Azam Tv kama Ulaya tu.!!!

Azam Tv kama Ulaya tu.!!!

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
25,298
Reaction score
38,438
POPOTE utakapotulia na kutazama pambano lolote litakaloonyeshwa moja kwa moja au kwa marudio, kupitia kituo cha Televisheni cha Azam (Azam TV), usiwe na shaka, utaliona pambano maridadi.

Weka soda yako sebuleni kando kisha watazame Jerry Santo na Amri Kiemba wakichuana katikati ya uwanja wowote ule wa soka nchini huku kamera nane za Azam TV zinazorekodi pambano lao zikiwachukua kwa umaridadi.

Kamera nane zamrekodi mchezaji

Katika pambano lolote litakaloonyeshwa na Azam TV kutakuwa na kamera nane uwanjani. Huu ni wastani wa juu wa idadi ya kamera zinazopaswa kuonyesha kwa ufasaha pambano lolote la soka ingawa katika mechi za ligi nyingine au michuano mingine kunakuwa na kamera zaidi za kuonyesha mbwembwe mbalimbali.

Kamera hizi ni ghali zikiwa zimegharimu kiasi cha kuanzia dola 180,000 hadi dola 200,000 kwa kila moja. Ndani ya kila kamera kuna mchanganyiko wa mashine ya Sony huku lensi ya kuvutia matukio kwa ufasaha ikiwa ni ya kampuni ya Cannon. Kamera mbili zitakuwa zinakaa katika kila nyuma ya lango la uwanja. Kamera hizi mbili zina kishikilio kirefu na kuifanya ining’inie katika eneo lote la nyuma ya lango kama tunavyoona katika mechi za Ligi Kuu England na michuano mbalimbali.

Katika pande mbili za uwanja, karibu na benchi la kila timu kutakuwa na kamera mbili ambazo watu wanaorekodi mpira wataweza kukimbia nazo huku na kule kwa ajili ya kutokana matukio yanayoendelea katika upande wa kulia na kushoto kuanzia pale anapokaa mwamuzi wa akiba.

Kamera ya nne ni ile iliyosimama katikati ya uwanja, karibu na mwamuzi wa akiba. Kamera hiyo huwa inasimama ilipo na haisogei. Dhumuni kubwa ni kuzivuta kwa karibu sura za wachezaji au mwamuzi inapohitajika.

Jukwaani kuna kamera kubwa zaidi, pengine kuliko zote. Mtambo huu unarekodi mechi yote kwa juu na ni nzuri kwa mwelekeo mzima wa ‘muvu’ kwa timu zote mbili. Lakini pia kando ya kamera hii kuna kamera nyingine kubwa ambayo nayo inadaka kwa haraka matukio ya ndani ya uwanja.

Pia bado kuna kamera ya saba ya mtu ambaye anazunguka katika kando ya uwanja kwa ajili ya kuchukua mahojiano kabla ya mechi, wakati wa mapumziko na mechi ikiisha. Kamera zote hizi saba zina uwezo wa kurekodi na kuvuta kwa karibu tukio lililo umbali wa mita 400 kutoka zilipo. Hii ni sawa na muunganiko wa viwanja vinne vya mpira!

OB Van ya kisasa zaidi barani Ulaya

Kamera hazina kazi yoyote kama huna OB (Outside Broadcasting)Van ya kisasa. OB Van ni gari linalokamata matangazo uwanjani na kwingineko nje ya studio kutokea katika kamera na kurusha katika setalaiti iliyo hewani. OB Van ya Azam TV ni ya kisasa zaidi ambayo ni zaidi ya OB Van zinazotumiwa na kampuni nyingine za Afrika.

Ikiwa imegharimu kiasi cha Euro 4 milioni, OB Van hiyo ililetwa nchini na Kampuni ya Broadcast Solutions ya Ujerumani chini ya mhandisi wake maarufu, Armando Santos ambaye ameondoka nchini jana Ijumaa baada ya kuendesha mafunzo maalumu ya jinsi ya kuitumia OB Van hiyo.
chanzo Mwanaspoti:

Hongereni Azam kwa kuonyesha utofauti kwenye soka la Tanzania.
 
Pumba tupu.
Watu wanataka kuona mpira 'live' na sio hadithi za kamera. Hizi hadithi za kamera zinamfaa Muhidini Issa Michuzi na Ludovic lakini sio sisi hapa JF.
 
chanzo Mwanaspoti:

Hongereni Azam kwa kuonyesha utofauti kwenye soka la Tanzania.

Jamaa kachukua posho ili awaandikie hizo habari. Haraka ya nini walianza kuonyesha si tutaona? Mwenye haambiwi tazama, ataona mwenyewe!
 
Watazamaji sisi tunataka end product...

Mathalani Tanzania tuna maliasili chungu tele lakini angalia maendeleo sasa...

Hivyo hata hao Azam Media waache kujitapa sisi tunawasubiri hapo watapoanza kwenda hewani tuone ubora wao...
 
sawa vfaa bora, tungojee na mtiririko mzuri wa picha, sio kichwa kikubwa akili ndgo kma kazi nduga..
 
Mkuu tupe hiyo channel ya hiyo TV tuitafute. Hatutaki hadithi, tunataka vitendo Bwana.

Tiba
 
Hongereni Azam!!nategemea kuwa mbali na kuonyesha mechi pia mtakuwa wawakilishi wazuri kwa magamba,eeh! Si ndiyo wanawaweka mjini?cc-Sibuka
 
Mkuu tupe hiyo channel ya hiyo TV tuitafute. Hatutaki hadithi, tunataka vitendo Bwana.

Tiba

Bado mpaka wazindue ving'amuzi vyao vya "Azam".!
 
Hongereni Azam!!nategemea kuwa mbali na kuonyesha mechi pia mtakuwa wawakilishi wazuri kwa magamba,eeh! Si ndiyo wanawaweka mjini?cc-Sibuka

Hongera umeshaiona au ndio Sifa za kijinga?
 
Ni mwanzo MZURI wa mapinduzi ya media, nadhani wengine nao 'watajaribu'.
 
"kaiona" kwenye gazeti la mwanasport la leo

Hapo ndipo huwa Nashangaa.... Ile Story ya mke na mume kupanga wakipata pesa wanunue kuku wafuge na mke kazi yake iwe ni kusafisha Banda la hao kuku watakaowanunua mwisho wa mipango mke akakataa kujakuwa msafisha banda akitaka mume ndie awe atakayekuwa anasafisha banda ...hawakuelewana ukawa ugomvi mkubwa walipopatanishwa wanaulizwa banda na kuku wapo wapi wakasema hawajapata hizo Pesa....

Mtu anasifia kitu ambacho akipo....

Akawaulize wana Mtwara mji wao kuwa wa Viwanda mwishowe wameambulia Mabomu!
 
Ni mwanzo MZURI wa mapinduzi ya media, nadhani wengine nao 'watajaribu'.

Kiukweli wanahitaji kutiwa moyo, acha wafanye. wakishindwa tutajua walijaribu wakashindwa.

Sio wale viongozi wetu wanatuonyesha picha wakitia saini makaratasi ya ujenzi wa uwannja kumbe blah blah tu.
 
Hapo ndipo huwa
Nashangaa.... Ile Story ya mke na mume kupanga wakipata pesa wanunue
kuku wafuge na mke kazi yake iwe ni kusafisha Banda la hao kuku
watakaowanunua mwisho wa mipango mke akakataa kujakuwa msafisha banda
akitaka mume ndie awe atakayekuwa anasafisha banda ...hawakuelewana
ukawa ugomvi mkubwa walipopatanishwa wanaulizwa banda na kuku wapo wapi
wakasema hawajapata hizo Pesa....

Mtu anasifia kitu ambacho akipo....

Akawaulize wana Mtwara mji wao kuwa wa Viwanda mwishowe wameambulia
Mabomu!

ah ah haa, huo ndio ukweli, tusubiri atakapoanza kuonysha ligi na katika ubora unaoridhisha, pongezi zake tutampa tu, sasa hv mapema mno.
 
chanzo Mwanaspoti:

Hongereni Azam kwa kuonyesha utofauti kwenye soka la Tanzania.

asante sana mkuu kwa kuliona hili watu hawajiuliziulizi kwenye hela bana... Grande SSB
 
Back
Top Bottom