dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,500
- 3,481
Ile kauli ya mtu kukata tawi alilokalia, imeanza kuwatokea Wabunge na Mawaziri wa CCM. Hali ya bunge kufanyikia backstage, imewafanya Mawaziri Waanze kuhaha kutafuta Video, Audio zao hasa zile walizoongea wakiwa ndani ya Bunge ili wazishee kwenye Mitandao ya Kijamii. Wapiga picha wa Bunge wamekuwa Wakisumbuliwa na Mawaziri ili wawape vipande vya sehemu walizoongea wao tu. Hii ni baada ya Mawaziri hao kukosa Mvuto kwa jamii, hivyo wanadhani Kuonekana kwao kwenye mitandao kutawarudishia hua kwenye jamii.
Ndo maana Sasa Mkitembelea kurasa za Mawaziri na manaibu waziri katika mitandao ya kijamii, mtakuta video, audio, maandishi ya kile walichokifanya bungeni tofauti na ilivyokuwa hapo mwanzo. Hii inadhihilisha waliunga mkono Bunge kufungiwa kuoneshwa bila kujua wafanyalo.
Hali hii imeongeza mwanya wa Rushwa Kwa Watendaji wa bunge kwa kile wanachosema nipe ile video yangu ntakupoza. Naomba TAKUKURU sasa mkunjue makucha. Kama mwataka muonekane na msikike, ruhusu live