Azam decoder wamezima channel za bure (FTA)

Azam decoder wamezima channel za bure (FTA)

Wamedecleare
IMG-20180810-WA0020.jpg
 
ukitaka bure Nunua dishi ft 6 au 8

na decoder ya fta


acha watu wafanye biashara



Habari wanajukwaa.
Hivi karibuni kumekuwa na mvutano wa mamlaka ya Mawasiliano TCRA na Warusha matangazo kwa njia ya Terrestrial na Satellite kwa Maana ya Wamiliki wa Ving'amuzi Vya Tanzania ambavyo ni Azam, Star media, Continental, Digitek, Ting na Multichoice (DStv)

Mvutano huu nadhani ni matokeo ya watanzania kulalamikia kulipishwa huduma ya Channel za bure. Ikumbukwe mara kadhaa mamlaka ya mawasilino imetoa notisi ikiwataka warusha matangazo kuto kutoza pesa kwa channel za bure

Hivi karibuni TCRA imetoa notisi ya nia ya kutaka kufuta leseni za kurusha matangazo baada watoa huduma kukaidi agizo la mamlaka.

Mimi binafsi nimekuwa nikfuatilia kwa karibu Sakata hili. Ila hatimae nimeona AZAM wameona wazitoe Channels za Bure isipokuwa TBC1. Tv kama ITV, Star TV, Ch. 10 na nyingine baadhi ambazo ni za maudhui ya bure hazionekani. Hivyo imebaki TBC1, Wasafi TV na ZBCs ndio zinaonekana.

Kwa maana rahisi AZAM naona anatekeleza Agizo la kurusha FTA Bure bila kulipia ila sasa amezitoa hizo channel nyingine kwenye King'amuzi chake.

Kwa maana hiyo Ukiwa umeishiwa kifurushi ukiwa na na AZAM Decoder utaweza kuona TBC may be na Wasafi na labda ZBCs ila sahau kuhusu izo channels nyingine Local

"TCRA wamemwaga Ugali, Azam wamemwaga mboga"
View attachment 831031
 
Juzi na jana king'amuzi cha Azam local channel zilikuwa TBC,ZBC na WasafiTV pekee, leo naangalia WasafiTV nayo pia imeondolewa.
 
Hizi local Chanel hawa Zuku, Dstv, Azam na wengineo wanapewa bure au wanazinunua? Na kama wanazinunua kwa nini walazimishwe kuzitoa bure? Mfumo wa kununua tulishauzoea, TCRA wazindue king"amuzi chao cha bure walete ushindani kama wanaona mambo ni rahisi. TTCL imezidiwa na Halotel kampuni ya juzi tuu, OK ngoja tuone hili game!!
 
Back
Top Bottom