VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Awamu ya tano, awamu mpya
Yataka kuwa mfano, kuja na mapya
Ikakataza mikutano, hata kuruka na chopa
Awamu ya tano!
Ziara lukuki, majipu lundo
Ukaguzi wa bunduki, askari kupewa lindo
Ukaja uhakiki, kuondoa uvundo
Awamu ya tano!
Serikali tu, Bunge tupa kule
Kuamua tu, hakuna vya bure
Ni kazi tu, urahisi wa shule
Awamu ya tano!
Hajaribiwi kabisa, amewaambia
Mkitaka kumtikisa, atawaharibia
Hataki ya visa, kuwahudumia
Awamu ya tano!
Ahadi zaendelea, mikutano lukuki
Zinafanyika rejea, msiseme hatufiki
Itafuata kuamua, wapatikane mashabiki
Awamu ya tano!
PhD mtaji, pongezi muhimu
Utavishwa taji, na uanze kuhudumu
Ukinyimwa jiji, basi sehemu muhimu
Awamu ya tano!
Vyama baadaye, kazi kwanza
Viache vipotee, kanda ile ya Mwanza
Viwanda vitokee, tuwe wa kwanza
Awamu ya tano!
Sema kwa hatua, usisahau umakini
Kwakuwa huwezi kujua, waweza wekwa kapuni
Dodoma kuhamia, mpango mkakatini
Awamu ya tano!
Zika na njaa, marufuku
Hewa zajaa, maradufu
Uchumi wapaa,umaarufu
Awamu ya tano!
Sifia, utakumbukwa
Kimbia, usije kutwa
Nyatia, utabahatika
Awamu ya tano!
Haiwezekani, siasa muhimu
Hata Marekani, watu wanatuhumu
Hapa nyumbani, Rais aheshimu
Awamu ya tano!
Polisi, sasa TRA
Hawamisi, kuongeza bei
Promisi, everi dei
Awamu ya tano!
Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Yataka kuwa mfano, kuja na mapya
Ikakataza mikutano, hata kuruka na chopa
Awamu ya tano!
Ziara lukuki, majipu lundo
Ukaguzi wa bunduki, askari kupewa lindo
Ukaja uhakiki, kuondoa uvundo
Awamu ya tano!
Serikali tu, Bunge tupa kule
Kuamua tu, hakuna vya bure
Ni kazi tu, urahisi wa shule
Awamu ya tano!
Hajaribiwi kabisa, amewaambia
Mkitaka kumtikisa, atawaharibia
Hataki ya visa, kuwahudumia
Awamu ya tano!
Ahadi zaendelea, mikutano lukuki
Zinafanyika rejea, msiseme hatufiki
Itafuata kuamua, wapatikane mashabiki
Awamu ya tano!
PhD mtaji, pongezi muhimu
Utavishwa taji, na uanze kuhudumu
Ukinyimwa jiji, basi sehemu muhimu
Awamu ya tano!
Vyama baadaye, kazi kwanza
Viache vipotee, kanda ile ya Mwanza
Viwanda vitokee, tuwe wa kwanza
Awamu ya tano!
Sema kwa hatua, usisahau umakini
Kwakuwa huwezi kujua, waweza wekwa kapuni
Dodoma kuhamia, mpango mkakatini
Awamu ya tano!
Zika na njaa, marufuku
Hewa zajaa, maradufu
Uchumi wapaa,umaarufu
Awamu ya tano!
Sifia, utakumbukwa
Kimbia, usije kutwa
Nyatia, utabahatika
Awamu ya tano!
Haiwezekani, siasa muhimu
Hata Marekani, watu wanatuhumu
Hapa nyumbani, Rais aheshimu
Awamu ya tano!
Polisi, sasa TRA
Hawamisi, kuongeza bei
Promisi, everi dei
Awamu ya tano!
Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam