awali ni awali

sugi

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
1,392
293
daah,namkumbuka mwalimu wangu wa darasa la kwanza,aliyenifundisha kusoma na kuandika,ni wa kike anaitwa mwaluko,alikuwa mkali sana,alikuwa anatunasa vibao,na kutupiga na rula nyuma ya vidole,aliwahi kukusanya vifutio vyetu vyoote na kuvitupilia mbali,kisa tunachafua madaftari kwa kufuta hovyo!je unamkumbuka mwalimu wako wa darasa la kwanza na vituko vyake?
 
Nakumbuka sana japo zaidi ya miaka ishirini imepita. Alikuwa anatupatia madaftari madogo yaliyogawanywa nusu. Mi nakumbuka nilikuwa nachezea kichapo kwa sababu nikiandika herufi 'a' tu inamaliza ukurasa mzima.
 
Namkumbuka mwl wangu Turufaina hapo ni Korongoni Primary Moshi,mwl huyu alikuwa mnene sana hivo anafundisha akiwa amekaa hivo walioanza jua kusoma ni wale siti za mbele,waoga tulilundikana back bencha na kusoma kulitupita pembeni
 
dah! 1991 mwalimu aliitwa mrs Njiro alikuwa mwembambamba huyo! afu akawa mjamzito sasa, tumbo likawa kubwa na wembamba wake ule ilikuwa balaa, ila alikuwa anapenda sana watoto so tulikuwa tunachwza naye kabisa kwenye vumbi na ndio hapo*2 anakufundisha kusoma na kuandika, so tulikuwa tunacatch fasta sana, muda wa darasani ulikuwa mcahache sana muda mwingi nje.
 
she was a good teacher,ila kwa wakati huo,ulijua tumbo limefanyaje?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom