Azam fc tv hewani ndani ya channel ten!!!

chamakh

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
1,024
1,261
Wadau,
Naona Azam FC wamefanya mapinduzi ya kweli ya kimaendeleo kwa soka ya Tanzania, kwani wao tayari wameweza kurusha hewani kipindi chao cha habari zao kinachoitwa Azam FC TV, Katibu MKuu wa Azam yupo studio Channel Ten kwa sasa akielezea mipango yao na anaonyesha baadhi ya facilities zilizopo kwenye uwanja wao wa Chamazi, kwa kweli ni za viwango vya juu sana kwa mpira wa kiafrica na anasema malengo yao wao ni kuwa miongoni mwa klabu bora barani Africa

Kiukweli nimewakubali Azam kwa mipango yenu na endeleeni hivyo hivyo labda sisi wengine tutaamka. Kuzinduliwa kwa kipindi hiki naona ni aibu kubwa kwa uongozi wa klabu yetu ya Simba ambao ulikuwa wa kwanza kuzindua SIMBA TV lakini twashangaa ni karibu miezi sita sasa kipindi hakijaenda hewani wakati kumetokea matukio mengi sana ya kuweza kujaza vipindi hata kumi, kuanzia mwisho wa ligi ya msimu uliopita, mechi za kombe la shirikisho, kombe la kagame, usajili, pre-season preparations, mashindano ya BancABC, uzinduzi wa msimu kila tarehe 8 Agosti (Simba Day) , Simba Ladies, ligi mpaka sasa, mechi ya watani na matukio kadha wa kadha ambayo yangeweza kurekodiwa. Sielewi nini kilichangia, wadhamini sidhani kwani mpaka sasa tunao Kilimanjaro na Vodacom kwa kuanzia na hawa siamini wangeshindwa kudhamini kipindi bado hujazungumzia MeTL, Bin SLUM, CXC, Aurora na wadau wengi walio mashabiki wa Simba

narudia tena hongereni sana Azam FC kwa kutufungulia njia
 
mkuu Ndetichia nilikutarajia uwe studio leo, nashangaa upo Mbeya au kwa kuwa kipindi sio Live?
 
Kuna timu moja yenyewe ikiambiwa ionyeshe kiwanja sijui itaonyesha nini. Timu ya zamani sana. Yenyewe inawekeza kwa marefa.

Fofader una akili sana,hili ulilolisema hapa ni la msingi sana basi tu..wadau wanajifanya hawajaliona
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom