Baada ya cdm, ccm nao kumwona rais mara moja!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,725
Baada ya CHADEMA KUUNDA KAMATI NDOGO itakayokutana na Rais Kikwete kuhusiana na Katiba, CCM nao wamesema wataongelea hatua hiyo katika vikao vyao vya kamati kuu, na hatimaye watapanga nao kwa upande wao kumwona Rais na Mwenyekiti wa ccm kwa suala hilohilo!
Maajabu haya ya kisiasa!
 
Haahaahaaaa! Vichwa vya panzi... Wazee wa kuiga na kukariri hakuna chema wanachoweza kubuni wenyewe, kazi yao kusikilizia tu wadandie.. Kuvimbiwa kubaya jamani.
 
ccm wana wakilisha kina nani?au wakazi wa dar,dom na zenj?
CCM watakuwa wanawakilisha wazee wa Dar na magamba wao bila shaka,kwenda kudeku na kujua mkulo kaambiwaje na wa CDM.
Huu ni umbea tuu kwa kweli.Wanaenda kuibia mtihani waje kusema ni wao ndio wamesema kama kawaida yao.
 
CCM wanajua sumu ya Chadema sio mchezo; ya King Cobra ina nafuu. Jiulize wakati wa uchaguzi mkuu na mdogo wa Igunga jinsi Chadema walivyowasumbua CCM kurudia kampeni zao kila walikopita - kwa mfano Mwanza.

CCM wanadhani watawashawishi wananchi na wanachama wao kwa kuiga kila kinachofanywa na Chadema! Wananchi watashawishika kwa hoja zenye mashiko na yakinifu; zenye kutanguliza maslahi ya taifa mbele na sio maslahi ya chama chao au usisi (uCCM) kama ambavyo imejidhihirisha Bungeni hivi karibuni.

Laiti CCM wangalitambua hili tangu zamani leo hii wasingalikuwa wanajisumbua bure au kukimbizwa mchaka mchaka na Chadema kwa ufadhili wa raia wenye mapenzi mema na nchi yetu.
 
Haahaahaaaa! Vichwa vya panzi... Wazee wa kuiga na kukariri hakuna chema wanachoweza kubuni wenyewe, kazi yao kusikilizia tu wadandie.. Kuvimbiwa kubaya jamani.
Halafu anayetangaza hayo bila aibu ni NAPE,
WANA MASHAKA SANA HAWA kuwa CDM wataua ndege wawili kwa jiwe moja!
 
Hiki chama cha ma......zzzzzzzzzzzzzzz kinachekesha kweli si wayaongelee huko waliko kwenye kikao chao kwani mpaka nao waende ikulu? Wanaogopa Chadema watamwaga ugali na mboga pamoja!! ccm mtavuna mlichopanda msitufanye sisi wajinga.
 
Baada ya CHADEMA KUUNDA KAMATI NDOGO itakayokutana na Rais Kikwete kuhusiana na Katiba, CCM nao wamesema wataongelea hatua hiyo katika vikao vyao vya kamati kuu, na hatimaye watapanga nao kwa upande wao kumwona Rais na Mwenyekiti wa ccm kwa suala hilohilo!
Maajabu haya ya kisiasa!
Heeeee! unanichekesha mkuu yaani unataka kunambia swala hili hawakulizungumzia kabla ndani ya vikao vya chama na kuwa na msimamo au hawamwamini JK?
 
wkigundua chadema wamemwaga vitu vya msingi kwa JK hao Magamba wataenda kumtisha au watamwabia kitu gani kinachoweza kufanana na hoja na fikra pevu za chadema?au wakitoka huko waje waseme wao wamemshauri JK kurejea nyuma katika mswada huo?anyway tutayaona hayo muda ukifika
 
Wacha nao waende wakatoe kero zao. Cha ajabu ni nini?
Kero zimeanza baada ya Cdm kupanga mkakati huo?...kabla hazikuwepo?
Cha ajabu ni wanamagamba kukosa kabisa strategists wake, hadi kutegemea cdm kuanzisha kila jambo ndipo waige!
Mambo yote wanayoanzisha wenyewe hawafanikiwi...mfano kuvua gaMBA!...AHADI ZA UCHAGUZI...
 
Back
Top Bottom