Azam F.C sio mbadala wa club za Simba na Yanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azam F.C sio mbadala wa club za Simba na Yanga

Discussion in 'Sports' started by TIQO, Aug 2, 2012.

 1. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Wapenzi wengi wa soka walikuwa wanajua kuwa timu ya Azam ndiyo itakuwa mbadala kwa soka letu la bongo kumbe ni danganya toto, hii inatokana na bosi wa Azam kuingilia kazi ya kocha kwa kumpangia wachezaji wa kutumia na alipo kaidi akaamua kumtupia vilago kocha.
  Kwa hiyo bosi akinuna tu kwa vile mchezaji kamkumbatia mchezaji wa Yanga au Simba simtaki na kocha akiona hoja haina mashiko na akamchezesha basi mchezaji pamoja na kocha vibarua vinaota nyasi kama hivi tunashuhudia. Mambo ya kupangiwa wachezaji au mambo ya kuingilia uhuru wa walimu tulikuwa tunasikia yapo Simba na Yanga na tulikuwa tunaamini Azam itakuwa timu bora na ya kisasa kumbe nayo ni timu ya kienyeji kwa mtindo huu Azam haifiki mbali itapotea kama ilivyo potea Kajumlo au African Lyon ngoja tusubiri.
   
 2. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Habari zinasema kwamba, mapema baada ya mechi ya Nusu Fainali ya Kagame, kati ya Azam na AS Vita ya DRC, Stewart aliitwa na kuambiwa asimtumie tena Ngassa kwa kitendo cha mchezaji huyo kwenda kuibusu na kuivaa jezi ya Yanga, baada ya kufunga bao la ushindi.
  Lakini Stewart katika kikao hicho, kwanza alimtetea Ngassa kutokana na kufunga bao la ushindi na kumuelezea kama mchezaji muhimu kwake, lakini msimamo wa bodi ulikuwa ni asipangwe tena.
  Katika fainali, Stewart alimvalisha jezi Ngassa akamuanzishia benchi, lakini kama ilivyokuwa kwenye Nusu Fainali alimuingiza kipindi cha pili timu ikiwa nyuma kwa 1-0 na mwisho wa mchezo ikashinda 2-1 yeye akifunga la pili, dhidi ya Yanga pia alimuingiza timu ikiwa nyuma kwa 1-0.
  Lakini Ngassa alishindwa kurudia kile alichofanya kwenye mechi na AS Vita na Yanga ikashinda 2-0.
  Kwa sasa mazungumzo yanaendelea kati ya Yanga na Azam juu ya Ngassa ili mchezaji huyo arejee Jangwani, lakini wakati huo huo, Simba nao wameweka dau la Sh. Milioni 25 katika 50 zinazotakiwa na Azam ili kumuuza mchezaji huyo.
  Mbali na Ngassa, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy' pia yuko katika wakati mgumu na jana inadaiwa alionekana akilia wakati anazungumza na kiongozi mmoja wa Azam, akiuliza ni lipi kosa lake.
  Sure Boy, ambaye ni mtoto wa kocha wa timu ya vijana ya Yanga, Abubakar Salum ‘Sure Boy' jana hajafanya mazoezi na leo pia, naye pia akituhumiwa kucheza kinazi katika mechi dhidi ya Yanga.
  Stewart anakuwa kocha wa nne ndani ya miaka minne kufukuzwa Azam, tangu Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin, Mbrazil mwingine.
   
 3. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Stewart bora arudi akafundishe Zanzibar heroes akale urojo na tende
   
 4. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kuandika hapa hii team ni USHUZI mtupu,baadhi ya watu wakanipinga lkn ni ukweli utakaokuja kudhihirika na wote muda si mrefu kuwa hakuna contribution yeyote itakayoweza kuwezeshwa na uwepo wa hii team ambayo ilianza kuteka akili za watu wengi kuwa mkombozi wa soka letu,kwanza very soon itakuja kuthibitishwa kama ni mojawapo ya team inayochangia kuua vipaji vya Vijana ambao wangeweza kulisaidia hili Taifa,angalia issue ya Ngassa,angalia issue ya Seleman Kassim "Serembe" ilivyokuwa,walisema amekwisha kumbe Mshikaji bado moto ile mbaya amewaumbua,angalia walivyomtoa Marehemu Mafisango (RIP) eti wakawapa Simba mchezaji (Mafisango) na pesa in exchange of Abdulrahim Humud,Marehemu akawaumbua faster,sasa wamemgeukia Salum Aboubakar....yaani inasikitisha sana,pamoja na mchango wake wote katika kuwezesha kuifikisha pale Azam bado wanamuona msaliti,shutuma za kis***e mpaka Dogo akalia,what is this?
  Haya hakuna mtu asiyeiona kazi ya Mtaalamu Stewart...kosa lake ni kushindwa kuifunga Yanga na kumchezesha Ngassa fainali,hivi kweli haya ni makosa ya kumsababishia mtu kufukuzwa kazi ukisahau mambo mazuri yote aliyoiletea Club?!!!
  Nakubaliana 1 kwa 1 na mleta mada kama hawatabadilika badala ya kuzidi kusonga mbele itashika njia za kina Kajumulo,sisi tupo.
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Azam wananikumbusha Man city kua ni team yenye hela na hata mafanikio yao yatakua coz of pesa. Team ka Yanga imetoka mbali ni team asilia
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  duu bin zubeiry na wenzake ni moja kati ya waandishi makanjanja ndio maana mambo ya ngasa yanatuvuruga tu ataenda simba na kama ataki aache soka ngasa kabugi na watu hawalioni hilo wanamlaumu tu kila la kheli azam fc na maamuzi yao..
   
 7. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,991
  Likes Received: 3,740
  Trophy Points: 280
  mbona kuna pretenders wengi tu huko miaka ya nyuma walikuja kama azam lakini wakapotea ghafla kutoka kwenye hii medani?
  majina kama pan afrika, tukuyu stars, mtibwa, etc yatakuwa yana-ring bell, siyo?

  dominance ya simba na yanga haiwezi kuondolewa na hivi vitimu vinavyomilikiwa na hawa matajiri wezi na wakwepa ushuru. hawa matajiri unakuta tayari wana affiliation na simba au yanga - so inakuwa rahisi sana kukumbwa na mawimbi ya kisiasa ya timu hizi mbili, just like ilivyotokea kwa ngasa na azam (ambao mmiliki wake anajulikana ni mnazi mkubwa wa simba). what did you expect?

  inahitajika mabadiliko makubwa (radical change) ya kisera zaidi kwenye football structure yetu ili kuua dominace ya hizi timu mbili, dominace ambayo kiukweli ndiyo inayodumaza soka letu.
   
 8. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  hakuna kitu muhimu kama nidhamu
   
Loading...