thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Ukifuatilia maelezo ya wachambuzi mbalimbali mitandaoni kuhusu kauli ya Mheshimiwa Kikwete msibani kwa marehemu Mkapa utagundua kuna mabishano ambayo hayana umuhimu wowote,sana yametanguliza chuki binafsi kwa hawa viongozi.
Kauli ya Jakaya kikwete ilijikita katika kumuelezea Mkapa kama muasisi wa mifumo tulionayo kwa sasa na ndoto yake katika kuipaisha Tanzania kiuchumi .
Kikwete kakiri Marehemu Mkapa aliipokea nchi toka kwa Mwinyi ikiwa na hali mbaya sana kiuchumi,hili halina ubishi,ndio maana akatengeneza mifumo ambayo mpaka anaachia madaraka nchi ilikuwa vizuri kiuchumi na serikali ilikuwa na fedha ya kutosha.alidhibiti mfumuko wa bei kwa kiwango cha hali ya juu sana.
Baada ya Kikwete kupokea kijiti alianza vizuri sana ,lakini ukiangalia muda ulivyozidi wasaidizi wa Kikwete walimuangusha sana,pamoja na nia yake njema , kwani baadhi yao hawakuwa waadilifu hata kidogo ,walikuwa ni mchwa,ushikaji pia ulimuharibia sana kazi,kipindi chake tumeona watumishi wa umma walikua na ukwasi usioelezeka , ndio maana wakati anamkabidhi Rais Magufuli kijiti ,serikali ilikuwa haina fedha ,serikali ilikuwa na dollar za kimarekani 1.8 billion tu,hii ilikuwa ni pesa ndogo sana kuendesha nchi kwa mtawala mpya, ilihitaji kazi ya ziada kupata fedha za kuendesha serikali,
Hata hivyo Rais Magufuli alisimama imara sana bila kuyumbishwa na wale waliozoea kuweka serikali mfukoni.
Kwanini nasema Magufuli alitakiwa ampokee kijiti Mkapa,kutupeleka kwenye hicho kipato cha dollar 3000? ,ni kwasababu Mkapa hakucheka na nyani ,alikua serious sana ,alikuwa mkali ,hakuyumbishwa na maneno maneno aliamini kile anachokisimamia,ukimuangalia Magufuli ni typical Mkapa ndio maana kupitia mifumo ilioachwa na Mkapa kafanya makubwa ndani ya muda mfupi sana (,Mega projects),nakadhalika , ili mifumo alioacha Mkapa ilete ufanisi ilihitaji kiongozi mkali asiecheka na watumishi wabovu wasio simamia mifumo ,hivyo "I repeat again Magufuli was a right person after Mkapa ".
Kwahiyo ndoto ya Mkapa ingetimia 2025 kama alivyofikiri, kua na kipato cha dollar 3000,kwani gap lisingekuwa kubwa kama tulionavyo sasa ikiwa awamu ya nne isingezembea kusimamia mifumo ilioachwa na Mkapa .
Nimalize kwa kusema mifumo ilioachwa na Mzee Mkapa ni madhubuti ispokua ilikosa na inakosa viongozi waadilifu wa kuitumikia .
Mwisho tuwaenzi viongozi wetu wote wakuu waliohai na waliotangulia mbele ya haki , kwani kila mmoja ana nafasi yake katika mafanikio ya taifa letu,tusiwabeze hata kidogo kwa chuki zetu binafsi , kufanikiwa kwa Tanzania si kazi ya mtu mmoja ,ni muunganiko wa juhudi zetu sote