Wadau wakati umefika kwa wananchi kushiriki kwa vitendo katika kuleta tija kwa taifa letu. sehemu ya kwanza ni kutafuta mbinu za kutatua changamoto za kielimu.
Je wadau tunaweza kumshauri raisi wetu juu ya kuimarisha elimu na kuifanya elimu yenye tija kwa taifa?
Naomba michango yenu ktk uzi huu.
Kwa upande wangu nafikiri mambo haya yafuatayo yanaweza kutuletea tija.
1. Wadau kupata nafasi zaidi ya kuchangia katika mbinu za uboreshwaji wa huduma hii muhimu katika jamii.
-vyuo vikuu na wasomi waongoze makongamano katika kutoa tafakari juu ya nini kifanyike katika kuleta na kuimarisha elimu yetu. si vema kuwa na mijadala isiyo na kikomo, lakini katika siku 100 za mwanzo wa awamu ya tano jambo hili lilitakiwa lipewe namba moja ili baada ya hapo tuanze kuonesha muelekeo mpya.
2. kuweka vigezo vya ubora, tuzo na adhabu kwa shule na taasisi zingine za elimu.
Kutengeneza vigezo kwa taasisi za kielimu ili tuwe na sifa zinazoendana katika mashule yote hapa nchini.
yes huwezi kosa uwepo wa shule zenye viwango vya juu, kati na chini lakini shule zipimwe kwa vigezo, daraja za ubora zibainishwe na taasisi husika iwe halmashauri au taasisi ya dini, shirika au mtu binafsi zipewe majukumu ya kufanyia uboreshwaji wa viwango katika vipindi maalum na kushindwa kufanya hivyo taasisi husika inyimwe haki ya kuendelea kutoa huduma na ifidie gharama za kuwahamisha wanafunzi na penalt ya usumbufu kwa taasisi. pale inapogusa halmashauri, basi na mkurugenzi wa halmashauri husika na maofisa wa elimu nao waondolewe katika nafasi zao kwa kushindwa kusimamia elimu.
Kwa vyuo vyote kuanzia vile vidogo vinavyotoa certificates pekee hadi universities, serikali isigharamie chochote ikiwemo kupeleka wanafunzi kama hawatofikia viwango ailivyowekwa.
-zawadi ikiwemo pamoja na pesa na medali kwa taasisi zitakazofanya vema pamoja na mkurugenzi na maofisa wa elimu.
3. Uwepo wa scholarships kwa wanafunzi wanaofanya vema.
kwa mpango uliopo sasa wa wanafunzi kusoma bure hadi A-level, wanafunzi wanapaswa kuwa na eneo jingine la kushindania inapokuja kumaliza elimu ya sekondari. Suala la bodi ya mikopo kutoa nafasi ya mikopo just kwa kufiwa na wazazi na kuwaacha watoto wengine wenye wazazi wa kipato cha kati lakini wenye ufaulu mzuri katika masomo yao ya sekondari kuishi kwa kutaabika wakiwa vyuo vikuu pia linapunguza ufanisi kwa wanataaluma wetu. Wale wenye umri wa kati watakumbuka kipindi kabla ya kluanza bodi ya mikopo, serikali ilikuwa inagharamia wanafunzi wote wenye alama za ufaulu wanapoingia vyuo vikuu. hapa ilikuwa ni kutokana na nafasi zinazopatikana UDSM, Mzumbe na Sokoine,. pamoja na vyuo vingine hasa vile vya ufundi kwa FTC. wote tulisoma na kupambana kupata nafasi hiyo, kwa hiyo ushindani na juhudi zilitumika kufikia malengo ya kuifikia nafasi hii hadhimu. mambo yamebadilika hasa baada ya kuanzishwa kwa bodi ambapo suala la kupata ni bahati nasibu tu, ufaulu sasa si kigezo, lakini vigezo vingine visivyo na tija ndio vimepewa kipaumbele zaidi, kwa bahati mbaya hata huko kukosa wazazi au kuishi mazingira magumu watu wamekuwa wakifoji maana kuna watoto wa vigogo wenye uwezo mzuri tu na wanapata 80-100% ya mkopo!
Nadhani special scheme yenye public na private scholarships ianzishwe ili kuhamasisha afaulu kwa wedge zetu, serikali irejee kuangalia vipimo vya alama za ufaulu kama ndio kigezo namba moja katika kutoa mkopo kwa ajili ya elimu ya juu. Vyuo vya umma vipewe kipaumbele, kisha taasisi nyingine zenye rekodi nzuri kama tulivyoainisha hapo juu (no.2).
4. Uwepo wa mitihani inayofanana kwa taasisi za juu
mfumo wetu wa sasa wa elimu unaweza kutoa Digrii moja ya fani hiyo hiyo lakini tunaweza kuwapata wanataaluma waliopitia elimu tofauti. Misisitizo ya kufuata mtaala unaofanana nadhani hadi sasa haupo, jambo hili linapelekea kuporomoka kwa taaluma na udhaifu wa wanataaluma wetu hasa hawa wasomi wa sasa.
Jambo hili linawezekana kwa wale waliofanya CPA au mitihani mingine ya bodi wanaweza kuona jinsi gani mtihani wa aina moja unaweza kutungwa na kuwapata watu wenye taaluma katika ushindani linganifu. kama tunataka kuset standards then hiki ni kigezo kikubwa sana. Vinginevyo A ya UDOM inaweza kuwa tofauti na UDSM na ile Ya Kampala University kwa kozi hiyohiyo.
tumefikia sehemu tunapaswa kustandardize elimu yetu.
5. Kufutwa kwa taasisi zote zisizona sifa
Wizara ya elimu inapaswa kutazama upya leseni zake zote ilizozitoa kwa taasisi mbalimbali ili kuona kama wamefikia vigezo, na kwa wale wanaoshindwa hakuna tena nafasi ya kufikiriwa, wafutiwe usajili ili kupunguza huu ubabaishaji tunaouona sasa.
Wadau naomba mchangie sana uzi huu labda tunaweza kuwafikia wadau wakasikia mawazo yetu.
Pia kukosoana kunaweza kuwafanya wenye nafasi katika nchi wakapima mawazo yao.