Baada ya hotuba ya mwisho wa mwezi ya JK, nini sasa kifanyike? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya hotuba ya mwisho wa mwezi ya JK, nini sasa kifanyike?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mystery, Oct 2, 2012.

 1. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,983
  Likes Received: 6,760
  Trophy Points: 280
  Tumemsikia Rais wetu akilihutubia Taifa mwisho wa mwezi, kupitia vyombo vya habari vya Televisheni na redio, katika utaratibu aliojiwekea yeye mwenyewe. Baada ya kumsikiliza, tulivyomuelewa ni kama vile anaona hakuna makosa yoyote ya polisi katika mauaji ya raia wasio na hatia, katika matukio mbalimbali yaliyotokea siku za karibuni, hususani katika mikutano ya kisiasa. Akahalalisha matumizi hayo kwa madai kuwa Jeshi la polisi linatimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Kutokana na maelezo ya Rais, sasa ndiyo tumepata jawabu, kwa nini Kamanda Kamuhanda alitamba kwenye vyombo vya habari kuwa hawezi kujiuzulu kutokana na tukio la kuuawa kwa mwandishi wa habari Daudi Mwangosi. Tumepata tafsiri pia kuwa ingawa 'OPERESHENI UA MWANGOSI' iliratibiwa na kuongozwa na Kamuhanda, lakini katika hali halisi, operesheni hiyo, ilikuwa na baraka zote za mkuu wa nchi!! Na ndiyo maana pamoja na wananchi wengi, baada ya kuziona zile picha za mauaji ya Mwangosi, walihoji sana, kwanini kamanda Kamuhanda na wenzake akina Shilogile, Chagonja na Mwema, wasiwajibike kwa matokeo hayo. Lakini wakuu hao wa polisi, walitulia kimya kabisa, na hadi kufikia hizo tambo za huyo Kamuhanda, ambaye anaeleza wazi kuwa yeye hawezi kujiuzulu ng'o!! Kwa maana hiyo kwa mazingira hayo, sioni hata maana ya pesa za walipa kodi kutumika ovyo kwa kuunda Tume za uchunguzi za akina IGP na Mwema, ambazo matokeo yake yanajulikana wazi kuwa yatawasafisha wauaji!! kwa kuwa ni dhahiri Tume hizo haziwezi kutoa taarifa kinyume na matamshi yaliyotolewa na mkuu wa nchi kuwa mauaji hayo yalibidi, kwa kuwa Jeshi la polisi lilikuwa linatekeleza wajibu wake wa kisheria!! Baada ya kufanya tathmini hiyo, nadhani ni wajibu wetu watanzania kuangalia what is the next step. Kwa maoni yangu kwa kuwa picha za mauaji, hasa katika tukio la Mwangosi zipo, na kwa kuwa ipo wazi kuwa hata huyo corporal Simion, aliyeburuzwa mahakamani ni geresha tu ya watawala, ambapo hatimaye hata yeye naye ataachiwa huru. Sasa naamini ni wajibu wa wanasheria wetu wazalendo,pamoja na wanaharakati na wenye uzalendo wa hali ya juu, kuziangalia sheria zetu, kama kutakuwa na uwezekano wa masuala haya ya mauaji wa makusudi wa raia wasio na hatia, kuweza kuyafikisha kwenye mahakama ya kimataifa ya the Hague. Nasema hivyo kwa kuwa kwa ushahidi usio na shaka yoyote, kwa sasa mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya raia wasio na hatia ni yeye mwenyewe Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. Kwa mujibu wa Katiba yetu ya sasa, hakuna uwezekano wowote wa Rais wetu, kumburuza mahakamani,wakati huu ambapo yupo madarakani, na hata hapo atakapoachia madaraka na kumkabidhi Rais wa awamu ya tano!! Kwa maana hiyo wadau mliobobea kwenye sheria, na wadau wengine wanaharakati, tuchangie mada hii, tuangalie namna gani tunaweza kuwafikisha wauaji wa raia wasio na hatia kwenye vyombo vya sheria, ambapo kwenye sheria za nchi yetu, zinawapa ulinzi wa hali ya juu kabisa, pamoja na Katiba hiyo hiyo kutamka wazi kuwa wananchi wote wapo sawa mbele ya sheria!!!
   
 2. m

  malaka JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huyu Jamaa mwacheni sasa na yeye apumizike. TUmeshajua kila kitu chake sasa tufanyaje?
   
 3. M

  Makyomwango JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tumwache apumzike kwa kuendelea kuua watu wasio na hatia na kodi zao ndizo zinamfadhili!
   
 4. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  walishasema 'liwalo na liwe'
   
 5. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  walishasema 'liwalo na liwe'
   
 6. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Kwa bahati mbaya watanzania hatujaamka kiasi hicho na ndo maana huyu jamaa anatoa kauli za kipuuzi namna hii. Cha kufanya ingekuwa ni kuingia mtaani na kukusanyika kwenye tahariri square na hapo ndo kila kitu kingekaa sawa. Ila kwa sasa acha tu wapete, though their time is coming. Ni sheria gani inayoruhusu kuua kwa namna ile???
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi na nyie bado mnasikiliza hizo hotuba zake? Dont u have better things to do?
   
 8. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  I queted his speech since last election and no more. Kuna jamaa yangu ameniambia siku hiyo alizima TV na hajawasha tena anahisi bado atakuwa anaongea mpaka sasa.
   
 9. MANI

  MANI Platinum Member

  #9
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,412
  Likes Received: 1,871
  Trophy Points: 280
  hata mie nashangaa!
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  hata Pharao alikuwa na kiburi sana kwa waisrael lakini walipukutika kama majani
   
 11. THE GAME

  THE GAME JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2012
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  The ends is coming
   
 12. S

  SUPERXAVERY Member

  #12
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kumbe bado wapiga kelele za chura bado mpo. Mbona ninyi watu wagumu kuelewa hivi? Ni wapi Rais amesema mauaji ya Mwangosi yalikua halali?
  Hotuba ile tumeisikiliza na tunao upeo wa kuelewa pia, hatuhitaji wavaa vigwanda mtuchambulie kwa kupotosha kile kilichosemwa na rais wetu tumpendae.
  Halafu uwe na nidhamu unapomzungumzia Rair wa Jamhuri ya Tanzania, usizani J. K ni sawa na huyo GOLD SEEKER WENU!! Dr Swala.
   
 13. f

  filonos JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  ww umeisha ambiwa futa shelia zainchi yako MLEMA alipgwamabom mbona hamkusema kule ZANZIBAR watu wali uwawa na wengine wakaenda SOMALIA akina DUNI waliwekwa ndani mda mrefu 2 hamku piga kelele sababu RAISI NI MKAPA... nahata sikumoja hamuongei lolote ju ya MKAPA nyie sio wana siasa bali ni............MAMBO MSETO
   
 14. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ... Mnaompinga mtoa mada, hadi siku ndugu yenu apoteze maisha for the same reason ndio mtatikisa mioyo yenu. Yeye amaomba watu wenye upeo wa sheria kutoa mwongozo ili kukomesha hili jambo, hata yale ya msingi pia hamuyaoni?
   
 15. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watanzania wanapiga kura kama vipofu, halafu wanalalama kama vichaa! (Generali Ulimwengu 2011)
   
 16. n

  nyantella JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hii riwaya yako ndeefu kweli ila moyoni unamfahamu unaye jaribu kumsafisha ila si rahisi saana ndiyo maana nafsi yako ina kusuta sababu inamjua mhalifu anaye stahili kwenda huko the Hague, mhamasishaji maarufu! ila soon tuta adopt Kenya style anaye hamasisha vurugu "atiwe" ndani mara moja! hamna haja ya the Hague wala nini!
   
Loading...