Awamu ya tano: Shauri nini kifanyike katika kuboresha Elimu

2kimo

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2014
Posts
2,029
Reaction score
2,072
Wadau wakati umefika kwa wananchi kushiriki kwa vitendo katika kuleta tija kwa taifa letu. sehemu ya kwanza ni kutafuta mbinu za kutatua changamoto za kielimu.
Je wadau tunaweza kumshauri raisi wetu juu ya kuimarisha elimu na kuifanya elimu yenye tija kwa taifa?
Naomba michango yenu ktk uzi huu.
Kwa upande wangu nafikiri mambo haya yafuatayo yanaweza kutuletea tija.
1. Wadau kupata nafasi zaidi ya kuchangia katika mbinu za uboreshwaji wa huduma hii muhimu katika jamii.
-vyuo vikuu na wasomi waongoze makongamano katika kutoa tafakari juu ya nini kifanyike katika kuleta na kuimarisha elimu yetu. si vema kuwa na mijadala isiyo na kikomo, lakini katika siku 100 za mwanzo wa awamu ya tano jambo hili lilitakiwa lipewe namba moja ili baada ya hapo tuanze kuonesha muelekeo mpya.
2. kuweka vigezo vya ubora, tuzo na adhabu kwa shule na taasisi zingine za elimu.
Kutengeneza vigezo kwa taasisi za kielimu ili tuwe na sifa zinazoendana katika mashule yote hapa nchini.
yes huwezi kosa uwepo wa shule zenye viwango vya juu, kati na chini lakini shule zipimwe kwa vigezo, daraja za ubora zibainishwe na taasisi husika iwe halmashauri au taasisi ya dini, shirika au mtu binafsi zipewe majukumu ya kufanyia uboreshwaji wa viwango katika vipindi maalum na kushindwa kufanya hivyo taasisi husika inyimwe haki ya kuendelea kutoa huduma na ifidie gharama za kuwahamisha wanafunzi na penalt ya usumbufu kwa taasisi. pale inapogusa halmashauri, basi na mkurugenzi wa halmashauri husika na maofisa wa elimu nao waondolewe katika nafasi zao kwa kushindwa kusimamia elimu.
Kwa vyuo vyote kuanzia vile vidogo vinavyotoa certificates pekee hadi universities, serikali isigharamie chochote ikiwemo kupeleka wanafunzi kama hawatofikia viwango ailivyowekwa.
-zawadi ikiwemo pamoja na pesa na medali kwa taasisi zitakazofanya vema pamoja na mkurugenzi na maofisa wa elimu.
3. Uwepo wa scholarships kwa wanafunzi wanaofanya vema.
kwa mpango uliopo sasa wa wanafunzi kusoma bure hadi A-level, wanafunzi wanapaswa kuwa na eneo jingine la kushindania inapokuja kumaliza elimu ya sekondari. Suala la bodi ya mikopo kutoa nafasi ya mikopo just kwa kufiwa na wazazi na kuwaacha watoto wengine wenye wazazi wa kipato cha kati lakini wenye ufaulu mzuri katika masomo yao ya sekondari kuishi kwa kutaabika wakiwa vyuo vikuu pia linapunguza ufanisi kwa wanataaluma wetu. Wale wenye umri wa kati watakumbuka kipindi kabla ya kluanza bodi ya mikopo, serikali ilikuwa inagharamia wanafunzi wote wenye alama za ufaulu wanapoingia vyuo vikuu. hapa ilikuwa ni kutokana na nafasi zinazopatikana UDSM, Mzumbe na Sokoine,. pamoja na vyuo vingine hasa vile vya ufundi kwa FTC. wote tulisoma na kupambana kupata nafasi hiyo, kwa hiyo ushindani na juhudi zilitumika kufikia malengo ya kuifikia nafasi hii hadhimu. mambo yamebadilika hasa baada ya kuanzishwa kwa bodi ambapo suala la kupata ni bahati nasibu tu, ufaulu sasa si kigezo, lakini vigezo vingine visivyo na tija ndio vimepewa kipaumbele zaidi, kwa bahati mbaya hata huko kukosa wazazi au kuishi mazingira magumu watu wamekuwa wakifoji maana kuna watoto wa vigogo wenye uwezo mzuri tu na wanapata 80-100% ya mkopo!
Nadhani special scheme yenye public na private scholarships ianzishwe ili kuhamasisha afaulu kwa wedge zetu, serikali irejee kuangalia vipimo vya alama za ufaulu kama ndio kigezo namba moja katika kutoa mkopo kwa ajili ya elimu ya juu. Vyuo vya umma vipewe kipaumbele, kisha taasisi nyingine zenye rekodi nzuri kama tulivyoainisha hapo juu (no.2).
4. Uwepo wa mitihani inayofanana kwa taasisi za juu
mfumo wetu wa sasa wa elimu unaweza kutoa Digrii moja ya fani hiyo hiyo lakini tunaweza kuwapata wanataaluma waliopitia elimu tofauti. Misisitizo ya kufuata mtaala unaofanana nadhani hadi sasa haupo, jambo hili linapelekea kuporomoka kwa taaluma na udhaifu wa wanataaluma wetu hasa hawa wasomi wa sasa.
Jambo hili linawezekana kwa wale waliofanya CPA au mitihani mingine ya bodi wanaweza kuona jinsi gani mtihani wa aina moja unaweza kutungwa na kuwapata watu wenye taaluma katika ushindani linganifu. kama tunataka kuset standards then hiki ni kigezo kikubwa sana. Vinginevyo A ya UDOM inaweza kuwa tofauti na UDSM na ile Ya Kampala University kwa kozi hiyohiyo.
tumefikia sehemu tunapaswa kustandardize elimu yetu.
5. Kufutwa kwa taasisi zote zisizona sifa
Wizara ya elimu inapaswa kutazama upya leseni zake zote ilizozitoa kwa taasisi mbalimbali ili kuona kama wamefikia vigezo, na kwa wale wanaoshindwa hakuna tena nafasi ya kufikiriwa, wafutiwe usajili ili kupunguza huu ubabaishaji tunaouona sasa.

Wadau naomba mchangie sana uzi huu labda tunaweza kuwafikia wadau wakasikia mawazo yetu.
Pia kukosoana kunaweza kuwafanya wenye nafasi katika nchi wakapima mawazo yao.
 
Naona umeandika blah blah nyingi sana, lakini kuhusu Elimu watanzania wanataka elimu iwe BURE kuanzia Chekechea mpaka PHd, kusiwe na mchango wowote wa kulipia katika Elimu.
 
Hii ndo kuboresha elimu??? Duh! Sema asiwepo mwanafunzi wa kukosa shule kwa kukosa ada. Elimu iwe bure hadi form six. Huku vyuoni watu wapewe mikopo ili warudishe pesa wakipata kazi kusaidia wengine kusoma. Elimu bora ni gharama.
 
Naona umeandika blah blah nyingi sana, lakini kuhusu Elimu watanzania wanataka elimu iwe BURE kuanzia Chekechea mpaka PHd, kusiwe na mchango wowote wa kulipia katika Elimu.

Umeenda shule?
Unaona dhambi ku-invest katika elimu kweli?
Kweli tunahamasishana kuchangia harusi lakini sio elimu?
Tunaombwa kuchangia wagombea wa kisiasa na tunahamasika lakini tunashawishiana tusiwalipie watoto wetu gharama za elimu?
Anyway, Kwa bahai mbaya, mgombea wako wa sera ya elimu bure kura hazikutosha. Sasa si wakati wa kampeni, hapa ndio tunaishi na uhalisia ndio huo, unafikiri tutawezaje kuchangia vijana wetu waende shule.
kwa mfano mimi katika university niliyosoma kama alumni itaanzishwa na kuhamasisha utoaji scholarships kwa undergraduates, naahidi kuchangia katika mfuko huo, lakini hata kama mfuko huo hautokuwepo bado nitachangia uboreshwaji wa elimu katika maeneo mengine. Siamini katika kipato changu kutosha kuondoa kero ya aina yeyote either ktk ada au uboreshwaji wa majengo, vitendea kazi au posho za watoa elimu, lakini kwa wenye mishahara kama mimi tukichanga, tunaweza kufanya makubwa mno!
Yes, vijana wetu wanaweza kusoma bure hadi PhD, ila lazima kuwe na taasisi zinazofanikisha hayo! labda taasisi za umma au binafsi.
 
Wadau wakati umefika kwa wananchi kushiriki kwa vitendo katika kuleta tija kwa taifa letu. sehemu ya kwanza ni kutafuta mbinu za kutatua changamoto za kielimu.
Je wadau tunaweza kumshauri raisi wetu juu ya kuimarisha elimu na kuifanya elimu yenye tija kwa taifa?
Naomba michango yenu ktk uzi huu.
Kwa upande wangu nafikiri mambo haya yafuatayo yanaweza kutuletea tija.

Umaongelea kuboresha elimu wakati huwezi hata ku edit post yako isomeke vizuri.
 
Toka lini nyie mkashaurika?
Mh. James Mbatia alishatoa ushauri mzuri tu bungeni namna ya kuboresha elimu Tanzania. Yaliingilia kushoto yakatokea kulia.
 
kwanza kabla sijachangia nieke angalizo umesema tumshauri rais wetu.mimi kwangu huyo ni rais wenu mpaka kesho sitabadilii msimamo wangu.alafu kuhusu elimu kuboreshwa labda kwanza niseme mfumo wa elim tanzania kwa ujumla wake niwakuvunja hakuna cha kuboresha hapo.hatuna elim ya kumsaidia mwanafunzi kujitegemea sasa munasema muna elimu?mimi hata sijui mawaziri wa elim nch hii na maraisi wao vichwa vyao vinakuga viko na ulevi.masaa yote au vipi.maana kuna vitu vingine hata ukimpa uwaziri mtoto wa darasa la tatu ataviona kua nitatizo.nitaje viwilitu japo naviona vingi.mtoto unampeleka shule kuanzia la kwanza to std seven anasoma masomo.yote kiswahili kingereza nisomo moja kama somo lingine anafaulu unampeleka sekondar za lowasa kule kata miaka minne anakutana na kila somo nikingereza na muda huo akili yake ishakomaa unamuanzisha tena darasa la awali la masomo.ya kingereza.unategemea apate elimu bora kutoka wapi?pili munapozungumzia elim bure ni elimu ya aina gani?munatoa neno ada munaweka michango ya madawati majembe mafagio na nk ambayo inazidi laki na ushee wazazi wanayolipia bado mlinz chakula hapa numetoa elim bure vipi?au nielim bure jina
 
Walimu wapewe mshahara unaokidhi na posho pia zana na miundombinu rafiki ziwepo.
 
nasikia tuliomuelewa Pombe kwamba Elimu itakuwa bure mpaka sekondari tunaambiwa tulimnukuu vibaya
 
hata wino wa kura aujafutika vidoleni tunaambiwa kwamba tulimnukuu vibaya Pombe kwamba Elimu itakuwa bure
 
kuwepo na reshen ya laki na nusu ktkt ya mwezi kwa waalimu wote.kuhamasisha uwajibikaji zaidi.
 
Wadau wakati umefika kwa wananchi kushiriki kwa vitendo katika kuleta tija kwa taifa letu. sehemu ya kwanza ni kutafuta mbinu za kutatua changamoto za kielimu.
Je wadau tunaweza kumshauri raisi wetu juu ya kuimarisha elimu na kuifanya elimu yenye tija kwa taifa?
Naomba michango yenu ktk uzi huu.
Kwa upande wangu nafikiri mambo haya yafuatayo yanaweza kutuletea tija.
1. Wadau kupata nafasi zaidi ya kuchangia katika mbinu za uboreshwaji wa huduma hii muhimu katika jamii.
-vyuo vikuu na wasomi waongoze makongamano katika kutoa tafakari juu ya nini kifanyike katika kuleta na kuimarisha elimu yetu. si vema kuwa na mijadala isiyo na kikomo, lakini katika siku 100 za mwanzo wa awamu ya tano jambo hili lilitakiwa lipewe namba moja ili baada ya hapo tuanze kuonesha muelekeo mpya.
2. kuweka vigezo vya ubora, tuzo na adhabu kwa shule na taasisi zingine za elimu.
Kutengeneza vigezo kwa taasisi za kielimu ili tuwe na sifa zinazoendana katika mashule yote hapa nchini.
yes huwezi kosa uwepo wa shule zenye viwango vya juu, kati na chini lakini shule zipimwe kwa vigezo, daraja za ubora zibainishwe na taasisi husika iwe halmashauri au taasisi ya dini, shirika au mtu binafsi zipewe majukumu ya kufanyia uboreshwaji wa viwango katika vipindi maalum na kushindwa kufanya hivyo taasisi husika inyimwe haki ya kuendelea kutoa huduma na ifidie gharama za kuwahamisha wanafunzi na penalt ya usumbufu kwa taasisi. pale inapogusa halmashauri, basi na mkurugenzi wa halmashauri husika na maofisa wa elimu nao waondolewe katika nafasi zao kwa kushindwa kusimamia elimu.
Kwa vyuo vyote kuanzia vile vidogo vinavyotoa certificates pekee hadi universities, serikali isigharamie chochote ikiwemo kupeleka wanafunzi kama hawatofikia viwango ailivyowekwa.
-zawadi ikiwemo pamoja na pesa na medali kwa taasisi zitakazofanya vema pamoja na mkurugenzi na maofisa wa elimu.
3. Uwepo wa scholarships kwa wanafunzi wanaofanya vema.
kwa mpango uliopo sasa wa wanafunzi kusoma bure hadi A-level, wanafunzi wanapaswa kuwa na eneo jingine la kushindania inapokuja kumaliza elimu ya sekondari. Suala la bodi ya mikopo kutoa nafasi ya mikopo just kwa kufiwa na wazazi na kuwaacha watoto wengine wenye wazazi wa kipato cha kati lakini wenye ufaulu mzuri katika masomo yao ya sekondari kuishi kwa kutaabika wakiwa vyuo vikuu pia linapunguza ufanisi kwa wanataaluma wetu. Wale wenye umri wa kati watakumbuka kipindi kabla ya kluanza bodi ya mikopo, serikali ilikuwa inagharamia wanafunzi wote wenye alama za ufaulu wanapoingia vyuo vikuu. hapa ilikuwa ni kutokana na nafasi zinazopatikana UDSM, Mzumbe na Sokoine,. pamoja na vyuo vingine hasa vile vya ufundi kwa FTC. wote tulisoma na kupambana kupata nafasi hiyo, kwa hiyo ushindani na juhudi zilitumika kufikia malengo ya kuifikia nafasi hii hadhimu. mambo yamebadilika hasa baada ya kuanzishwa kwa bodi ambapo suala la kupata ni bahati nasibu tu, ufaulu sasa si kigezo, lakini vigezo vingine visivyo na tija ndio vimepewa kipaumbele zaidi, kwa bahati mbaya hata huko kukosa wazazi au kuishi mazingira magumu watu wamekuwa wakifoji maana kuna watoto wa vigogo wenye uwezo mzuri tu na wanapata 80-100% ya mkopo!
Nadhani special scheme yenye public na private scholarships ianzishwe ili kuhamasisha afaulu kwa wedge zetu, serikali irejee kuangalia vipimo vya alama za ufaulu kama ndio kigezo namba moja katika kutoa mkopo kwa ajili ya elimu ya juu. Vyuo vya umma vipewe kipaumbele, kisha taasisi nyingine zenye rekodi nzuri kama tulivyoainisha hapo juu (no.2).
4. Uwepo wa mitihani inayofanana kwa taasisi za juu
mfumo wetu wa sasa wa elimu unaweza kutoa Digrii moja ya fani hiyo hiyo lakini tunaweza kuwapata wanataaluma waliopitia elimu tofauti. Misisitizo ya kufuata mtaala unaofanana nadhani hadi sasa haupo, jambo hili linapelekea kuporomoka kwa taaluma na udhaifu wa wanataaluma wetu hasa hawa wasomi wa sasa.
Jambo hili linawezekana kwa wale waliofanya CPA au mitihani mingine ya bodi wanaweza kuona jinsi gani mtihani wa aina moja unaweza kutungwa na kuwapata watu wenye taaluma katika ushindani linganifu. kama tunataka kuset standards then hiki ni kigezo kikubwa sana. Vinginevyo A ya UDOM inaweza kuwa tofauti na UDSM na ile Ya Kampala University kwa kozi hiyohiyo.
tumefikia sehemu tunapaswa kustandardize elimu yetu.
5. Kufutwa kwa taasisi zote zisizona sifa
Wizara ya elimu inapaswa kutazama upya leseni zake zote ilizozitoa kwa taasisi mbalimbali ili kuona kama wamefikia vigezo, na kwa wale wanaoshindwa hakuna tena nafasi ya kufikiriwa, wafutiwe usajili ili kupunguza huu ubabaishaji tunaouona sasa.

Wadau naomba mchangie sana uzi huu labda tunaweza kuwafikia wadau wakasikia mawazo yetu.
Pia kukosoana kunaweza kuwafanya wenye nafasi katika nchi wakapima mawazo yao.

pongezi kwa hoja ya KIELIMU
MIMI nadhani tuungane na mheshimiwa kwa elimu bure mpaka kidato cha nne.

lakini ili elimu iwe bora inabidi mkakati madhubuti wa kupandisha jamasa ya walimu.molari ya walimu ipewe kipaumbele,ili walimu wajitume wai own kazi, hapo tutapata elimu bora.
 
Walimu wapewe Laptop kila mmoja, ikiwezekana wakuu wa shule wapewe mbilimbili.
 
Mtanzania wa leo amekata tamaa, mimi ni mwalimu ilakimsingi nakusihi mheshimiwa rais kwa namna yoyote ilebadili katiba kwanza. Elimu hii inayumba kwasababu walimu hatuthaminiwi na kama tunathaminiwa basi ni kidogo sana.

RUDISHA MOYO WA WALIMU KWA KUBORESHA STAHIKI ZAO.

Mimi naidai serikali mishahara ya miezi miwili tangu 2013, je hata kama ungekuwa wewe ungefanya kazi vizuri na mtu asiyekulipa haki zako?

TUNAVUMILIA TU!!!!
 
kwanza kabla sijachangia nieke angalizo umesema tumshauri rais wetu.mimi kwangu huyo ni rais wenu mpaka kesho sitabadilii msimamo wangu.alafu kuhusu elimu kuboreshwa labda kwanza niseme mfumo wa elim tanzania kwa ujumla wake niwakuvunja hakuna cha kuboresha hapo.hatuna elim ya kumsaidia mwanafunzi kujitegemea sasa munasema muna elimu?mimi hata sijui mawaziri wa elim nch hii na maraisi wao vichwa vyao vinakuga viko na ulevi.masaa yote au vipi.maana kuna vitu vingine hata ukimpa uwaziri mtoto wa darasa la tatu ataviona kua nitatizo.nitaje viwilitu japo naviona vingi.mtoto unampeleka shule kuanzia la kwanza to std seven anasoma masomo.yote kiswahili kingereza nisomo moja kama somo lingine anafaulu unampeleka sekondar za lowasa kule kata miaka minne anakutana na kila somo nikingereza na muda huo akili yake ishakomaa unamuanzisha tena darasa la awali la masomo.ya kingereza.unategemea apate elimu bora kutoka wapi?pili munapozungumzia elim bure ni elimu ya aina gani?munatoa neno ada munaweka michango ya madawati majembe mafagio na nk ambayo inazidi laki na ushee wazazi wanayolipia bado mlinz chakula hapa numetoa elim bure vipi?au nielim bure jina
Mshana na unaofanana nao mnasahau kuwa Tanzania ni kubwa kuliko ukawa!
Raisi aliyeko madarakani akishindwa kufanya anayoyadhamiria tunakwama wote!
Ni ubinafsi wa hali ya juu kufikiri kuwa raisi unayemtaka ni lazima achaguliwe, wewe kumbuka kura yako ni moja miongoni mwa kura mil 15, haiwezekani utashi wako ndio uwe sawa na kudharau matakwa ya wengine. Lakini katika demokrasia ya kweli vyama vyetu na uchaguzi ni just tools za kuleta maendeleo na ustawi wa Tanzania. Vyama na wagombea ni vyombo vya kutufikisha katika mafanikio, kama hatukupanda chombo ulichochagua haimaanishi kuwa tuendelee kusimama kwa miaka 5 kusubiri usafiri wako, nadhani inatakiwa ifike saa, busara zitumike na nyinyi chadema mnatakiwa kutumia akili zenu sasa.
unasema hatuna elimu ya kumsaidia mwanafunzi, na wewe utakuwa dent au mdogo wako au mwanao, unafikiri wakati utawekwa pause kumsubiri raisi wako, huyo kijana hakui?
Lakini bahati mbaya pia, hata 2010 mgombea mliyegoma kwa ajili yake saa ilipofika nyinyi wenyewe mlimkata! bado mliona maendeleo yanaweza kupatikana kupitia chombo kingine (UKAWA na Lowasa na sio chadema na Slaa), hivi ndivyo maendeleo yanavyotafutwa, huwa tuna preferences lakini machaguzi yetu sio absolute tunaruhusiwa kuwa wide options ikiwemo vyama mnavyopambana navyo!
Back to business, hoja yak ni ya msingi ya kupangua mfumo mzima wa elimu na kutazamwa upya!
nchi haisuswi mshana!
 
kosa kubwa walilofanya ni kushusha viwango vya ufaulu kwa o-level and Advance level na kuweka mfumo wa GPA km tulivokutia sisi chuo, kushusha viwango vya ufaulu hiyo mdo "worst blunder" iliyofanywa na shukuru kawambwa.
 
Wadau wakati umefika kwa wananchi kushiriki kwa vitendo katika kuleta tija kwa taifa letu. sehemu ya kwanza ni kutafuta mbinu za kutatua changamoto za kielimu.
Je wadau tunaweza kumshauri raisi wetu juu ya kuimarisha elimu na kuifanya elimu yenye tija kwa taifa?
Naomba michango yenu ktk uzi huu.
Kwa upande wangu nafikiri mambo haya yafuatayo yanaweza kutuletea tija.
1. Wadau kupata nafasi zaidi ya kuchangia katika mbinu za uboreshwaji wa huduma hii muhimu katika jamii.
-vyuo vikuu na wasomi waongoze makongamano katika kutoa tafakari juu ya nini kifanyike katika kuleta na kuimarisha elimu yetu. si vema kuwa na mijadala isiyo na kikomo, lakini katika siku 100 za mwanzo wa awamu ya tano jambo hili lilitakiwa lipewe namba moja ili baada ya hapo tuanze kuonesha muelekeo mpya.
2. kuweka vigezo vya ubora, tuzo na adhabu kwa shule na taasisi zingine za elimu.
Kutengeneza vigezo kwa taasisi za kielimu ili tuwe na sifa zinazoendana katika mashule yote hapa nchini.
yes huwezi kosa uwepo wa shule zenye viwango vya juu, kati na chini lakini shule zipimwe kwa vigezo, daraja za ubora zibainishwe na taasisi husika iwe halmashauri au taasisi ya dini, shirika au mtu binafsi zipewe majukumu ya kufanyia uboreshwaji wa viwango katika vipindi maalum na kushindwa kufanya hivyo taasisi husika inyimwe haki ya kuendelea kutoa huduma na ifidie gharama za kuwahamisha wanafunzi na penalt ya usumbufu kwa taasisi. pale inapogusa halmashauri, basi na mkurugenzi wa halmashauri husika na maofisa wa elimu nao waondolewe katika nafasi zao kwa kushindwa kusimamia elimu.
Kwa vyuo vyote kuanzia vile vidogo vinavyotoa certificates pekee hadi universities, serikali isigharamie chochote ikiwemo kupeleka wanafunzi kama hawatofikia viwango ailivyowekwa.
-zawadi ikiwemo pamoja na pesa na medali kwa taasisi zitakazofanya vema pamoja na mkurugenzi na maofisa wa elimu.
3. Uwepo wa scholarships kwa wanafunzi wanaofanya vema.
kwa mpango uliopo sasa wa wanafunzi kusoma bure hadi A-level, wanafunzi wanapaswa kuwa na eneo jingine la kushindania inapokuja kumaliza elimu ya sekondari. Suala la bodi ya mikopo kutoa nafasi ya mikopo just kwa kufiwa na wazazi na kuwaacha watoto wengine wenye wazazi wa kipato cha kati lakini wenye ufaulu mzuri katika masomo yao ya sekondari kuishi kwa kutaabika wakiwa vyuo vikuu pia linapunguza ufanisi kwa wanataaluma wetu. Wale wenye umri wa kati watakumbuka kipindi kabla ya kluanza bodi ya mikopo, serikali ilikuwa inagharamia wanafunzi wote wenye alama za ufaulu wanapoingia vyuo vikuu. hapa ilikuwa ni kutokana na nafasi zinazopatikana UDSM, Mzumbe na Sokoine,. pamoja na vyuo vingine hasa vile vya ufundi kwa FTC. wote tulisoma na kupambana kupata nafasi hiyo, kwa hiyo ushindani na juhudi zilitumika kufikia malengo ya kuifikia nafasi hii hadhimu. mambo yamebadilika hasa baada ya kuanzishwa kwa bodi ambapo suala la kupata ni bahati nasibu tu, ufaulu sasa si kigezo, lakini vigezo vingine visivyo na tija ndio vimepewa kipaumbele zaidi, kwa bahati mbaya hata huko kukosa wazazi au kuishi mazingira magumu watu wamekuwa wakifoji maana kuna watoto wa vigogo wenye uwezo mzuri tu na wanapata 80-100% ya mkopo!
Nadhani special scheme yenye public na private scholarships ianzishwe ili kuhamasisha afaulu kwa wedge zetu, serikali irejee kuangalia vipimo vya alama za ufaulu kama ndio kigezo namba moja katika kutoa mkopo kwa ajili ya elimu ya juu. Vyuo vya umma vipewe kipaumbele, kisha taasisi nyingine zenye rekodi nzuri kama tulivyoainisha hapo juu (no.2).
4. Uwepo wa mitihani inayofanana kwa taasisi za juu
mfumo wetu wa sasa wa elimu unaweza kutoa Digrii moja ya fani hiyo hiyo lakini tunaweza kuwapata wanataaluma waliopitia elimu tofauti. Misisitizo ya kufuata mtaala unaofanana nadhani hadi sasa haupo, jambo hili linapelekea kuporomoka kwa taaluma na udhaifu wa wanataaluma wetu hasa hawa wasomi wa sasa.
Jambo hili linawezekana kwa wale waliofanya CPA au mitihani mingine ya bodi wanaweza kuona jinsi gani mtihani wa aina moja unaweza kutungwa na kuwapata watu wenye taaluma katika ushindani linganifu. kama tunataka kuset standards then hiki ni kigezo kikubwa sana. Vinginevyo A ya UDOM inaweza kuwa tofauti na UDSM na ile Ya Kampala University kwa kozi hiyohiyo.
tumefikia sehemu tunapaswa kustandardize elimu yetu.
5. Kufutwa kwa taasisi zote zisizona sifa
Wizara ya elimu inapaswa kutazama upya leseni zake zote ilizozitoa kwa taasisi mbalimbali ili kuona kama wamefikia vigezo, na kwa wale wanaoshindwa hakuna tena nafasi ya kufikiriwa, wafutiwe usajili ili kupunguza huu ubabaishaji tunaouona sasa.

Wadau naomba mchangie sana uzi huu labda tunaweza kuwafikia wadau wakasikia mawazo yetu.
Pia kukosoana kunaweza kuwafanya wenye nafasi katika nchi wakapima mawazo yao.

BRN ifutwe maana ni Janga kwa taifa, mfumo wa zamani urudishwe.
 
maslahi ya walimu yaboreshwe. pia vifaa na majengo yaimarishwe. pia watoto wafaulu kihalali toka shule ya msingi kwenda sekondari.kusiwe na mtoto anayeingia form one hajui kusoma na kuandika...
 
Back
Top Bottom