Azam kumbukeni pana 'points' 3 Yanga imewekeza TFF

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,711
Reaction score
1,738
Timu ya Azam hivi sasa inatembea kifua mbele kwa kuwa inaongoza ligi, hivo kuwa na tegemeo la kuwa bingwa wa nchi yetu kwa mara ya kwanza lakini wanasahau kuwa timu ya Yanga imekata rufaa dhidi ya timu ya Mgambo japo muda ulishapita lakini TFF wakaipokea na bado sijasikia majibu yake. Nionavo TFF wanasubiri matokeo yatakayo pelekea Azam isiizidi Yanga 'points' 3 ndipo watoe uamuzi dhidi ya Mgambo na hivo Yanga kutangazwa mshindi.
 
Kutokana na vigezo walivyovitoa yanga, je yule mchezaji alistahili kucheza ligi?? kama hakustahili, Mgambo wakipokonywa pnt 3 kwenye mechi zote walizoshinda watakuwa wameonewa?,
 
kama mgambo hawakufuata taratibu zote basi ni lazima yanga ilambe alama zake tatu kama kanuni zinavyotaka, na wala si dhambi kuchukua hizo alama. jana nimemsikia huyo mchezaji mlalamikiwa akihojiwa, akadai yeye ni mwenyeji wa Tanga, yule mtangazaji akaanza kumsalimia kwa lugha ya huko Tanga yule jamaa akachemka na kujitetea kuwa amekulia dodoma. bado anatia mashaka ingawa kutojua lugha ya kwake si kigezo kikuu
 
Timu ya Azam hivi sasa inatembea kifua mbele kwa kuwa inaongoza ligi, hivo kuwa na tegemeo la kuwa bingwa wa nchi yetu kwa mara ya kwanza lakini wanasahau kuwa timu ya Yanga imekata rufaa dhidi ya timu ya Mgambo japo muda ulishapita lakini TFF wakaipokea na bado sijasikia majibu yake. Nionavo TFF wanasubiri matokeo yatakayo pelekea Azam isiizidi Yanga 'points' 3 ndipo watoe uamuzi dhidi ya Mgambo na hivo Yanga kutangazwa mshindi.

Duh!
TFF vipi? imerudia enzi za FAT?
Hakika mkuu Jamal Malinzi unakazi kwelikweli. Tufafanulie na hili je ni kweli muda ulikuwa umepita?
 
Last edited by a moderator:
Timu ya Azam hivi sasa inatembea kifua mbele kwa kuwa inaongoza ligi, hivo kuwa na tegemeo la kuwa bingwa wa nchi yetu kwa mara ya kwanza lakini wanasahau kuwa timu ya Yanga imekata rufaa dhidi ya timu ya Mgambo japo muda ulishapita lakini TFF wakaipokea na bado sijasikia majibu yake. Nionavo TFF wanasubiri matokeo yatakayo pelekea Azam isiizidi Yanga 'points' 3 ndipo watoe uamuzi dhidi ya Mgambo na hivo Yanga kutangazwa mshindi.

Sio TFF tu, sheria na kanuni lazima zizingatiwe wakati wote. Kwani hili suala la mchezaji kutokuwa halali lina tofauti gani na lile la Simba dhidi ya TP Mazembe kwenye CAF? Kunya anye kuku bata anaharisha!
 
Kwa utaratibu wa sasa, rufaa inayohusu usajili haitoi point za mezani, ila timu iliyofanya udanganyifu ikakatiwa rufaa itatozwa sh. 1,000,000/= kila mechi iliyomchezesha mchezaji anayelalamikiwa, na afisa wa TFF aliyeidhinisha usajili wake atapewa adhabu. Matokeo ya uwanjani yanabaki kama yalivyokuwa
 
Back
Top Bottom