Awamu ya Tano ya Serikali ya JPM, nini tofauti inatufanya tushangae?

enery

JF-Expert Member
Aug 21, 2015
368
437
Nimejaribu kukaa na kutafakari na kujaribu kuziangalia tawala zote toka ya kwanza hadi ya tano sasa, nimeona kuna kitu kinaitwa UTAWALA na UONGOZI. Awamu ya kwanza ilikuwa UTAWALA kuwa lazima ufanye atakavyo au rekebisha mawazo yako yawe hivi uko sahihi ila hapa fanaya hivi. Awamu ya pili ikawa UONGOZI kuwa ni ruksa kufanya utakacho biashara sawa, oa mtoto wa kiarabu sawa. Awamu ya tatu ikawa UTAWALA kuwa nimesema magari ya serikali mwisho kutembea saa 12 wananchi mkikuta gari ya serikali zaidi ya saa 12 nahali pasipo stahili kuwepo piga mawe kesho dereva ataeleza alikuwa wapi? Awamu ya nne UONGOZI kuwa umevurunda hapa nakuhamishia pale kaendelee fanya yako. Awamu ya tano UTAWALA umekosea nakutumbua nenda nyumbani wengine wanakuja fanya kazi wako wengi wanatafuta kazi. Lakini nikajaribu kuzama kidogo nikagundua kuwa katiba ina vipengele viwil ambavyo raisi anaweza simamia atakapo, kuwa kuna SHALL na MAY. Atachagua asimamie SHALL lazima ufanye atakavyo na si vinginevyo. MAY waweza fanya ukitaka ama ukaacha. Sasa utawala huu naona upo katika SHALL, naomba maoni yako pia
 
Back
Top Bottom