Azania Sec. School (SPECIAL THREAD)

Yaan pale full package.

Kuna vipanga.

Kuna watu wenye vipaji

Alaf kuna sisi sasa, hatupo kotekote, kazi yetu kuchonga modo tuu na kuvaa milegezo.
 
Kuna arusha school ya 1932
 
Big Nation kwa Dar ni Tambaza Azania hawatuwezi kiUgomvi ,kwa Unyamwezi ,KwaExposure nk

Tazama Mbali Zaidi (Tambaza) ndio moto wa kuotea mbali.
 
Dah nimekumbuka mbali enzi za Ngoozye,Mwalimu wa michezo marehemu Hatia,Mzee Matawa,Mganga,Nkya,Luchwaza,Mlokozi nk

Niliwahi dakwa nikiwa natoroka mida ya saa 9 na Luchwaza akaenda nikabidhi kwa Mganga ilikua noma sana
.
 
Dah,
Kitambo sana.
Walimu kama Tokyo (History), Mugituti, Andrew Kwayu (Head Master), Mchwampaka (Discipline), Christian, Kuna wa Physics nadhan ndio alikua msaidiz wa Kwayu, Fuvu kwenye mathematics, etc.

Bifu Azania vs Jitegemee, Pigana sana bisibisi na viwembe pale feri kulikua na kituo Cha daladala mbele ya NBC Bank au ile bustani. Bifu lilikua eti kugombea hicho kituo Cha daladala.

Bifu Azania vs Al-haramain tukikutana kwenye mechi za UMISETA Ilala. Na Kuna bifu maaarufu la Azania vs Tambaza ambalo sikulikuta. Bifu hili lilipelekea kufutwa kwa O-Level Tambaza. Wanasema kuna mwamba wa Tambaza alitoka bonden Kwa madiba na formula ya kutengeneza mabomu ya petrol, hiyo ndio iliyoipa ushindi Tambaza against Azania.

🎶 Azania Azania Azania our school,
We look at you with pride,
you are known far and wide, you are always our guide,
we will never forget you 🎶
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…