Azam Media hii ni sawa lakini?

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Kwanza hujiuliza 'chanel' ya UTV imejichomeka vipi? Zamani tulikuwa tukipata habari kupitia Azam 2 baada ya sekeseke la leseni ndipo huyu UTV akaonekana.

Kinachonishangaza sasa ni kitendo cha uongozi wa TV hii kuonesha EPL kupitia UTV ambayo wameifanya ya bure kwa maana hata kama hujalipia unaipata lakini ligi yetu huwezi iona mpaka ulipie ndipo upate hizo 'chanel' za michezo.

Akili gani hii?
 
Wabongo ni wangese sana laiti wangejua fedha aliyotumia kuwekeza wasingelala wangelipia hiyo 18,000 kwa mwezi. Ila mijitu ina kazi ya kulalama tu.
 
Moja ya kitu kibaya kwenye maisha ni kutokujua jambo alafu ukaliongelea.
.
Mechi za EPL zinazorushwa na Azam UTV, Kiss tv Kenya na EATV (sina uhakika kama bado wanarusha) ni FTA na zinatolewa na Kwèse Sports.
Sawa mkuu, lakini hiyo 'chanel' ya UTV ni ya michezo??????
 
Wabongo banaaa hua hatuna shukurani, tunachojua ni kulalamika tu,
Tukitendewa ubaya tunalalamika, tukitendewa wema pia tunalalamika.
 
I wish Azam Media mtaiweka na ile Tv yetu pendwa ya Kikatoliki (Tv Tumaini) kwenye king'amuzi chenu, badala ya Upendo Tv tu.

Nimeiona ipo Startimes. Tafadhali kama inawezekana lakini.
 
Sawa mkuu, lakini hiyo 'chanel' ya UTV ni ya michezo??????
Kwani lazima iwe ya michezo ndo waonyeshe michezo......mbona kuna channel zinaonyesha miziki ila hazitambuliki kama ni channel za miziki. ...jambo dogo sana hilo
 
I wish Azam Media mtaiweka na ile Tv yetu pendwa ya Kikatoliki (Tv Tumaini) kwenye king'amuzi chenu, badala ya Upendo Tv tu.

Nimeiona ipo Startimes. Tafadhali kama inawezekana lakini.
Mkuu huwa naisikia tu hiyo tumaini tv sijawahi kuitazama kabisa vipi ubora wa vipindi vyao?
Upande wa radio nawakubali sana hasa kucheza nyimbo zenye utulivu wa kiibada.
 
Back
Top Bottom