Azikwa na kreti za bia na soda Kahama

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,800
34,189
makaburi.jpg

Kahama. Wakati serikali ikipigia kelele kukemea imani za kishirikina, wilayani Kahama bado ni kitendawili baada ya mkazi mmoja wa Kijiji cha Mwamande, Kata ya Mwanase katika Halmashauri ya Msalala kufariki na baadaye wanakijiji kumzika na mali zake zote yakiwemo makreti ya bia na soda aliyokuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya baa.

Tukio hilo limetokea jana katika kijiji hicho baada ya mwanakijiji huyo, Mahushi Lutaja kufariki na baadaye familia yake kupitisha maadhimio ya kumzika na mali zake zote kwa imani ya kwamba kifo chake kimetokana na kurogwa na wao kuhofia kwamba wakibaki na mali zake nao watakumbwa na mauti.

Kwa mujibu wa diwani wa Kata ya Mwanase, Samson Masanja, Lutaja baada ya kifo chake alizikwa na baisikeli moja vitanda vinne na magodolo yake pamoja na masanduku ya nguo zake zote na vitu vingine vidogovidogo alivyokuwa akivitumia

Pia Masanja alisema, Lutaja alizikwa na makreti ya bia na soda ambayo kabla ya kifo chake alikuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya kuuza vinywaji kwenye kijiji hicho cha Mwamande ambapo tukio hilo limehusishwa na imani za kishirikina

Wakati akiugua ndugu zake waliamini kwamba ugonjwa huo uliopelekea kifo chake ulitokana na kurogwa hivyo familia yake iliingiwa na hofu hiyo hasa kutokana na kuwepo madai ya waganga wa jadi kuamini kwamba ndugu yao alirogwa

Azikwa na kreti za bia na soda Kahama
 
Hii ni kali ya kufungulia mwaka, cha kushukuru ni mjane kama yupo kasalimika maanake wangeazimia naye azikwe ingekuwa majanga
 
Na hao ndugu wazikwe nao, ni watu wa marehemu kama walivyozika vitu.
 
Vipi kuhusu hela zake mbona hawajazungumza kuhusu cash money au hizo hazina mkosi
Hahaa nani akuzike na pesa, yani hilo kaburi lingekua hapa Dar wajanja wangeshalifukua na kuondoka na kila kitu mpaka nguo alizovaa
 
nadhani kaburi lilikuwa kama fish pond

baiskeli
kreti za bia
vitanda 4
magodoro hahahaha nimecheka sana
 
Huko Usukumani bado sana ... uchawi, ujinga, ubabe, mauaji ya wazee & albino ... labda ndiyo maana yule jamaa alikuwa anasisitiza elimu, elimu, elimu.
 
Naomba kuuliza, je wamezika na pesa za marehemu? Au pesa hazihusiki?
 
Back
Top Bottom