Aveva, uliahidi mechi tatu pointi tatu

Aveva, uliahidi mechi tatu pointi tatu

Mwanza Kocha msaidizi wa Stand United, Athumani Bilali ametoboa siri kuwa mfumo wa 4-3-2-1 walioutumia ndio uliofanya Simba washindwe kuondoka na pointi tatu kwenye mechi yao ya Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.

Timu hizo mbili zilitoka sare ya 1-1 kwenye mchezo huo na bao la Simba likipachikwa na Shabani Kisiga wakati bao la Stand United likiwekwa kimiani na mshambuliaji wake, Kheri Mohamed.

Akizungumza na gazeti hili, Bilali alisema kuwa Simba hawakuwashinda kwa kuwa mfumo waliotumia Stand United wa 4-3-2-1, ambao unatumia mabeki wanne, viungo watano, uliwanyima nafasi.

Alisema katika mchezo huo walicheza kwa kupaki basi zaidi na wakitumia mashambulizi ya kushtukiza jambo lililofanya waweze kupata bao la kusawazisha.

"Huu mfumo tunautumia kwenye mechi ngumu, tunakuwa na wachezaji saba wanaokaba sana na tunashambulia kwa kushtukiza, hivyo ndivyo tulivyofanya katika mechi dhidi ya Simba na wakati mwingine tulitumia mfumo wa total football na ndiyo maana uliona hata hao akina Emmanuel Okwi walishindwa kufurukuta uwanjani," alisema Bilali.

Kocha huyo, ambaye ana rekodi ya kutofungwa na Simba kwa timu alizokuwa akifundisha kwenye Ligi Kuu katika miaka yake yote ya kufundisha klabu, alisema mfumo huo wa kukaba zaidi ndiyo uliowamiza wekundu hao.

"Nilijua Simba hawanifungi, sijawahi kupoteza mechi na hao jamaa nikiwa kama kocha, nilikuwa na Toto African kwenye Ligi Kuu niliwafunga mechi zote," alisema kocha Bilali.

Big Up Bilal; asante kwa kuendelea kutuletea raha tangu enzi za Toto Africans ya Mwanza hadi sasa ukiwa na Stand United (Banyawima) ya Shinyanga.
 
Wambura na waliotimuliwa Simba ndo wanaimaliza Simba.

Wanaimaliz kivipi mkuu...?hebu elezea profesionally? Tusipende kutafuta visingizio bila sababu.

Mimi ni simba na hua sikosi mechi uwanjani kama nipo dar.

Tuna tatizo kwenye ulinzi...beki yetu haiko imara...Ni rahisi kufungika.....Tuombe Mungu mzunguko wa kwanza tusifungwe sana...ili wa pili tumrudishe Musoti tuliyempeleka kwa mkopo na tumwache kwizera....

So far Okwi is doing an excellent job...mogoli yote hadi sasa tangu ligi ianze amesababisha yeye
 
mh rais; biashara asubuhi kama azam na mtibwa wafanyavyo, kwa mwendo huu ubingwa tutausikia tu aveva, hebu tazama hii mh rais na ujue tunavyoumia, nasikitika kwamba wapenzi wa simba hukata tamaa mapema hivyo usishangae kuona mapato yakipungua pia.............View attachment 189215

haya matusi mengine mnatukana babazenu jamani embu wasameheni yameshawakuta waangalie mbele
 
NDANI YA UWANJA IKO HIVI

SIMBA ILISAJILI WACEHZAJI WENGI IKIAMINI WANGEKUWA TEGEMEO SANA


  1. Cassilas awe mbadala wa Ivo lakn bado anatetemekaa sana LANGONI
  2. Banda aliyesajiliwa kwa makeke bado hajawa msaada Simba na sasa anatupwa jukwaani
  3. Mgeveke ukubwa wa mwili tu hana msaada Simba na anatoa maboko
  4. Kwizera (hakabi) ni heri ya Mkude na kiujumla mpira wao unafanana sana kwa kutoa pasi za mguso zaidi badala ya kupiga miezi (high balls) kama alivyokuwa Mafisango akimchezesha Okwi (shame kwa professional kukaa benchi)
  5. Maguli ni maguvu zaidi si akili sehemu za kutoa pasi anapiga mashuti sehemu za mashuti anatoa pasi
  6. Kiongera kama alivyokua Echesa ni pancha mwanzo mwisho japo ametupia mbili kirafiki
  7. Kisiga asiyetegemewa ndilo limekua jiwe kuu la pembeni

Simba ina tatizo kubwa kwenye beki na kiungo


  1. viungo wa chini wote wanacheza mpira unaofanana na kisiga hachezi kwa spidi ya akina Okwi na Tambwe na si mtu wa kumaliza tisini
  2. Kiungo wa pmbeni singano kwisnney hasaidii timu anacheza na jukwa kama alivyo Uhuru na Chanonngo

  1. Owino naye ni tatizo kwani pancha inamfanya awe mwoga kuchapa mafowadi wasumbufu na kufika kwa nguvu miguuni
  2. Isihaka anacheza beki kama midifield hana hasira/upako wa kuchapa na hana nguvu (stamina)

wacheni imani za uchawi hazisaidii karne hii
Jirani, mbona wakati wa usajili ulijisifu sana kuwa umefanya usajili wa kimataifa??????
 
namuona alipita karibu na jengo la yanga nini labda bado hajaanza ligi
we mansoor wa wapi wewe si kilajengo la njano la yanga we huoni hilo jengo jipya na la kisasa utalinganisha na gofu la kaole
 
Wanaimaliz kivipi mkuu...?hebu elezea profesionally? Tusipende kutafuta visingizio bila sababu.

Mimi ni simba na hua sikosi mechi uwanjani kama nipo dar.

Tuna tatizo kwenye ulinzi...beki yetu haiko imara...Ni rahisi kufungika.....Tuombe Mungu mzunguko wa kwanza tusifungwe sana...ili wa pili tumrudishe Musoti tuliyempeleka kwa mkopo na tumwache kwizera....

So far Okwi is doing an excellent job...mogoli yote hadi sasa tangu ligi ianze amesababisha yeye
mkuu hivi musoti mmempeleka kwa mkopo timu gani kweli? au unayemwongelea c yule anayewadai baada ya kukiuka mkataba?
 
mkuu hivi musoti mmempeleka kwa mkopo timu gani kweli? au unayemwongelea c yule anayewadai baada ya kukiuka mkataba?

Musoti yuko kwa mkopo zanzibar.....hayo ya kudai ni magazeti sio musoti
 
mkuu hivi musoti mmempeleka kwa mkopo timu gani kweli? au unayemwongelea c yule anayewadai baada ya kukiuka mkataba?
Musoti alisumbua sana akitaka aende Qatar hata wewe ungemafanya kafara tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom