Baada ya awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa kumaliza muda wake, mtu sahihi wa kumrithi alitakiwa awe Magufuli. Nchi ingepaa sana

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
105,140
2,000
Kwani yeye ni kutoka chama gani hapa nchini?
Ni kweli kabisa, ila kitendo cha Magufuli kupokea nchi kilofa haina hela mpaka kuahirisha sherehe za uhuru kimagirini kusingizia usafi kumbe hakuna hela kilimtia uchungu. Ndo maana asubuhi asubuhi aliamkia wizara ya fedha kimachungumachungu na kwa kweli ana uchungu na wezi mchwa walioitafuna nchi hii na wote wenye nia hiyo.
 
sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
5,199
2,000
Mkuu unafikiri ni akili za kijamaa? Incompetency yake ndo inamfanya aamini kuwa akitembelea kivuli Cha Nyerere labda ataonekana yeye ni bora,yaani hata wakati aliopo haujui
Ila hicho kivuli cha nyerere ndio kimejenga na kumalia hospitali ya rufaa mkoani mara iliyosimama tika mwaka 1986.

Kivuli cha nyerere ndio kimehamishia makao makuu dodoma plan ya mwaka 1974.

Kivuli cha nyerere ndio kinajenga mradi wa stieglers gorge ambao plani yake ni ya mwaka 1969.

Kivuli cha nyerere ndio kimeifanya dar es salaam iwe kwenye top ten ya majiji yanayokuwa kwa kasi africa kutokana na miradi ya kimkakati na miundo mbinu ya kisasa zikiwemo
Streets lights and street roads.
Barabara za kisasa kama mwenge morocco, ubungo chalinze.
Tanzanite bridge & Ubungo interchange. Airport ya kisasa iliyomaliziwa kwa ustadi mkubwa chini ya jpm.
Upanuzi wa bandari ya dar es salaam. Upatikanaji wa maji kwa zaidi ya 80%. Ujenzi wa mradi wa mwendokasi mbagala - gerezani.
Masoko ya kisasa kama magomeni, kisutu, tandale na maeneo mengine.
Stendi ya kisasa ya mkoani ambayo ujenzi wake unaendelea.
Machinjio ya kisasa ya vingunguti.
Kituo cha kisasa cha SGR ambacho muundo wa jengo lake unafanana na madini ya tanzanite.
 
mzee wa liver

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
77,126
2,000
Nini kinamfanya hivi sasa ashindwe kuifanya nchi ikapaa?!

Kakuta GNI per capita ikiwa USD 980 lakini hadi sasa ndo kwanza amefikisha USD 1080; an increase of ONLY USD 100 kwa muda wote aliokaa madarakani!!

View attachment 1522988

Mkapa aliachaForeign Reserve ikiwa roughly USD 2 Billion, na JK akaacha ikiwa USD 4.4 Billion, lakini hadi sasa ndo kwanza inacheza around USD 5 Billion!!

View attachment 1522990

View attachment 1522992

Nchi ina uhaba mkubwa wa Walimu wa Sayansi; na awamu iliyopita ilifanya jitihada mbalimbali ili kutatua tatizo hilo, na iliposhindikana kabisa, waka-introduce Special Diploma (Science & Mathematics) ili kukabiliana na upungufu huo!!!

JPM alipoingia tu, akafuta ile programme kwa madai wanaosoma ni vilaza, lakini miaka 5 anamaliza sasa lakini bado hajaleta alternative!!

Kwa kuona umuhimu wa Sayansi katika ulimwengu wa leo, awamu iliyopita ikahamasisha ujenzi wa maabara! JPM baada ya kuingia alitarajiwa aanzie wengine walipoishia ili kuhakikisha shule zetu zina maabara lakini kinyume chake, maabara kazipiga chini na bado hana alternative!!

Sasa nchi angeipaza vipi wakati hadi leo hajaona umuhimu wa sayansi?! Wakati hadi sasa hajaona umuhimu wa kuwa na walimu wa kutosha kwa masomo ya sayansi?! Wakati hadi sasa hajaona umuhimu wa kuwa na maabara?!
Mkuu big up Sana kwa data hoja ujibiwa kwa hoja
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,893
2,000
Yaani nyie watu pasua kichwa kweli kweli!!! Yaani ningesema hazina kulikuwa na nini wakati nimeonesha hapo taarifa ya BoT inayoonesha Hazina kulikuwa na nini?!
View attachment 1524474
Tatizo lenu ni moja! JPM keshasema hadharani wakati mwingine anafanya maamuzi kutegemea na ameamkaje! Kwahiyo akiamika na kusema alikuta hazina hakuna kitu ( though I know Magu hajawahi kusema ujinga kama huu), nanyi mnafanya ndiyo agenda yenu bila hata ya ku-verify!!
Mkuu baada ya hii comment,Kama atarudi na huo utopolo wake wa hoja naomba ianzishwe harambee apelekwe hospitali probably atakuwa na corono
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,893
2,000
Ila hicho kivuli cha nyerere ndio kimejenga na kumalia hospitali ya rufaa mkoani mara iliyosimama tika mwaka 1986.

Kivuli cha nyerere ndio kimehamishia makao makuu dodoma plan ya mwaka 1974.

Kivuli cha nyerere ndio kinajenga mradi wa stieglers gorge ambao plani yake ni ya mwaka 1969.

Kivuli cha nyerere ndio kimeifanya dar es salaam iwe kwenye top ten ya majiji yanayokuwa kwa kasi africa kutokana na miradi ya kimkakati na miundo mbinu ya kisasa zikiwemo
Streets lights and street roads.
Barabara za kisasa kama mwenge morocco, ubungo chalinze.
Tanzanite bridge & Ubungo interchange. Airport ya kisasa iliyomaliziwa kwa ustadi mkubwa chini ya jpm.
Upanuzi wa bandari ya dar es salaam. Upatikanaji wa maji kwa zaidi ya 80%. Ujenzi wa mradi wa mwendokasi mbagala - gerezani.
Masoko ya kisasa kama magomeni, kisutu, tandale na maeneo mengine.
Stendi ya kisasa ya mkoani ambayo ujenzi wake unaendelea.
Machinjio ya kisasa ya vingunguti.
Kituo cha kisasa cha SGR ambacho muundo wa jengo lake unafanana na madini ya tanzanite.
Mkuu unadhani kujenga soko moja unahitaji kuwa na bei gani? Please zungumzieni issues,umesikia kuwa mkapa alihangaika na hizi petty issues? Sasa nisaidie huo ujenzi wa masoko unasaidieje Tanzania kucompete kwenye regional and global markets?
 
sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
5,199
2,000
Mkuu unadhani kujenga soko moja unahitaji kuwa na bei gani? Please zungumzieni issues,umesikia kuwa mkapa alihsngaika na hizi petty issues? Sasa nisaidie huo ujenzi wa masoko unasaidieje Tanzania kicompete kwenye regional and global markets?
Kwanza kama umeelewa mainly nimezungumzia ukuaji wa miji ikiwemo jiji la dar es salaam. Huwezi ukaona umuhimu ya barabara kama huna. Hizo advantages zinakuja kupitia ukuaji wa mji.

Huwezi ita petty issues wakati hukuwa nazo na dunia iliyoendelea inazo. Huwezi vutia uwekezaji kama huna hizo unazoita petty issues kama umeme wa uhakika, maji ya uhakika, miundo mbinu ya uhakika.

Ukianza kuzungumzia suala bei utachekesha mzee maana unamaanisha havitakuwa na maana ya kuvifanya sababu ni cheap au?? Je zahanati ya million 400 isijengwe sababu ni cheap?? Unajua umuhimu wa uwepo wa hiyo miradi?
 
babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,339
2,000
Mkapa aligubikwa na rushwa kubwa nyingi. Awamu hii hatujui nn kinaendelea taarifa zote muhimu zimetundikwa
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,893
2,000
Kwanza kama umeelewa mainly nimezungumzia ukuaji wa miji ikiwemo jiji la dar es salaam. Huwezi ukaona umuhimu ya barabara kama huna. Hizo advantages zinakuja kupitia ukuaji wa mji.

Huwezi ita petty issues wakati hukuwa nazo na dunia iliyoendelea inazo. Huwezi vutia uwekezaji kama huna hizo unazoita petty issues kama umeme wa uhakika, maji ya uhakika, miundo mbinu ya uhakika.

Ukianza kuzungumzia suala bei utachekesha mzee maana unamaanisha havitakuwa na maana ya kuvifanya sababu ni cheap au?? Je zahanati ya million 400 isijengwe sababu ni cheap?? Unajua umuhimu wa uwepo wa hiyo miradi?
Magu hajawahi Jenga barabara Wala kufanya lolote la maana,five years ametembelea nyota ya watangulizi wake huku akitumia propoganda uchwara kuerode akili watu wa aina yako
 
lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,988
2,000
Inawezekana huu ukawa miongoni mwa chambuzi za hovyo 2020! Uchumi hauwezi paa kwa kununua ndege kiholela!
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,956
2,000
Kawaulize wapinzani watakwambia, kumbuka wakati wa kambpeni walisema serikari imemaliza pesa zote imeenda kununua magari ya washa washa,
Pia kuna machangiaji kasema magufuli amekuta kuna 1.8 bilioni dollar kwa hiyo ni pesa ndogo sana kwa ahadi alizozitoa kwa nchi na mahitaji yake.
Huyo aliyesema kuwa Magufuli aliingia na kukuta reserve ya Taifa $1.8 billion, sijui hizo taarifa anaokototeza wapi!

Mkapa wakati anaondoka aliacha zaidi ya $3 billion. Kikwete aliacha zaidi ya $4.4 billion.

Kati ya Mkapa, Kikwete na Magufuli, katika uchumi Magufuli has performed the worst. Na kwa namna Magufuli alivyoharibu misingi ya ujenzi wa uchumi, hata akipita miaka 5 ijayo yena, hataweza kurekebisha makosa aliyoyayafanya. Katika historia, atabakia kiulinganifu ndiye aliyefanya vibaya katika ujenzi wa uchumi.

Rais aliyefanya radical economic positive changes ni Hayati Benjamin Mkapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,244
2,000
Ukifuatilia maelezo ya wachambuzi mbalimbali mitandaoni kuhusu kauli ya Mheshimiwa Kikwete msibani kwa marehemu Mkapa utagundua kuna mabishano ambayo hayana umuhimu wowote,sana yametanguliza chuki binafsi kwa hawa viongozi.

Kauli ya Jakaya kikwete ilijikita katika kumuelezea Mkapa kama muasisi wa mifumo tulionayo kwa sasa na ndoto yake katika kuipaisha Tanzania kiuchumi .

Kikwete kakiri Marehemu Mkapa aliipokea nchi toka kwa Mwinyi ikiwa na hali mbaya sana kiuchumi,hili halina ubishi,ndio maana akatengeneza mifumo ambayo mpaka anaachia madaraka nchi ilikuwa vizuri kiuchumi na serikali ilikuwa na fedha ya kutosha.alidhibiti mfumuko wa bei kwa kiwango cha hali ya juu sana.

Baada ya Kikwete kupokea kijiti alianza vizuri sana ,lakini ukiangalia muda ulivyozidi wasaidizi wa Kikwete walimuangusha sana,pamoja na nia yake njema , kwani baadhi yao hawakuwa waadilifu hata kidogo ,walikuwa ni mchwa,ushikaji pia ulimuharibia sana kazi,kipindi chake tumeona watumishi wa umma walikua na ukwasi usioelezeka , ndio maana wakati anamkabidhi Rais Magufuli kijiti ,serikali ilikuwa haina fedha ,serikali ilikuwa na dollar za kimarekani 1.8 billion tu,hii ilikuwa ni pesa ndogo sana kuendesha nchi kwa mtawala mpya, ilihitaji kazi ya ziada kupata fedha za kuendesha serikali,
Hata hivyo Rais Magufuli alisimama imara sana bila kuyumbishwa na wale waliozoea kuweka serikali mfukoni.

Kwanini nasema Magufuli alitakiwa ampokee kijiti Mkapa! ,kutupeleka kwenye hicho kipato cha dollar 3000 ,ni kwasababu Mkapa hakucheka na nyani ,alikua serious sana ,alikuwa mkali ,hakuyumbishwa na maneno maneno aliamini kile anachokisimamia,ukimuangalia Magufuli ni typical Mkapa ndio maana kupitia mifumo ilioachwa na Mkapa kafanya makubwa ndani ya muda mfupi sana (,Mega projects),nakadhalika , ili mifumo alioacha Mkapa ilete ufanisi ilihitaji kiongozi mkali asiecheka na watumishi wabovu wasio simamia mifumo ,hivyo "I repeat again Magufuli was a right person after Mkapa ".

Kwahiyo ndoto ya Mkapa ingetimia 2025 kama alivyofikiri, kua na kipato cha dollar 3000,kwani gap lisingekuwa kubwa kama tulionavyo sasa ikiwa awamu ya nne isingezembea kusimamia mifumo ilioachwa na Mkapa .

Nimalize kwa kusema mifumo ilioachwa na Mzee Mkapa ni madhubuti ispokua ilikosa na inakosa viongozi waadilifu wa kuitumikia .

Mwisho tuwaenzi viongozi wetu wote wakuu waliohai na waliotangulia mbele ya haki , kwani kila mmoja ana nafasi yake katika mafanikio ya taifa letu,tusiwabeze hata kidogo kwa chuki zetu binafsi , kufanikiwa kwa Tanzania si kazi ya mtu mmoja ,ni muunganiko wa juhudi zetu sote
Utakuwa na minyoo mkuu
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
9,962
2,000
Ila hicho kivuli cha nyerere ndio kimejenga na kumalia hospitali ya rufaa mkoani mara iliyosimama tika mwaka 1986.

Kivuli cha nyerere ndio kimehamishia makao makuu dodoma plan ya mwaka 1974.

Kivuli cha nyerere ndio kinajenga mradi wa stieglers gorge ambao plani yake ni ya mwaka 1969.

Kivuli cha nyerere ndio kimeifanya dar es salaam iwe kwenye top ten ya majiji yanayokuwa kwa kasi africa kutokana na miradi ya kimkakati na miundo mbinu ya kisasa zikiwemo
Streets lights and street roads.
Barabara za kisasa kama mwenge morocco, ubungo chalinze.
Tanzanite bridge & Ubungo interchange. Airport ya kisasa iliyomaliziwa kwa ustadi mkubwa chini ya jpm.
Upanuzi wa bandari ya dar es salaam. Upatikanaji wa maji kwa zaidi ya 80%. Ujenzi wa mradi wa mwendokasi mbagala - gerezani.
Masoko ya kisasa kama magomeni, kisutu, tandale na maeneo mengine.
Stendi ya kisasa ya mkoani ambayo ujenzi wake unaendelea.
Machinjio ya kisasa ya vingunguti.
Kituo cha kisasa cha SGR ambacho muundo wa jengo lake unafanana na madini ya tanzanite.

Machinjio na Stendi ni achievements ndogo sana kwa mtu wa hadhi ya raisi
Ukihesabu stendi zilizojengwa enzi za JK ni nyingi, utakesha, lakini hatuwezi kumsifu kwa vitu kama hivyo.

Huwezi kumsifu rais kwa barabara ya kilometa mbili, ya morocco - Mwenge, tena ambayo mradi ulitafutwa na Serikali ya Kikwete.

sisi tunasifu miradi mikubwa kama
1. Daraja la Mkapa alilojenga BWM
2. Daraja la Kwenye mto Malagarasi alilojenga JK
3. Mradi kama Mwendokasi zilizowekwa na JK
4. Uwanja kama wa Taifa uuliojengwa na Mkapa

Tukianza kusifu vitu vidogovidogo tutakuletea hapa miradi iliyoziduliwa na Mbeba mikasi wa JK Dr Gharib Bilal na tutakesha humu kuiorodhesha. Miradi ua hivyo JK alikuwa haangaiki kuizindua kwa sababu haikuwa hadhi yako

Wewe sifu SGR na Stieglers hayo ni mambo makubwa lakini mambo ya machinjio na Stendi ni vitu vidogo sana kwa hadhi ya rais
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom