Baada ya Ethiopia na Msumbiji kuvurugwa; who is next -- ni sisi Tanzania?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,890
Nawaza sana juu ya yanayoendelea

Tazameni Msumbiji hali ilivyo.

Hata sielewi ISIS wana maslahi gani hadi waende Msumbiji wavuke nchi zote hizo.

Huko Ethiopia mambo sio shwari ndo kwanza walikua wameanza kupaa kiuchumi japo walianza na maendeleo ya vitu kitu ambacho sio sahihi sana unapaswa ubalance vyote viwili.

Na hapo linalotafutwa na lile bwawa tu libomolewe maana ule ndo mradi mkubwa wa umeme Afrika na Waziri Mkuu wao ni kibaraka, tena double agent!

Na sisi lile bwawa la Rufiji (refer history yake) nalo limepigwa vita sana sitaki niwe mnafiki kwa hili ule mradi ni muhimu na wa manufaa na tija kubwa sana kwa taifa yaani sio muungaji mkono wa huu utawala kwa mambo wanayotenda kwa asilimia 95 ila kwa huu mradi walau nawapa 5% ya kuwakubali.

Sasa baada ya Ethiopia who is next kama sio sisi Tanzania. Yes ukitafakari sana utaona ni sisi

Na udhaifu mkubwa ni watawala wetu kungalikua na fair nchi hii zingekuja changamoto tungelikabilana nazo sote lakini sasa nchi imekatika vipande vipande dhulma imetamalaki nchini.

Naihurumia sana Mama Tanzania kwa siku zijazo uroho wa watu wachache utatufanya tuwe na disunity katika kupambana na mambo ya siku za usoni.

Ningeandika mengi naomba niishie hapa.

Tafakari kwa makini hili bandiko langu
 
Hao wa magharibi mnaowaabudu ndo wafadhili wa hivi vikundi, na hao walio kimbia kwao ndo wachochezi na watengeneza mikakati ili damu zimwagike , kwaajiri ya maslai yao kisiasa.

Kwa hiyo hamna sababu ya kuogopa, sisi Watanzania tuungane coz wasaliti ni sisi sisi, na wale sio wajinga hivyo hawana "mission with nothing", kila kitu kinatokea kwa sababu so na sababu zenyewe ni hawahawa watanzania wasaliti ndugu zetu, waliotanguliza tumbo mbele.
 
Hata kama nipo upinzani au sipo upinzani. Nilisha declare muda mrefu. Anaye fanya juhudi zozote za kurudisha swala la nishati nyuma ktk nchi hii basi huyo ni adui yangu.

Hata leo hii magufuli akisema anarutubisha uranium nitaunga mkono bila kujiuliza mara mbilimbili.
 
Nanye Go,

wakati unaongea uo ushenzi wako, kumbuka kuna wazee vikongwe , watoto wadogo, na wengine tegemezi ambao hawan maslai yoyote ya kisiasa ila ndo mara nyingi damu zao humwagika bila sababu. Bora kama una maslai uwe msatari wa mbele ww na familia yako, na damu yako, ili miaka ijayo uonekane shujaa au siyo
 
Sioni sababu ya kujiita tuna amani ilihali serikali imekuwa adui number moja wa raia wake...leo hii nchi ndani ya muungano inavamiwa kijeshi na watu kuuwawa hovyo harafu tunajisema kuwa Tz mambo shwari. Dadeq
 
Nanye Go

Wewe unadhani isis wakija Tanzania watakuacha sababu wewe ni Chadema?

Familia yako ndugu zako wote watapigwa risasi hadharani unadhani utachukua hatua gani.

Mkuu vita isikie kwa jirani wewe now umeshika smartphone unatype bila wasiwasi huko nje raia wazee watoto na kina mama wanakimbia 24hours na kuchinjwa na kupigwa risasi hakuna chakula hakuna huruma hakuna kulala.

Mpaka hapo unadhani upo sahihi?
 
Sioni sababu ya kujiita tuna amani ilihali serikali imekuwa adui number moja wa raia wake. Leo hii nchi ndani ya muungano inavamiwa kijeshi na watu kuuwawa hovyo harafu tunajisema kuwa Tz mambo shwari. Dadeq
Halafu waje waanzie kwako, hapo hivi. Mkikosa kura hampendwi, eti mnataka watu wafe, mkipata kura mnakula na watoto wenu. Tulia dawa iwaingie
 
naamini damu yako itakuwa mstari wa mbele, na familia yako ili kuikomboa nchi, ni ushenzi kutaka damu ya mwingine imwagike kwa sababu ya utopolo ulioandika
Huyo jamaa sijui anatumia nini kufikiri.
 
Sioni sababu ya kujiita tuna amani ilihali serikali imekuwa adui number moja wa raia wake. Leo hii nchi ndani ya muungano inavamiwa kijeshi na watu kuuwawa hovyo harafu tunajisema kuwa Tz mambo shwari. Dadeq
Mkuu wewe umeshika smartphone unatype hakuna amani bila hata wasiwasi.

Huko nje kina mama watoto na wazee wasio na hatia wanakimbia 24h hakuna kula hakuna kulala na no home no hope.
Wanachinjwa na kupigwa risasi hadharani bila ya hatia.

Wakija wewe familia yako ndugu zako wote mtaenda hakuna atakayeachwa.

Then unasema Tanzania hakuko shwari wakati hapo ume relax na smartphone na una uhakika wa kunywa maji.

Think again.
 
Kuna haja gani ya kujiwazia mema ilihali kuna watu wametiwa vilema na kuharibiwa makazi yao, usipoguswa na matatizo ya jirani zako jua kabisa una roho ya kinyama na utu haumo ndani yako, yaliyotokea zanj yananiuma kama mwanadamu mwenye hisia.
 
kuna haja gani ya kujiwazia mema ilihali kuna watu wametiwa vilema na kuharibiwa makazi yao, usipoguswa na matatizo ya jirani zako jua kabisa una roho ya kinyama na utu haumo ndani yako, yaliyotokea zanj yananiuma kama mwanadamu mwenye hisia..
Kwahiyo hao IS wakija ndo yatatulia, eeeh. Na je kama hiyo trela ulimuona yule aliyechinjwa juzi, assume ni kaka, mdogo wako au baba yako. na hata hao wa zenzi wamepumpiwa na watu ambao wantaka wengine wafe ili watoto wao wakasome ughaibuni, yani ww ufe yeye apate maisha mazuri, acha kuwza utopolo amka kafanye kazi huko
 
Kuna haja gani ya kujiwazia mema ilihali kuna watu wametiwa vilema na kuharibiwa makazi yao, usipoguswa na matatizo ya jirani zako jua kabisa una roho ya kinyama na utu haumo ndani yako, yaliyotokea zanj yananiuma kama mwanadamu mwenye hisia.
Ni kweli hisia.

Lakini haitakiwi kumake decision kwa kutumia hisia bali ondoa hisia then tumia ufahamu kumake decision.

Solution sio kuendeleza chaos bali ni kuzuia hizo chaos ili zisije kuleta madhara kwenye generations zijazo na kuepukana nazo kabisa zisitokee tena.
 
Sioni sababu ya kujiita tuna amani ilihali serikali imekuwa adui number moja wa raia wake. Leo hii nchi ndani ya muungano inavamiwa kijeshi na watu kuuwawa hovyo harafu tunajisema kuwa Tz mambo shwari. Dadeq
Nonsense.
 
Bulaya001
Sasa kama akili zako ni hizi, basi naweza sema upinzani bado hamna kiongoz hata mmoja wa kumpa nchi labla klizazi kijacho kabisa, mm nilikuwa upinzani but siwez kukana kufikiria sawa na watu kama ww, ndo mana mmeshindwa
 
Huwezi kukombolewa na shetani, shetani kaiba kura na shetani ataleta ugaidi
 
Back
Top Bottom