Azam Media tunaomba mechi ya UEFA champions league live

wakikosi

JF-Expert Member
Feb 28, 2015
1,354
1,485
Azam media imeshakuwa media kubwa sasa lakini mimi hawanifurahishi na jambo moja tu, hawaoneshi mashindano ya club bingwa Ulaya (Uefa Champions league). Ninawaomba muwe mnatuletea live mashindano hayo.

Lakini pia kama mnaonesha mashindano fulani acheni kuonesha kwa kupitia ZBC2, ,maana channel hiyo mara ibada mara mpira sasa hata mtu unashindwa kufuatilia mpira vizuri.

Kwakweli nimechoka kuondoka nyumbani kwenda kucheki UCL kwenye media nyingine wakati ninyi azam naamini mnaweza kutuletea wateja wenu live UEFA champions league tukiwa na familia zetu nyumbani.
 
wataongeza malipo kwa mwezi kama huwajui vizuri azam
Kama huduma ni bora tutalipia tu,tatizo mtu una TV nyumbani lakini unalazimika kumuacha Mke wako kitandani SAA 4 usiku kwenda kwenye baa au banda la mitaani ambako kuna super sport.
Sasa kuangalia mechi za usiku uswahilini nako tabu unaweza kupigwa roba na kuibiwa pindi unarudi au lolote linatokea
 
Hiv Zbc2 ni mali ya bakhresa?
Hata sijui lakini mara nyingi huitumia kurusha mechi huko,tatizo zbc2 ni ya dini kama kukiwa na mechi Kali lakini pia muda huo kuna ibada inabidi irushwe ibada badala ya mechi
 
Back
Top Bottom