Sijijui
JF-Expert Member
- Jan 14, 2018
- 7,879
- 8,800
Na hapo amepiga marufuku shughuli za vyama vya siasa eti afanye kazi? Je Kama vyama vingeendelea na mikutano yake si ndo angeongeza negative kabisa? UtopoloKumbe mkapa alichukua nchi ikiwa katika GNI per capita $170. Muhula wake wa kwanza aliifikisha nchi katika GNI per capita $410. Wakati anaondoka iliacha GNI per capita $500.
Alipoingia kikwete, muhula wa kwanza alifikisha GNI per capita $720. Nawakati anaondoka aliacha GNI per capita $980.
Tena hii $1,080 aliieleza kikwete juzi, lakini kabla ya hapo tulikuwa tunaimbishwa wimbo wa kwamba tumeingia uchumi wa kati mapema kuliko muda ulio tarajiwa yaani 2025, bila kuambiwa tupo GNI ngapi adi sasa. Na kumbe matarajio ya hiyo 2025 ni GNI per capita $ 3,000. Ukiangalia hesabu zilivyo JK alibakisha GNI $ 56 tu kuingia uchumi wa kati lakini ndie rais anae onekana muovu na ameharibu uchumi wa nchi.
Muhula wa kwanza wa mkapa ni GNI per capita $240.
Muhula wa kwanza wa kikwete ni GNI per capita $220.
Muhula wa kwanza wa magufuli ni GNI per capita $100. Tena ukirudisha ile $20 ambayo magufuli aliipoteza katika $980 iliyoachwa na kikwete utapata jibu kwamba muhula wa kwanza wa magufuli amepata $80.