Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Si dhani kama wanashaurika hawa watu? Ila mimi najuwa wanafahamu kila kitu kinachoendelea na wanauwezo wa kukomesha kabisa hata bila kuundwa hiyo tume ambayo itachukua kodi za wananchi.
===================
Asasi Za Kiraia (AZAKI) zaidi ya 300 nchini zimewasilisha mapendekezo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), zikitaka kuundwa kwa tume huru ya kiraia kuchunguza matukio ya utekaji na kupotea kwa watu, pamoja na serikali kusaini mikataba ya kimataifa ya kulinda watu dhidi ya kupotezwa kwa kulazimishwa.
Kupitia Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, AZAKI hizo zimesema kuwa mapendekezo hayo yanahusisha pia hatua za haraka kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ikiwemo kukomesha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, kulinda uhuru wa vyombo vya habari na kuhakikisha mazungumzo ya kitaifa yanafanyika kwa ajili ya maridhiano na umoja wa kitaifa.