kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,298
- 12,599
Hakuna mtanzania mpenda haki anayetamani kuona katiba hiihii tuliyonayo inakutwa na kutumiwa na kiongozi anaefanana hata kwa nusu tu na yule kiongozi wa awamu ya tano (RIP).
Awamu ile ni sawa na kusema kuwa nchi ilikuwa imetekwa na watu kutoka sayari nyingine. Ni katiba ambayo kila mtu anasubiri busara za Rais tu baaasi. Ni awamu ambayo hata Mlandizi inaweza kuwa mkoa kamili.
Woga wetu sisi wengine unasababishwa na kile kilichotokea kwenye awamu ileee ya wanaharakati huru. Hatujaagana na nyonga, sisi tunapanga na Mungu anapanga, watanzania wote bila kujali itikadi ya vyama vyetu tunahitaji katiba mpya na safi mapema kabisa iwezekavyo, not later than 2025.