Baada ya kazi unaenda nyumbani au unasogeza muda sehemu gani na kwanini?

shadownet

Senior Member
Aug 4, 2015
133
674
po.png

kuna wafanyabiashara na wafanya kazi wengi wa serikalini ambao muda wa kutoka huwa ni saa kumi hadi saa 12 jioni ambao wana maamuzi mawili, kunyoosha moja kwa moja nyumbani ama kwenda sehemu kuoteza na kusogeza muda ili wafike nyumbani usiku, pia kuna ambao hufanya shughuli za kujiendeleza kama kusoma ama kufatilia miradi yao.

hao kundi la pili ambao wanapoteza muda mara nyingi wakitoka kazini wanaenda bar kujibutua, wanaenda kwa michepuko yao kuomboleza kifo cha mende, wanaenda kubeti, n.k pia kuna wengine husogeza muda bila kutenda dhambi, hawa huenda kufanya mazoezi, kucheza draft, n.k

JE, WEWE UKITOKA KAZINI UNAENDAGA WAPI
 
Nawahi kuvuta Bange home nipate fikra sahihi na utulivu wa kujua wapi nimekosea na wapi nisahishe.
 
Umegusa palepale napopataka
na mimi kuna jambo nataka kuweka
kila kukicha wanaochelewa kurudi wanaongezeka
hili nalisema kwa uhakika

kwa utafiti wangu nyumbani ni pachungu siku zote hasa kwa wanaume, akiwa kijana ataona nyumbani kwa wazazi wake hakuna uhuru ataenda kupanga geto, akihamia geto au hata nyumba yake ataoa ila bado ataona anakosa uhuru hivyo anaweza kufungua tawi lengine na kujikuta kaingiwa na tamaa ya kuweka chombo kwenye tawi, na hili tawi akilichoka anafungua lingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom