Azampesa vs Selcom Pesa. Msaada tafadhali.

Azampesa vs Selcom Pesa. Msaada tafadhali.

DexterLab

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2024
Posts
286
Reaction score
299
Salamu wadau, kwema?

Nilikuwa nataka kujua hizo huduma hapo juu, Kwa anayetumia. Yupi yup ahead zaidi ya mwenzie? Wapi Kuna makato nafuu? Nasoma komenti
 
Sijatumia ila leo nimeona jamaa anaizungumzia kwa TV. Nikakukumbuka kuna jamaa fulani mkenya alisema, huduma ya mpesa safaricom kuipiga ukaishinda kwa sasa ni kama haiwezekani kwa sababu unakuta hata ukiwa na huduma yako ya malipo yanapita humo kwao kwanza kiasi kwamba mtu anaona ni usumbufu bora atumie safaricom moja kwa moja
 
selcom pesa ndio nzuri makato yake sio makubwa ila muhimu ili ujiunge selcom utahitaji number yako ya nida
 
Salamu wadau, kwema?

Nilikuwa nataka kujua hizo huduma hapo juu, Kwa anayetumia. Yupi yup ahead zaidi ya mwenzie? Wapi Kuna makato nafuu? Nasoma komenti
Selcom Pesa wametisha zaidi. Makato nafuu kuliko. Unaweza fanya miamala mitano kwa jero pia Selcom Pesa unapata bank account hapo kwa papo. Kifupi jamaa wameweza sana
 
Azam pesa Ina miaka kama 3 sokoni ila bado haijaweza kupenya kwenye soko la ushindan. Nadhani alitakiwa kuja na laini zake kuliko huu mfumo ambao anaitumia Sasa hivi.
SELCOM kwasasa wamekuja na mfumo wa kibank. Unapakuwa app halafu unafungua akaunti, namba yako ya akaunti ni ile namba ya simu. Nimeona Makato yao ni nafuu, na kitu kizuri waliaza kuboresha mashine zao kupendana na mfumo wa kisasa. Kama watawekeza kwenye matangazo watapata wateja.
 
Wanasubir mjae waweke makato.
Hii kitu watu hawaijui naona wamesahau hata halotel kipindi cha nyuma ilikuwa na makato madogo sana ila asaivi ni kama mitandao mingine mikubwa kwa makato
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom