Azam TV waondoa chaneli za bure

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,967
4,254
Kama kuna mageuzi yaliyonisikitisha, ni uamuzi wao wa kuondoa chaneli muhimu za ndani kama ITV, Star TV, Channel 10, ...katika free to air pavkage. Kwa sasa wamebakisha chaneli 2 tu: Azam Extra na TBC (a.k.a cherekochereko tv). Ili kuangalia chaneli muhimu za ndani itakupasa kuzilipia.
Katika hali kama hii sioni haja ya TCRA kuhubiri kwa nguvu kubwa zama zile ya kuwa chaneli za ndani zitarushwa bure (bila ya mwenye kisimbusi kuzilipia). Hii kuhama kutoka analojia kwenda digitali ni mwiba kwa Watanzania wengi.
 
Mkurugenzi TCRA ni jipu lililoiva tokea mwaka Jana, nashangaa Mh Magufuri analiruka!
 
Tcra hamna kitu ni ubabaishaji tu, wanatuzuga kupiga makampuni vifaini vidogo vidogo ili kuua soo lakini Kuna hujuma kwenye decoder, Kuna hujuma kwenye gharama za simu wanajifanya hawaoni. Haya mambo ya mb8 ni hujuma za wazi kabisa kwamba watu wamekaa wamepanga watunyonye. Nakumbuka wakati mkonga wa taifa unajengwa walisisitiza itakuwa Mkombozi kwenye huduma ya Internet lakini leo gharama ndio zimepanda maradufu
 
Mwanzoni hao TCRA walijitamba ya kuwa TV kama tano hivi za ndani hazitokuwa za kulipia. Je nini kimetokea?
Au ndio tuamini ni mpango wa Nnauye kuminya uenezwaji wa habari?
Ukiona taasisi ya serikali inawekwa 'mfukoni' jua maslahi ya watu fulani vigogo yameshinda dhidi ya umma.
 
Tatizo lilipo ni kuwa azam lazima awalipe itv na star tv kila mwezi
 
Kama kuna mageuzi yaliyonisikitisha, ni uamuzi wao wa kuondoa chaneli muhimu za ndani kama ITV, Star TV, Channel 10, ...katika free to air pavkage. Kwa sasa wamebakisha chaneli 2 tu: Azam Extra na TBC (a.k.a cherekochereko tv). Ili kuangalia chaneli muhimu za ndani itakupasa kuzilipia.
Katika hali kama hii sioni haja ya TCRA kuhubiri kwa nguvu kubwa zama zile ya kuwa chaneli za ndani zitarushwa bure (bila ya mwenye kisimbusi kuzilipia). Hii kuhama kutoka analojia kwenda digitali ni mwiba kwa Watanzania wengi.
Kwa muktadha waulaghai huu TCRA inangukia kwenye Jipu.

Zuku TV haijawahi kurusha bure hizo channels za kibongo...kwa sasa inaScratch ile mbaya na ni jambo linalojirudia mara kwa mara .....Ukiwaandikia hujibiwi.
 
kuhusu zuku ku scratch dish lako litakuwa limeyumba mbona kwangu mwemwele...
 
Tuwe wakweli ni TV station gani inaonyesha TV za ndani bure?wengine tushasahau msamiati wa neno''bure''kwenye ving'amuzi.
 
Kwa muktadha waulaghai huu TCRA inangukia kwenye Jipu.

Zuku TV haijawahi kurusha bure hizo channels za kibongo...kwa sasa inaScratch ile mbaya na ni jambo linalojirudia mara kwa mara .....Ukiwaandikia hujibiwi.
Kabisa mkuu, zuku haijawahi kutoa hizo channels za bure na nasikia wanapandisha bei hadi 18,000 badala ya 15,500 kwa mwezi kuna ukweli?? Ila nina siku 2 scratch kibao, tbc ndo angalau
 
Nilikwepa kununua Startimes kwa kuchukia Scratching lakini sasa Zuku imekuwa zaidi ya Startime
 
Mimi nilisema bora ningenunua azamu ili niwe napata local channels free kumbe nao wanaondoa
 
Juzi nilinunua package ya azam sports hd nikalipia elfu 15,ile nikaangalia fresh,jana imekata ipo access denied!elfu 15 kwa cku 1!
 
Waziri Prof. Mkoma ametoka hapo TCRA, naamini anafahamu uhujumu wanaofanyiwa wananchi kwenye hivi ving'amuzi na simu. Je tumaini letu litatoka wapi? Huwa nakuwaga mgumu kuamini, japo inaonekana wazi, TCRA imewekwa kiganjani na 'wakubwa'
 
Back
Top Bottom