Avast 5.0 v/s avg 9.0 - unachagua nini


Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Messages
4,235
Likes
52
Points
0
Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined Nov 2, 2006
4,235 52 0
Avast 5.0 V/S AVG 9.0

Sahau kuhusu Autorun ambayo ilikuwa inasumbua watu wengi sana mpaka kufikia hatua ya kuogopa kutumia bidhaa hii ukijumlisha muonekano mpya na wakipekee kabisa hiyo ni Avast Antivirus 5.0 ,ambayo ina Toleo la bure unayoweza kudownload kutoka kwenye tovuti yao www.avast.com pia ina toleo la kununua leseni ambalo pia unaweza kufanya hivyo kwa njia ya mtandao bila tabu nyingine yoyote bila kusahau bidhaa yao nyingine ya Usalama wa mtandao Internet Security .

Kwa haraka Avast 5.0 ni jibu la wale walio nunua AVG 9.0 free Edition , Pro pamoja na internet Security na hata wale walionunua Bidhaa ya Microsoft inayoitwa Microsoft Security Essentials , lakini hapa nitaongelea kidogo kuhusu Avast 5.0 kulinganisha na AVG 9.0.

Kwanza kabisa Tovuti ya Avast imebadilika vitu vingi sana kwa wale watu waliozoea kutembelea tovuti hii watakuwa wameona tofauti ya kuanzia rangi na mambo mengine mengi , mfano kwenye tovuti ya mwanzo ulitakiwa kuangalia sehemu ya updates tu na kwenda moja kwa moja kushusha updates za antivirus yako hii ya sasa hivi ni tofauti inabidi kwenda kwenye Linki ya support ndio utaona updates unazoweza kudownload .

Ukifika hapo unapata nafasi 2 za kudownload ambapo moja ni kwa ajili ya toleo lililo pita yaani 4.8 na update nyingine ni ya 5.0 , hii ni tofauti na Antivirus nyingi ambapo updates zote huwa kwenye file moja kwahiyo inasaidia sana hata kwa wale ambao hawajui wanatumia matoleo gani ya bidhaa husika , hii ipo kwenye AVG 9.0 hata Mcafee Virus Scan .

Unapo weka programu hii kwenye kompyuta yako pia haina njia ndefu na maelezo mengine kama ilivyo AVG , kwa mfano AVG unatakiwa kufunga baadhi ya kazi unazofanya kwa wakati huo au kama umefungua programu yoyote , kwenye AVAST 5.0 hutakiwi kufanya hivyo unaweza kuendelea na shuguli zako huku ukiendelea kuingiza kwenye komputa husika .

Pindi unapomaliza kuingiza kwenye kompyuta yako basi Avast Huanza kufanya kazi hapo hapo hii ni toleo la 5.0 tofauti na matoleo yaliyopita ambapo mtu ulilazimika kurestart computer yako ili iweze kuweka settings zingine kwenye komputa yako kwa ajili ya kufanya kazi na nzuri zaidi ni kwamba ile boot time scan bado iko kwenye toleo hili la AVAST .

Kompyuta yako ikiwa ina matatizo kwenye Saa yake au matatizo yoyote ya muda ujue utapata tatizo na Toleo hili la Avast , hii ni tofauti sana AVG ambapo unaweza kuidanganya kwa kutumia Tarehe na ukaweka updates za nyuma ikakubali kufanya hivyo , ukijaribu kufanya uwongo kwenye AVAST haitofanyakazi .

Kwa upande wa wepesi na kasi ya kuscan files kwenye kompyuta au vifaa vyake vingine Avast imekuwa na kasi zaidi kwa wakati huu , naweza kusema kushinda antivirus zingine zote nilizowahi kutumia kwa kipindi cha miaka 4 iliyopita , hata hivyo huko tunapoenda kampuni zinazotengeneza bidhaa hizi zinatakiwa kuhakikisha zinakuwa na bidhaa ambazo ni nyepesi katika utendaji wa kazi mbalimbali zinazohusu usalama na ulinzi wa komputa au vifaa vinavyochomekwa kwenye kompyuta hizo

Kwenye masuala ya Licence , unapotumia AVG 9.0 Pro au IS kama ina matatizo kwenye leseni yake yaani bandia basi ina sehemu ya kukuruhusu kurudisha antivirus yako kwenda kwenye toleo la Bure ambalo kuna baadhi ya vitu unaweza kuvikosa kwenye toleo hilo , Kwa AVG kupitia tovuti yao inasehemu ya kuweza kurudisha Leseni yako kama ulipoteza au komputa yako ilipata tatizo ukapoteza Leseni hiyo .

Na mwisho ni kuhusu uwezo wake wa kugundua tabia za baadhi ya programu zako ndani ya kompyuta na kukupa taarifa pale programu hizo zinapofanya kazi kinyume , ingawa hii inaweza kutumika na wahalifu kwa siku za mbele na kuweza kuwadanganya watu pamoja na programu yenyewe .

Hayo ndio maelezo mafupi kuhusu AVAST 9.0 ,mengine unaweza kusoma kupitia tovuti yao au kusoma Mada mbalimbali zinazohusu bidhaa hii lakini ni nzuri inafaa sana haswa kwa watu wenye kompyuta zilizokuwa na spects ndogo .
 
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
7,239
Likes
333
Points
180
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2009
7,239 333 180
sichagui yoyote, I better go to kaspersky
 
Original Pastor

Original Pastor

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2007
Messages
1,256
Likes
12
Points
135
Original Pastor

Original Pastor

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2007
1,256 12 135
SHY wewe ni mjanja unataka computer zetu zidedi ili upate tenda hivi hii avast what next after one month ahead??? si inageuka Virus kwani wewe hujui yaani Muzungu akupe kitu bureeeeee!!! labda angekuwa Mwafrika ana roho ya Binadamu je wewe umeshatumia hii zaidi ya Mwezi hii bidhaa yako??? na Unasemaga hutaki ma paires sasa wewe unatuletea nini??? Futa hiyo thread yako tafuta ingine . Mimi nimepata antvirus ingine ipo nimenunua for Users 100 nitawatumia watakao wahi watakuwa wamepata baada ya hapo license yako inaisha baada ya mwaka mmoja.
 
Kang

Kang

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2008
Messages
5,310
Likes
819
Points
280
Kang

Kang

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2008
5,310 819 280
Microsoft Security Essentials > All that.
 

Forum statistics

Threads 1,250,505
Members 481,371
Posts 29,736,026