kwani ilani yenu aliyojinadi nayo huyo rais wenu inasemaje kuhusu elimu?
mmeanza upuuzi wenu ambao ndiyo unadidimiza taifa hili. kama hamjui cha kufanya tuachieni nchi yetu.
Elimu ikiwa bure watoto wengi watapata bila vikwazo. Kuna watoto leo wanakaa nyumbani sababu ya kukosa michango ya shuleni. Acha watoto wengi wasome ubora ni changamoto inayohitaji mkakati wa kudumu.
Hao walimu nao wabadilike wamezidi kulialia utafikiri wao ndio wanapokea pesa ndogo wakati wana mishahara mikubwa tu siku hizi. Kazi wengi hawafanyi ni kuiba michango ya watoto wa maskini kila mwaka watu wanachangia madawati ila cha kushangaza kila siku hayatoshi na wanaaoondoka wanayaacha.
Hehehe wajaribu kufanya hivyo tuone.Ajira ya ualimu ifunguliwe, waajiri walimu kutoka nchi zote bila, working permit.
Walimu wa malawi,Kenya, Uganda , Zambia nk waje wapewe ajira ya ualimu . Walimu waende interview bila kujali anatoka nchi gani wakashindanishwe wapelekwe mashuleni wakafundishe.