walikuwa wakifanya hivyo huko nyuma kabla ya uongozi

Sema Mimi sikutaka kugombana nao kwa ajili ya mirathi kwani uongozi sio kulazimishana na wala sio kujiona hero maana kitu kibaya kikikutokea hao wanaokuona hero watakugeuka japo ulikuwa unawapigania wao

Kuhusu kuwaambia changamoto wote nimewaambia ila pia hawana la kufanya wengine ilimradi wapo tu nao wanaacha liwalo na liwe
 
Mkuu sikuwaita kwasababu wanajua na nilikuwa nawasiliana nao mara kwa mara wanafamilia wote na ndio utaratibu tulioweka ili kuwahabarisha makusanyo au uwekezaji mpya unaotokea

Hivyo kila tunapopata changamoto huwa tunawashirikisha wanafamilia wote kwa simu na hadi najiuzulu niliwaambia mmoja mmoja kwa kutumia simu lengo lilikuwa sitakutaka kuendelea kugombana na kaka zangu kwa ajili ya mirathi
Wewe waite, kisha uwachane wote, ishu ilipoanzia, ulipojitoa na wanayokufanyia, wachane hao wengine kwa uoga wao na unafiki, mi huwa sicheki na kima, waeleze ulichokuwa unachokipambania ni haki ya wote, na kama wameamua kukutenga kisa uhalia na iwe hivyo, ila haki zako unazitaka wasilete ukima.
 
Sasa kama mnagombana na mwisho wanalipa kuna shida? Huenda wewe unavijihela kidogo kwahiyo unataka wenzako walipe ontime wakati wanaunga unga maisha lazima wavumilie kidogo. Afu mambo ya kuzila zila kwa mwanaume hayapendezi. Rudi kwenye familia
Nahisi hujanipata vema mkuu jaribu kusoma tena tupate kwenda pamoja
 
Kuhusu kuwaambia changamoto wote nimewaambia ila pia hawana la kufanya wengine ilimradi wapo tu nao wanaacha liwalo na liwe
Umewaambia ukiwa wapi? Nimekwambia uwaambie kwenye kikao na hao waizi waulizwe kwamba unachosema ni ukweli au sio kweli? Najua wataeleza vizuri au unaogopa kurupushani nao wanaweza wakakushika shati?
 
Wewe waite, kisha uwachane wote, ishu ilipoanzia, ulipojitoa na wanayokufanyia, wachane hao wengine kwa uoga wao na unafiki, mi huwa sicheki na kima, waeleze ulichokuwa unachokipambania ni haki ya wote, na kama wameamua kukutenga kisa uhalia na iwe hivyo, ila haki zako unazitaka wasilete ukima.
Tuliweka utaratibu wa vikao vya kila mwaka na tulikaa vikao viwili toka tuanze nilitarajia kikao cha mwaka huu ambacho kilitakiwa kikaliwe kwenye sikukuu ya iddi niwepo nieleze ukweli badala yake kikao hakikukaliwa
 
Umewaambia ukiwa wapi? Nimekwambia uwaambie kwenye kikao na hao waizi waulizwe kwamba unachosema ni ukweli au sio kweli? Najua wataeleza vizuri au unaogopa kurupushani nao wanaweza wakakushika shati?
Vikao vyenyewe siku hizi hata sishirikishwi na vile vya kila mwaka ambavyo tuliviweka ambapo ndugu wote tunakuwepo hata aliembali lazima aje havikaliwi cha mwaka huu naona kimepita kimyakimya
 
Back
Top Bottom