Azimio la Arusha: Kwanini shule za Seminari hazikutaifishwa?

Moja ya Nguzo za Azimio la Arusha la mwaka 1967 ni kutaifisha vyanzo vyote vya Uchumi ikiwamo Mabenki, Mashirika ya Bima, Vyuo & Shule binafsi.

Swali ni kwamba kwanini Shule za Seminari hazikutaifishwa?
Nyingi zilichukuliwa na serikali mfano Forodhani, Ilboru, Kigurunyemebe chuo cha ualimu, Pugu secondari n.k.
 
Nadhani mleta Mada umeshapata baadhi ya majina ya shule zilizotaifishwa wakati wa azimio la Arusha shule Kama Nganza,Tosamaganga,pugu,Nsumba,Milambo na nyingine nyingi tu zilikuwa za kanisa katoriki.
Yeye kaulizia kuhusu Seminari,siyo Kila shule ya Kanisa ni seminari.Zingine hutoa elimu kwa watu wote hazina lengo la kuandaa watawa.
 
Una uhakika Tabora boys ilikuwa ya Kanisa?
 
Hivi kumbe Tabora boys nayo ilikuwa ni ya kanisa,sikufahamu hili nilikua najua ni Milambo high school tu pale Tabora manispaa ndiyo iliyotaifishwa kwa wakati ule.
Tabora boys ilikuwa shule ya serikali kwa ajili ya watoto wa Mchifu ikiitwa Tabora school.
 
Tunasubiri msaada kutoka Oman# kila mwenye dini yake anakuambia mi nina ndugu zangu Oman mwisho wanabaki kuletewa tende,mikeka na simu.
 
Moja ya Nguzo za Azimio la Arusha la mwaka 1967 ni kutaifisha vyanzo vyote vya Uchumi ikiwamo Mabenki, Mashirika ya Bima, Vyuo & Shule binafsi.

Swali ni kwamba kwanini Shule za Seminari hazikutaifishwa?
Azimio la Arusha lilikuwa kwa ajili ya kuzuia kujilimbikizia mali kama mtu binafsi, sio taasisi, na makanisa ni taasisi

Hivi mnafundishwa nini huko shule siku hizi? Namna mbalimbali za kupiga chabo?
 
Nyingi tu ziligeuzwa kuwa za serikali,pugu,tosamaganga, songea TTC, mpwapwa TTC,na nyingine nyingi huko tanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…