Awamu zilizopita kulikuwa na maadhimisho ya kila mwaka?

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
Nakumbuka kusikia siku 100 za Rais ila sikumbuki kusikia maadhimisho ya mwaka mmoja, miwili, mitatu, minne au mitano ya serikali ya awamu yoyote iliyopita isipokuwa hii ya awamu ya sita. Kama nasema uongo nisahihishwe.

Hili la maadhimisho ya mwaka mmoja, mara miaka miwili ya Mama ni fitina tu dhidi ya tarehe 17 March na linafanywa na machawa kwa maslahi ya matumbo yao.

Ibada za kumbukumbu za marehemu ni imani ya kanisa katoliki. Walioikuza sana hii ya tarehe 17 March ni hao hao machawa kwa fitina zao na wakajikuta mwaka Jana wamekimbilia Chato wote. Mwaka huu wakataka isifanyike kabisa kwasababu ya fitina hizo hizo baada ya kulikoroga mwaka Jana.

Sasa matokeo yake wameandaa maadhimisho ya miaka miwili ili Rais ashiriki na asiende Chato. Kwani kusingekuwa na maadhimisho na Chato asiende ingekuwaje?

Ukitaka kujua kuna fitina na unafiki mkubwa DC ambaye inasemekana ameteuliwa kumdhibiti Kalemani baada ya kufutiwa mashtaka ya ufisadi juzi aliingia mitini kwa hofu. Mama Samia akawakilishwa na mtoto wake sijui ni shangazi yake!?

Kama kuna kosa ambalo atalifanya Mama mbele ya Mungu, mbele ya mila za kiafrika na m ele ya nafsi yake mwenyewe ni kumbagaza Magufuli. Karma itamletea shida mbeleni. Asikiaye na Afahamu. Chawa ni wagombanishi. Penye mgogoro ndio wanapopata hela na maisha
 
Kweli kabisa.
Ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Kizuri hata kisiposifiwa, kitaonekana tu. Ukiona sifa zinazidi ujue kuna kisicho sawa mahali
 
Back
Top Bottom