Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,322
- 33,126
Habari kutoka kwa mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakupenda jina lake liandikwe, zilitaja kisa cha mauji hayo kuwa ni hasira za wananchi waliomtuhumu kijana huyo kwa kupanga njama za kutaka kuiba katika nyumba ya mzee mmoja aliyetajwa kwa jina la Rajabu.
Ilielezwa kwamba kabla ya kuuawa, marehemu akiwa na wenzake watano walionekana kuzengea vitu (havikutajwa) vya mzee huyo kwa lengo la kuviiba.
Kwa bahati wakati wanataka kuiba mwenye nyumba aliwaona akapiga kelele za mwizi wananchi wakatoka na silaha za jadi, yule kijana akawa anakimbilia kanisani, alipofikia kiwanjani kabla hajaingia ndani wakamkamata, wakampiga na kumuua, alisema shuhuda huyo.
Katika mauaji hao wananchi walimkata marehemu kwa panga ambapo picha za tukio hilo zinatisha hivyo tumeshindwa kuzichapisha gazetini kutokana na sababu za kimaadili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Bw. Emmanuel Kandihabi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Source: Gazeti la Amani