Serikali ya awamu ya tano na dhana ya disillusionment kwa Watanzania

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Katika somo la lugha ya kiingereza (English language) kuanzia kidato cha tatu Kuna somo la Kazi ya fasihi (work of arti) ambayo kwa lugha ya kiingereza huitwa Literature.

Kidato cha tatu Kuna kitabu cha fasihi cha tamthilia (play) kinachoitwa "THE BLACK HERMIT". Kitabu hiki kimeandikwa katika setting ya Nchini Uganda na kimeandikwa na mwandishi Ngugi wa Thiong'o.

Katika kitabu hicho, muhusika mkuu anaitwa Remi ambaye alikua ni msomi mzuri lakini alimbia kijiji Chake kutokana na mila na desturi mbaya ya kurithi wanawake wajane (inheritance of Windows)

Remi alimpenda Sana Mschana mrembo aliyeitwa Thoni lakini kwa kuwa alikua domo zege (muoga wa kutongoza) alikua anaumia moyoni tu hakumwambia Thoni kwamba anampenda. Kwa bahati Mbaya Kaka yake Remi yeye alikua na mdogo lojo lojo (jasiri wa kutongoza) akamtongoza Thoni na kumuoa. Suala Hilo lilimuumiza Sana Remi. Kaka yake Remi alipata ajali ya piki piki na kufariki

Remi alisisitizwa kumrithi Thoni na baba yake aliyeitwa Mzee Ngome kama mila zilivyotaka . Lakini Remi alikataa kata kata kumrithi Thoni mbele ya baba yake. Baba yake alikua mgonjwa kitandani na majibu ya Remi na stress za kupoteza kaka yake Remi, Mzee Ngome alifariki kwa msongo wa Mawazo.

Remi alipokwenda mjini alitumiwa barua na mama yake aliyeitwa Nyobi kwamba arudi kijijini kwa ajili ya kumrithi Thoni. Ingawa Remi alimpenda kabla ya kuolewa na kaka wa Remi lakini Remi hakua tayari.

Wakati Remi akiwa mjini, wanakijiji wa kijiji Chake walikua wanaoenewa na wakoloni kwa kuporwa ardhi, kuteswa, kufungwa na kuuawa na wakoloni. Wanakijiji wakafanya Mkutano wa hadhara na kujadili kwamba nani anaweza kuwakomboa wanakijiji kutoka katika mateso makubwa ya wakoloni??

Mkutano uliazimia kwamba Remi ndiye anafaa Sana kuwakomboa maana ni msomi na mwenye upeo mkubwa Sana wa mambo. Mkutano uliwateua wazee watatu (3 elders) waende mjini Ili wakamshawishi Remi arudi kijijini kuja kuwaondoa wakoloni Ili wananchi wapate ukombozi.

Wakati hayo yakifanyika, Nyobi mama yake Remi naye akamfuata mchungaji wa kanisa (Pastor) na kumueleza kwamba, anamuomba Pastor aende mjini kumshawishi Remi arudi kijijini Ili aje amrithi Thoni na kuwa mchungaji wa baadaye. Pastor akakubali kwamba Remi atakua future Pastor.

Hivyo Mgogoro wa kundi la wanakijiji wanaomtaka Remi kwa ajili ya ukombozi wa kijiji kutoka kwa wakoloni na upande wa Nyobi na Pastor wanamtaka Remi aje kumrithi Thoni na kuwa mchungaji.

Wazee watatu walifika mjini na kumshawishi Remi arudi kijijini. Remi alikataa. Wazee wakazingushia dawa kuzunguka nyumba ya Remi kwamba dawa hizo zitasaidia kumshawishi Remi kurudi kijijini kwa ajili ya ukombozi.

Baada ya Wazee watatu kugonga mwanba kumshawishi Remi kurudi kijijini, Pastor naye akafika mjini kumshawishi Remi kurudi kijijini kwa ajili ya Kumrithi Thoni na kuwa mchungaji wa baadaye. Remi alikubali kurudi kijijini.

Lakini kabla Remi hajarudi kijijini, Remi alimsimulia Rafiki yake Omange hali ya wananchi wa kijijini kwake jinsi wanavyoteseka na ukoloni pamoja na mila na desturi za hovyo hovyo za kurithi wajane. Omange alishangazwa na jamii hiyo ambayo ilikua inaishi maisha ya kale ya mila na desturi zilizopitwa na wakati. Omange Rafiki wa Remi aliomba aongozane na Remi kwenda kijijini kukomboa kijiji na kuondoa mila na desturi za kizamani. Remi alitoa taarifa ya kurudi kijijini.

Wanakijiji wakamsibiri kwa hamu kubwa kujua kwamba mkombozi wa kijiji anakuja leo. Thoni, Nyobi na Pastor nao wakafurahi kwamba Remi anakuja kumrithi Thoni na kuwa mchungaji. Hivyo furaha ikatamalaki. Wanakijiji wakamwita REMI kama MKOMBOZI WAO (THEIR SAVIOUR /THEIR REDEEMER). Waliamini kwamba kupitia Remi Mateso ya kupigwa, kuumizwa, kuporwa chakula na ardhi yatakwisha. Waliweka imani kubwa Sana kwa Remi. Walimuona kama ndio Silaha ya mwisho ya kuitumia dhidi ya utumwa na ukoloni.

Remi aliopofika kijijini alidhihirisha DHANA YA DISILLUSIONMENT yaani hali ya watu kuwa na matumani makubwa Sana chanya kwa mtu au taasisi lakini inajitokeza kinyume Chake, inakua ni kufedheheshwa na kujeruhiwa moyo. Kwa lugha nyingine ni kutarajia mema na kupata mabaya zaidi waingereza husema DISSAPPOINTMENT.

Remi aliapeleka DISILLUSIONMENT kijijini mana badala ya kuwasikiliza wananchi walichomuitia, alianza kuwashambulia kwa matusi na dhihaka. Alisema ninyi ni wapuuzi, mnaishi maisha ya kizamani na yaliyopitwa na wakati, ninyi hamfai kuvumiliwa. Aliwashambulia wanakijiji kwa kila neno la udhalilishaji, kejeli na maneno ya dhihaka na kiburi. Kila aliyeamini kwamba Remi ni mkombozi wa kijiji alipoteza imani, kila mmoja alipoteza matumani ya ukombozi Bali kupata Fedha na mateso yenye uchungu zaidi.

Remi hakuishia hapo, alimfuta Mchungaji na kumshambulia vikali. Akamwambia wachungaji gani wezi ninyi badala ya kufanya Kazi mnaendekeza mila za kizamani za kurithi wajane, kuibia watu sadaka bila kufanya Kazi. Remi akasema hawezi kufanya Kazi ya uchungaji wala Kazi za wizi kama uchungaji. Mchungaji alidhalilishwa kwa kiwango kikubwa. Disillusionment

Remi alimfuta mama yake mzazi Nyobi na kumtamkia maneno makali Sana dhidi ya lengo Lake la kutaka Remi amrithi Thoni kama mila zinavyosema. Remi alimdhalilisha mama yake kwamba ni dwarfed katika fikra na utashi(kilaza aliyedumaa fikra) Remi akamwambia mama yake hawezi kuwa mtumwa wa mila za kishenzi (hethen traditions) yeye kama msomi. Mama yake Remi akaumia Sana. Disillusionment...

Wakati huo huo, Remi alimfuta pia Thoni, nyumbani kwa akina Remi akiwepo mama yake Nyobi akamwambia Thoni kwamba siwezi kukurithi ingawa nilikupenda kabla ya kuolewa (I used to love you before you get married) lakini kwa sasa I'm not ready to be slave of outdated mila na desturi. You are not outdated and out fashioned.

Remi alisababisha kila mmoja katika kijiji kuguswa na maumivu makali ya udhalilishaji. Remi akatwaa Disillusionment kijiji kizima. Thoni alishindwa kuvumilia kabisa maumivu na matokeo ya Disillusionment ya Remi. Aliamua kukimbilia katika msitu na kujiua....

Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 nchini Tanzania kilimsimamisha mgombea wa urais John Pombe Magufuli na kumpachika majina ya "Muadilifu", "Mfuatiliaji "," mchapa Kazi " na kusindikizwa na kibwagizo cha kauli mbiu ya" HAPA KAZI TU "

Watanzania walirubunika na maelezo ya Kwamba John Pombe Magufuli ni Muadilifu, mchapa Kazi na Mfuatiliaji kwa kuhusiaanisha na utendaji wake uliopewa jina zuri la utendaji uliotukuka katika wizard ya Ujenzi....

Chama cha Mapinduzi na mgombea mwenyewe kilitoa ahadi lukuki kwa watanzania na kuwajaza imani na matumani hewa ambayo leo yanatafsiriwa kuwa ni DISILLUSIONMENT.... Magufuli akiwa mjini Musoma alitamka kwamba tarehe 26/10/2016 atamteua Waziri wa maji na atamtaka Waziri huyo kupeleka maji Musoma na akishindwa atamfanya Waziri yeye mwenyewe kuwa maji.. Kwa Watu wanaoshirikisha Halmashauri ya ubongo na manispaa ya akili walihoji atateuaje Waziri tarehe 26/10/2015 wakati matokeo yatakua bado kutangazwa?? Lakini mazuzu walishangilia na kufurahia ahadi hiyo hewa....

Mgombea huyo wa Urais aliwaahidi watanzania kwamba akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania suala la dawa katika Hospitali itakua ni lazima na endapo dawa hazitakuwepo atalala nao mbele japo hakusema atalala nao mbele akina nani.. Leo maelfu ya watanzania wanapoteza maisha kwa kukosa dawa huku Rais na serikali yake wakiwa bize kuhamia Dodoma, kujenga uwanja wa ndege Chato na kununua Bombardier...

Akiahidi kuhusu elimu ya Juu, Magufuli aliitangazia dunia Kwamba hakuna mtoto wa maskini wa taifa hili atakayekosa mkopo chuo kikuu. Alisema Tena pesa yenyewe ni mkopo kwa nini serikali isitoe. Bodi ya mikopo nitalala nao mbele kama hawatatoa mkopo....

Kwa mujibu wa bodi ya Mikopo Batch ya kwanza na ya pili, ni wanafunzi 7904 tu ndio wamepata mkopo huku maelfu ya wanafunzi wakikosa mkopo.. Mfano, Chuo kikuu cha Dar Es Salaam kimefanya udahili wa wanafunzi mwaka 2016/2017 idadi ya wanafunzi 8583 Sawa na 100% huku wanafunzi waliopata mkopo ni wanafunzi 3966 Sawa na 46% huku wanafunzi 4617 wamekosa mkopo Sawa na 54%.Hii ni zaidi ya nusu ya wanafunzi waliodahiliwa. Je hali ikoje katika vyuo vikuu vingine kama chuo kikuu cha Dar Es Salaam tu 54% ya wanafunzi ni NO LOAN??

Serikali inayoitwa ya AWAMU ya tano iliahidi kuboresha maisha ya watumishi wa umma hasa walimu na madaktari ambao maisha yao yako chini Sana ikiwepo jeshi la polisi na magereza. Rais Magufuli akawaita waliokua wanapata mishahara ya milioni 40 ambao aliwaita wanaishi kama malaika sasa watapata mshahara wa milioni 15 Ili waishi kama mashetani.

Kwa tafsiri ya kawaida, kama wanaoishi kwa milioni 15 kwa mwezi ni mashetani basi watumishi wa umma wanaopata mshahara wa chini ya hata laki tano hao watakua wanaishi kama misukule au mapepo hawajafikia hata hadhi ya kuishi kama mashetani. Badala ya serikali kuwapandisha hawa misukule(walimu, polisi, wauguzi, madaktari nk) waishi angalau kama mashetani kwa kupata angalau hata robo ya mashetani (robo you milioni 15) Serikali yake imekua ikiwatesa kwa kile kinachoitwa ukaguzi wa vyeti na uhakiki. Watumishi wanaoishi vijijini wanatumia Fedha zao nje ya bajeti ya familia zao kufika Halmashauri kwa uhakiki kila mara.

Watanzania waliopatwa na maafa yanayotokana na majanga ya asili (Natural Hazards/calamities/disasters) wanapuuzwa na serikali inayojinasibu ni ya watanzania maskini. Wananchi waliochangiwa Fedha na watu mbalimbali na taasisi mbalimbali baada ya kupata maafa ya mvua ya Mawe kule Mwakata na Kahama Fedha zao serikali ya Magufuli imebadilisha matumizi na kusema Fedha zikajenge Shule na hospitali na serikali ya AWAMU ya tano imejikita katika Ujenzi wa reli ya standard gauge haitajihusisha na kujengea wananchi nyumba.

Kwamba serikali haitajihusisha na madhara ya maafa. Kauli kama hiyo ilitolewa tena na Magufuli kwamba tetemeko la ardhi la Kagera halikuletwa na serikali ya Ccm hivyo serikali haitajihusisha na Ujenzi wa Nyumba za wananchi Bali itajikita kujenga taasisi za umma /serikali kama shule nk. Utajiuliza mabilioni ya Fedha yaliyopatikana kutoka mtaifa mbalimbali kama Uingereza (billion 6),India (Milioni 500) , nk pamoja na taasisi mbalimbali nchini na nje ya nchi zitafanya Kazi moja tu ya kujenga taasisi za umma???? Je serikali inayojiita serikali ya maskini imewasaidia maskini hapo au imewaumiza?????

Waziri wa Kilimo, mifugo na uvuvi akiwa Nane nane Jijini Mbeya tarehe 08/08/2016 aliitangazia Tanzania kwamba mwaka huu wa Fedha, serikali imetenga Fedha kidogo Sana za Ruzuku ya pembejeo kwa wakulima hivyo wakulima wajiandaye kujinunulia mbolea maana hakutakua na Mbolea ya Ruzuku ya kutosha. Hii ni ishara kwamba wakulima watapata pigo kubwa katika kilimo. Tusubiri...

NDANI ya utawala wa Serikali ya AWAMU ya tano chini ya Rais Muadilifu, msema kweli na mpenzi wa Mungu serikali imeshakopa Fedha zaidi ya trillion 2sawa na billion 2000 za kitanzania na den la taifa kufikia Trillion 51.2sawa na kila Mtanzania kudaiwa Shilingi Milioni 1. Hakuna tangible development projects ambazo serikali imeanza kuzifanya au kuzitekeleza mpaka kukopa Fedha hizo. Ndege zilizonunuliwa zilitengewa bajeti yake isiyozidi billion 800.

VIJANA waliohitimu vyuo vikuu, hasa taaluma ya ualimu na uuguzi pamoja na udaktari wameachwa mitaani kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa bila ajira. Serikali ilitangaza kuajiri mwezi Aprili kupitia Simbachawene na mwezi mei kupitia Suleman Jaffo na iliposhindikana Rais Magufuli Juni 2016 aliomba mwezi mmoja au miezi miwili ya uhakiki na baada ya hapo atatoa ajira. Miezi miwili iliisha Agosti 22, leo inaelekea mwezi wa nne kumalizika hakuna dalili ya ajira hizo wala watumishi waliopo katika ajira kupandishwa madaraja, mishahara kupanda na kulipwa malimbikizo.

Serikali inayoelezwa ina uwazi na Uadilifu imepiga Marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya Upinzani, imezima bunge na kulifanya kuwa kibogoyo, imedhibiti vyombo vya habari, imedhibiti wanaharakati na Wasomi. Wote hao wanalazimishwa kuimba wimbo wa kusifu na kuabudu serikali ya JPM

Mpaka kufikia Oktoba 2016 karibu kila kundi la Mtanzania limeisoma namba tena kwa taabu tupu.
 
Too much of any thing is toxic, you have good idea but you used too much words unnecessarily
 
Katika somo la lugha ya kiingereza (English language) kuanzia kidato cha tatu Kuna somo la Kazi ya fasihi (work of arti) ambayo kwa lugha ya kiingereza huitwa Literature.

Kidato cha tatu Kuna kitabu cha fasihi cha tamthilia (play) kinachoitwa "THE BLACK HERMIT". Kitabu hiki kimeandikwa katika setting ya Nchini Uganda na kimeandikwa na mwandishi Ngugi wa Thiong'o.

Katika kitabu hicho, muhusika mkuu anaitwa Remi ambaye alikua ni msomi mzuri lakini alimbia kijiji Chake kutokana na mila na desturi mbaya ya kurithi wanawake wajane (inheritance of Windows)

Remi alimpenda Sana Mschana mrembo aliyeitwa Thoni lakini kwa kuwa alikua domo zege (muoga wa kutongoza) alikua anaumia moyoni tu hakumwambia Thoni kwamba anampenda. Kwa bahati Mbaya Kaka yake Remi yeye alikua na mdogo lojo lojo (jasiri wa kutongoza) akamtongoza Thoni na kumuoa. Suala Hilo lilimuumiza Sana Remi. Kaka yake Remi alipata ajali ya piki piki na kufariki

Remi alisisitizwa kumrithi Thoni na baba yake aliyeitwa Mzee Ngome kama mila zilivyotaka . Lakini Remi alikataa kata kata kumrithi Thoni mbele ya baba yake. Baba yake alikua mgonjwa kitandani na majibu ya Remi na stress za kupoteza kaka yake Remi, Mzee Ngome alifariki kwa msongo wa Mawazo.

Remi alipokwenda mjini alitumiwa barua na mama yake aliyeitwa Nyobi kwamba arudi kijijini kwa ajili ya kumrithi Thoni. Ingawa Remi alimpenda kabla ya kuolewa na kaka wa Remi lakini Remi hakua tayari.

Wakati Remi akiwa mjini, wanakijiji wa kijiji Chake walikua wanaoenewa na wakoloni kwa kuporwa ardhi, kuteswa, kufungwa na kuuawa na wakoloni. Wanakijiji wakafanya Mkutano wa hadhara na kujadili kwamba nani anaweza kuwakomboa wanakijiji kutoka katika mateso makubwa ya wakoloni?? Mkutano uliazimia kwamba Remi ndiye anafaa Sana kuwakomboa maana ni msomi na mwenye upeo mkubwa Sana wa mambo. Mkutano uliwateua wazee watatu (3 elders) waende mjini Ili wakamshawishi Remi arudi kijijini kuja kuwaondoa wakoloni Ili wananchi wapate ukombozi.

Wakati hayo yakifanyika, Nyobi mama yake Remi naye akamfuata mchungaji wa kanisa (Pastor) na kumueleza kwamba, anamuomba Pastor aende mjini kumshawishi Remi arudi kijijini Ili aje amrithi Thoni na kuwa mchungaji wa baadaye. Pastor akakubali kwamba Remi atakua future Pastor.

Hivyo Mgogoro wa kundi la wanakijiji wanaomtaka Remi kwa ajili ya ukombozi wa kijiji kutoka kwa wakoloni na upande wa Nyobi na Pastor wanamtaka Remi aje kumrithi Thoni na kuwa mchungaji.

Wazee watatu walifika mjini na kumshawishi Remi arudi kijijini. Remi alikataa. Wazee wakazingushia dawa kuzunguka nyumba ya Remi kwamba dawa hizo zitasaidia kumshawishi Remi kurudi kijijini kwa ajili ya ukombozi.

Baada ya Wazee watatu kugonga mwanba kumshawishi Remi kurudi kijijini, Pastor naye akafika mjini kumshawishi Remi kurudi kijijini kwa ajili ya Kumrithi Thoni na kuwa mchungaji wa baadaye. Remi alikubali kurudi kijijini.

Lakini kabla Remi hajarudi kijijini, Remi alimsimulia Rafiki yake Omange hali ya wananchi wa kijijini kwake jinsi wanavyoteseka na ukoloni pamoja na mila na desturi za hovyo hovyo za kurithi wajane. Omange alishangazwa na jamii hiyo ambayo ilikua inaishi maisha ya kale ya mila na desturi zilizopitwa na wakati. Omange Rafiki wa Remi aliomba aongozane na Remi kwenda kijijini kukomboa kijiji na kuondoa mila na desturi za kizamani. Remi alitoa taarifa ya kurudi kijijini.

Wanakijiji wakamsibiri kwa hamu kubwa kujua kwamba mkombozi wa kijiji anakuja leo. Thoni, Nyobi na Pastor nao wakafurahi kwamba Remi anakuja kumrithi Thoni na kuwa mchungaji. Hivyo furaha ikatamalaki. Wanakijiji wakamwita REMI kama MKOMBOZI WAO (THEIR SAVIOUR /THEIR REDEEMER). Waliamini kwamba kupitia Remi Mateso ya kupigwa, kuumizwa, kuporwa chakula na ardhi yatakwisha. Waliweka imani kubwa Sana kwa Remi. Walimuona kama ndio Silaha ya mwisho ya kuitumia dhidi ya utumwa na ukoloni.

Remi aliopofika kijijini alidhihirisha DHANA YA DISILLUSIONMENT yaani hali ya watu kuwa na matumani makubwa Sana chanya kwa mtu au taasisi lakini inajitokeza kinyume Chake, inakua ni kufedheheshwa na kujeruhiwa moyo. Kwa lugha nyingine ni kutarajia mema na kupata mabaya zaidi waingereza husema DISSAPPOINTMENT.

Remi aliapeleka DISILLUSIONMENT kijijini mana badala ya kuwasikiliza wananchi walichomuitia, alianza kuwashambulia kwa matusi na dhihaka. Alisema ninyi ni wapuuzi, mnaishi maisha ya kizamani na yaliyopitwa na wakati, ninyi hamfai kuvumiliwa. Aliwashambulia wanakijiji kwa kila neno la udhalilishaji, kejeli na maneno ya dhihaka na kiburi. Kila aliyeamini kwamba Remi ni mkombozi wa kijiji alipoteza imani, kila mmoja alipoteza matumani ya ukombozi Bali kupata Fedha na mateso yenye uchungu zaidi.

Remi hakuishia hapo, alimfuta Mchungaji na kumshambulia vikali. Akamwambia wachungaji gani wezi ninyi badala ya kufanya Kazi mnaendekeza mila za kizamani za kurithi wajane, kuibia watu sadaka bila kufanya Kazi. Remi akasema hawezi kufanya Kazi ya uchungaji wala Kazi za wizi kama uchungaji. Mchungaji alidhalilishwa kwa kiwango kikubwa. Disillusionment

Remi alimfuta mama yake mzazi Nyobi na kumtamkia maneno makali Sana dhidi ya lengo Lake la kutaka Remi amrithi Thoni kama mila zinavyosema. Remi alimdhalilisha mama yake kwamba ni dwarfed katika fikra na utashi(****** aliyedumaa fikra) Remi akamwambia mama yake hawezi kuwa mtumwa wa mila za kishenzi (hethen traditions) yeye kama msomi. Mama yake Remi akaumia Sana. Disillusionment...

Wakati huo huo, Remi alimfuta pia Thoni, nyumbani kwa akina Remi akiwepo mama yake Nyobi akamwambia Thoni kwamba siwezi kukurithi ingawa nilikupenda kabla ya kuolewa (I used to love you before you get married) lakini kwa sasa I'm not ready to be slave of outdated mila na desturi. You are not outdated and out fashioned.

Remi alisababisha kila mmoja katika kijiji kuguswa na maumivu makali ya udhalilishaji. Remi akatwaa Disillusionment kijiji kizima. Thoni alishindwa kuvumilia kabisa maumivu na matokeo ya Disillusionment ya Remi. Aliamua kukimbilia katika msitu na kujiua....

Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 nchini Tanzania kilimsimamisha mgombea wa urais John Pombe Magufuli na kumpachika majina ya "Muadilifu", "Mfuatiliaji "," mchapa Kazi " na kusindikizwa na kibwagizo cha kauli mbiu ya" HAPA KAZI TU "

Watanzania walirubunika na maelezo ya Kwamba John Pombe Magufuli ni Muadilifu, mchapa Kazi na Mfuatiliaji kwa kuhusiaanisha na utendaji wake uliopewa jina zuri la utendaji uliotukuka katika wizard ya Ujenzi....

Chama cha Mapinduzi na mgombea mwenyewe kilitoa ahadi lukuki kwa watanzania na kuwajaza imani na matumani hewa ambayo leo yanatafsiriwa kuwa ni DISILLUSIONMENT.... Magufuli akiwa mjini Musoma alitamka kwamba tarehe 26/10/2016 atamteua Waziri wa maji na atamtaka Waziri huyo kupeleka maji Musoma na akishindwa atamfanya Waziri yeye mwenyewe kuwa maji.. Kwa Watu wanaoshirikisha Halmashauri ya ubongo na manispaa ya akili walihoji atateuaje Waziri tarehe 26/10/2015 wakati matokeo yatakua bado kutangazwa?? Lakini mazuzu walishangilia na kufurahia ahadi hiyo hewa....

Mgombea huyo wa Urais aliwaahidi watanzania kwamba akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania suala la dawa katika Hospitali itakua ni lazima na endapo dawa hazitakuwepo atalala nao mbele japo hakusema atalala nao mbele akina nani.. Leo maelfu ya watanzania wanapoteza maisha kwa kukosa dawa huku Rais na serikali yake wakiwa bize kuhamia Dodoma, kujenga uwanja wa ndege Chato na kununua Bombardier...

Akiahidi kuhusu elimu ya Juu, Magufuli aliitangazia dunia Kwamba hakuna mtoto wa maskini wa taifa hili atakayekosa mkopo chuo kikuu. Alisema Tena pesa yenyewe ni mkopo kwa nini serikali isitoe. Bodi ya mikopo nitalala nao mbele kama hawatatoa mkopo.... Kwa mujibu wa bodi ya Mikopo Batch ya kwanza na ya pili, ni wanafunzi 7904 tu ndio wamepata mkopo huku maelfu ya wanafunzi wakikosa mkopo.. Mfano, Chuo kikuu cha Dar Es Salaam kimefanya udahili wa wanafunzi mwaka 2016/2017 idadi ya wanafunzi 8583 Sawa na 100% huku wanafunzi waliopata mkopo ni wanafunzi 3966 Sawa na 46% huku wanafunzi 4617 wamekosa mkopo Sawa na 54%.Hii ni zaidi ya nusu ya wanafunzi waliodahiliwa. Je hali ikoje katika vyuo vikuu vingine kama chuo kikuu cha Dar Es Salaam tu 54% ya wanafunzi ni NO LOAN??

Serikali inayoitwa ya AWAMU ya tano iliahidi kuboresha maisha ya watumishi wa umma hasa walimu na madaktari ambao maisha yao yako chini Sana ikiwepo jeshi la polisi na magereza. Rais Magufuli akawaita waliokua wanapata mishahara ya milioni 40 ambao aliwaita wanaishi kama malaika sasa watapata mshahara wa milioni 15 Ili waishi kama mashetani. Kwa tafsiri ya kawaida, kama wanaoishi kwa milioni 15 kwa mwezi ni mashetani basi watumishi wa umma wanaopata mshahara wa chini ya hata laki tano hao watakua wanaishi kama misukule au mapepo hawajafikia hata hadhi ya kuishi kama mashetani. Badala ya serikali kuwapandisha hawa misukule(walimu, polisi, wauguzi, madaktari nk) waishi angalau kama mashetani kwa kupata angalau hata robo ya mashetani (robo you milioni 15) Serikali yake imekua ikiwatesa kwa kile kinachoitwa ukaguzi wa vyeti na uhakiki. Watumishi wanaoishi vijijini wanatumia Fedha zao nje ya bajeti ya familia zao kufika Halmashauri kwa uhakiki kila mara.

Watanzania waliopatwa na maafa yanayotokana na majanga ya asili (Natural Hazards/calamities/disasters) wanapuuzwa na serikali inayojinasibu ni ya watanzania maskini. Wananchi waliochangiwa Fedha na watu mbalimbali na taasisi mbalimbali baada ya kupata maafa ya mvua ya Mawe kule Mwakata na Kahama Fedha zao serikali ya Magufuli imebadilisha matumizi na kusema Fedha zikajenge Shule na hospitali na serikali ya AWAMU ya tano imejikita katika Ujenzi wa reli ya standard gauge haitajihusisha na kujengea wananchi nyumba. Kwamba serikali haitajihusisha na madhara ya maafa. Kauli kama hiyo ilitolewa tena na Magufuli kwamba tetemeko la ardhi la Kagera halikuletwa na serikali ya Ccm hivyo serikali haitajihusisha na Ujenzi wa Nyumba za wananchi Bali itajikita kujenga taasisi za umma /serikali kama shule nk. Utajiuliza mabilioni ya Fedha yaliyopatikana kutoka mtaifa mbalimbali kama Uingereza (billion 6),India (Milioni 500) , nk pamoja na taasisi mbalimbali nchini na nje ya nchi zitafanya Kazi moja tu ya kujenga taasisi za umma???? Je serikali inayojiita serikali ya maskini imewasaidia maskini hapo au imewaumiza?????

Waziri wa Kilimo, mifugo na uvuvi akiwa Nane nane Jijini Mbeya tarehe 08/08/2016 aliitangazia Tanzania kwamba mwaka huu wa Fedha, serikali imetenga Fedha kidogo Sana za Ruzuku ya pembejeo kwa wakulima hivyo wakulima wajiandaye kujinunulia mbolea maana hakutakua na Mbolea ya Ruzuku ya kutosha. Hii ni ishara kwamba wakulima watapata pigo kubwa katika kilimo. Tusubiri...

NDANI ya utawala wa Serikali ya AWAMU ya tano chini ya Rais Muadilifu, msema kweli na mpenzi wa Mungu serikali imeshakopa Fedha zaidi ya trillion 2sawa na billion 2000 za kitanzania na den la taifa kufikia Trillion 51.2sawa na kila Mtanzania kudaiwa Shilingi Milioni 1. Hakuna tangible development projects ambazo serikali imeanza kuzifanya au kuzitekeleza mpaka kukopa Fedha hizo. Ndege zilizonunuliwa zilitengewa bajeti yake isiyozidi billion 800.

VIJANA waliohitimu vyuo vikuu, hasa taaluma ya ualimu na uuguzi pamoja na udaktari wameachwa mitaani kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa bila ajira. Serikali ilitangaza kuajiri mwezi Aprili kupitia Simbachawene na mwezi mei kupitia Suleman Jaffo na iliposhindikana Rais Magufuli Juni 2016 aliomba mwezi mmoja au miezi miwili ya uhakiki na baada ya hapo atatoa ajira. Miezi miwili iliisha Agosti 22, leo inaelekea mwezi wa nne kumalizika hakuna dalili ya ajira hizo wala watumishi waliopo katika ajira kupandishwa madaraja, mishahara kupanda na kulipwa malimbikizo.

Serikali inayoelezwa ina uwazi na Uadilifu imepiga Marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya Upinzani, imezima bunge na kulifanya kuwa kibogoyo, imedhibiti vyombo vya habari, imedhibiti wanaharakati na Wasomi. Wote hao wanalazimishwa kuimba wimbo wa kusifu na kuabudu serikali ya JPM

Mpaka kufikia Oktoba 2016 karibu kila kundi la Mtanzania limeisoma namba tena kwa taabu tupu.
Duuh naona umahiri wako katika uandishi.
 
ccm wanachezea watanzania mchezo haramu wa karata tatu,kila watanzania wakiweka hela(kura)wanaliwa.

katika mchezo huu haramia anayechezesha huahidi hata laki kama.utafanikiwa kushinda kwa kuweka kwenye karata sahihi,mchezaji(mwananchi)anaweka.laki(kura)ili ashinde laki mbili(maendeleo),akiweka analiwa

anapewa matumaini kwamba sasa kakaribia kushinda,acheze tena(awapigie kura ccm)....inakuwa.ni endless mpaka leo.
 
Haya ukimaliza kukosoa na kulalamika, shauri nini kifanyike:
-uje na namba hasa za waomba mikopo na fedha zinazohitajika, uonyeshe pia zitatoka wapi.
-uzungumzie uhakiki na pesa za nauli za hao zitatoka wapi.
- hiyo ruzuku pia iainishe kwa takwimu.
 
Too much of any thing is toxic, you have good idea but you used too much words unnecessarily
Huu ndio ukweli wenyewe.

Na aghalabu ukweli utabaki kuwa ukweli, mpaka uje wakati mkweli, utakaoutambua ukweli huu!!
 
Haya ukimaliza kukosoa na kulalamika, shauri nini kifanyike:
-uje na namba hasa za waomba mikopo na fedha zinazohitajika, uonyeshe pia zitatoka wapi.
-uzungumzie uhakiki na pesa za nauli za hao zitatoka wapi.
- hiyo ruzuku pia iainishe kwa takwimu.
wewe umeshindwa unataka kutafuniwa tu? mwishowe,mwishowe utatafuniwa mamsap
 
nimeupenda huu mfano japokuwa huko tofauti kidogo ya yale ninayowaambieni kila siku kwamba,miaka hii mitano itakuwa ya kusikia na kuona mambo mengi ya ajabu hasa kutoka kwa watu tuliokuwa tunawategemea kutuletea maendeleo
 
Asante sana mkuu
 
miaka 10 itapita holaa tutazidi kuongezwa wagonjwa wa akili maana wtu wanategemea kutoka awamu hii watajikuta katiikati ya wimbi zito sana
 
Back
Top Bottom