Azam decoder wamezima channel za bure (FTA)

Azam decoder wamezima channel za bure (FTA)

Hazchem plate

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Posts
11,053
Reaction score
15,515
Habari wanajukwaa.
Hivi karibuni kumekuwa na mvutano wa mamlaka ya Mawasiliano TCRA na Warusha matangazo kwa njia ya Terrestrial na Satellite kwa Maana ya Wamiliki wa Ving'amuzi Vya Tanzania ambavyo ni Azam, Star media, Continental, Digitek, Ting na Multichoice (DStv)

Mvutano huu nadhani ni matokeo ya watanzania kulalamikia kulipishwa huduma ya Channel za bure. Ikumbukwe mara kadhaa mamlaka ya mawasilino imetoa notisi ikiwataka warusha matangazo kuto kutoza pesa kwa channel za bure

Hivi karibuni TCRA imetoa notisi ya nia ya kutaka kufuta leseni za kurusha matangazo baada watoa huduma kukaidi agizo la mamlaka.

Mimi binafsi nimekuwa nikfuatilia kwa karibu Sakata hili. Ila hatimae nimeona AZAM wameona wazitoe Channels za Bure isipokuwa TBC1. Tv kama ITV, Star TV, Ch. 10 na nyingine baadhi ambazo ni za maudhui ya bure hazionekani. Hivyo imebaki TBC1, Wasafi TV na ZBCs ndio zinaonekana.

Kwa maana rahisi AZAM naona anatekeleza Agizo la kurusha FTA Bure bila kulipia ila sasa amezitoa hizo channel nyingine kwenye King'amuzi chake.

Kwa maana hiyo Ukiwa umeishiwa kifurushi ukiwa na na AZAM Decoder utaweza kuona TBC may be na Wasafi na labda ZBCs ila sahau kuhusu izo channels nyingine Local

"TCRA wamemwaga Ugali, Azam wamemwaga mboga"
View attachment UFAFANUZI_KUONDOA FTA_DTH - August, 2018.pdf
 
Dstv wenyewe wamebakiza tu ITV, STAR TV NA TBC zingine wametoa
 
Naona Wachina (Startimes) waliishika roba serikali/TCRA! Inavyoelekea Wachina waliwakomalia TCRA kwamba, wakitaka Startimes warudishe chaneli 5 za bure basi TCRA nao wahakikishe Pay TVs (DSTV, Azam, Zuku) nao wanaziondoa hizo channels kwenye ving'amuzi vyao!

DSTV na wenzake wakiziondoa hizo channels, wateja wa DSTV ambao wanadhani maisha hayaendi pasipo na ITV na wenzake hivi sasa watalazimika kuwa na king'amuzi cha Startimes na kukifanya nyumba ndogo!!!

Kwa mtaji huu wa akina Azam kuwapiga chini akina ITV, basi kaeni mkao wa kula wale wote waliokuwa wanasubiria channels za bure!
 
TANZANIA INGEKUA KAMA NCHI NYINGINE SAA HIZI UNGEKUTA WANANCHI TUNAISHTAKI SEREKALI NA KAMPUNI ZA VING, AMUZI KWA KUTUDANGANYA TUTAONA CHANEL 5 BURE LAKINI BAADA TU YA KUZIMA ANALOGY WANANCHI TUKAANZA KUISOMA NAMBA, YAANI KILA CHANEL TUNALIPIA ISIPOKUA TU TBC 1. KINYUME NA TULIVYOELEZWA NA TCRA HUKU STAR TIME WAKIJITETEA UONGO ETI WANA DECORDER ZA AINA MBILI YA BURE NA YA KULIPIA. SASA MBONA HAWAKUTUTAARIFU WANANCHI TANGU MWANZO? AU KWAKUA WANANCHI WA TANZANIA NI WANYONGE WANYONGE KWENYE KILA KITU NDIO SABABU TUNAZIDI KUONEWA?
 
Hasara tunapata wote kasoro startimes..azam bila local channel watakosa soko,huku wenye hivyo vingamuzi vya azam sijui watavifanyia nini!!
 
Hapa mi naenjoy na frresat yangu
 

Attachments

  • IMG_20180809_170440.jpg
    IMG_20180809_170440.jpg
    77.4 KB · Views: 120
Back
Top Bottom